Sheikh Ponda akamatwa Dar!

Sabato masalia

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2011
Posts
228
Reaction score
134
Yule 'Mwanaharakati' maarufu wa dini ya kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda amekamatwa na polisi usiku huu akiwa katika msikiti wa Temeke Tungi

UPDATES:
Ni taarifa za kweli na aliwindwa kwa siku tatu ili akamatwe katika mazingira salama yasiyoweza kuibua mtafaruku na huu ni mwanzo, huenda hatua kubwa zaidi zitachukuliwa kwa Redio Imaan.
- Ponda alikamatwa mida ya saa 5 usiku muda ambao unahisiwa kuwa sawa na ambao mwenzake Sheikh Farid wa Uamsho (Zanzibar) anadaiwa kupotea; unaweza kufuatilia - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wa-uamsho-atekwa-nyara-visiwani-zanzibar.html
- Wafuasi wa Ponda wameanza purukushani, unaweza kusoma - https://www.jamiiforums.com/habari-...si-wa-sheikh-ponda-waanzisha-purukushani.html

KAULI YA KAMANDA KOVA:
 
Sasa isiwe akamatwe kwa sababu wameamua kumtoa kafara; Ponda hajaanza leo kusema anayoyasema. Kama muda wote (miaka yote) wameweza kumvumilia imekuwaje leo waamke na kusema wanamkamata?

Kama kosa ni yale ya Mbagala au anayoyasema ukweli ni kuwa itakuwa ni kumuonea! Kosa ni la serikali inayotawala. Ukiacha mlango wazi kwenye zizi kila sikuw watu wanakuambia chui ataingia na kula mbuzi nawe ukapuuzia siku chui akiingia na kula utalaumu zizi kwanini halikufungwa?
 
Ni taarifa za kweli na aliwindwa kwa siku tatu ili akamatwe katika mazingira salama yasiyoweza kuibua mtafaruku na huu ni mwanzo, huenda hatua kubwa zaidi zitachukuliwa kwa Redio Imani.

Nini kiliizuia serikali kuchukua hatua kubwa kwa radio Imani siku za nyuma? Bado naamni serikali adilifu ingekwisha shughulikia tatizo na chuki za kidini muda mrefu nyuma.
 
Yote 9 hii habari iwe ni kweli na kama ni kweli wasitufanye watoto wadogo kwa kumwachia bila vigezo vya kueleweka! Anastahili kujibu tuhuma nyingi sana na awajibishwe! Tumechoka na maneno na vitendo vyake vilivyojaa chorus!
 
Mzee Mwanakijiji

Labda ya mbagala ndio yame waamsha huu sio utani tena, na ni watu gani anaowaamsha kwa fikra zake ambazo hazifai.

Let it be true na anyongwe
 
Last edited by a moderator:
Hapo sijakupata mwanakijiji. Kwa hiyo kama kwa muda mrefu ulikuwa unaacha mlango wa zizi wazi kwa kuamini kwamba chui hataingia, lakini ikatokea siku moja akaingia hutachukua hatua? Kinachoonekana ni kwamba serikali ilikuwa inampuuza kwa muda mrefu. Sasa imeanza kuona matunda ya kauli za huyu mhuni, na imechukua hatua.

Kama ni kwa mfano wako basi, serikali inachukua hatu za kufunga zizi ili huyu chui asirudi tena. Ninaungana na wale wanaosema polisi wasiishia kwa Ponda tu, bali waende mbali zaidi kwa kuifuta kabisa Radio Iman na gazeti la Al-nuur. Hivi ni virusi vibaya sana kwa mstakabali wa amani yetu. Sioni kibaya kwa serikali kuchukua hatua hiyo.
 
ni kweli wamemkamata maana ni janga kwa taifa letu akati yeye sio mtz...mbona sheikh mkuu hana reasons kama zake...a behave bwana, hatutaki kuwa kama somalia na vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…