Sheikh Mattaka: BAKWATA ndio wengi kesho misikiti zaidi ya 300 Dar itatumika kwa ajili ya swala ya Idd

Kwa hiyo Mungu wao hawa wote wa leo na kesho anaitwa "MWEZI" siyo?

Duuuh, hii Kali. Ngoja sisi tupumzike kwa sikukuu za wanaoongozwa na MUNGU MWEZI...!

Na kwa upande mwingine, aliyeumba MWEZI akiamua kuuzuia usijitokeze mpaka mwakani maana yake hakuna sikukuu na malumbano ya wanaosubiri MWEZI yatawaka moto mkubwa zaidi...
Acha kukashifu imani za wenzio UMBWA WEWE
 
Natamani mada kama hizi zisingejadilwa humu,
Enyi wasomi wa kiislamu itaneni mujadili ili mupate msimamo mmoja kama nchi (japo ni ngumu lakini inawezekana na itapendeza) muondoshe aibu hizi.

Fikirieni jambo hili kujadiliwa na wasiokuwa waislamu na nyie kila mmoja anavutia kwake mwishowe wanaishia kukebehi dini yetu.
Whats a mess!!!
Ukikaa na bakwata mkajadili wenzenu wakitoka wanaenda ccm kujadili upya
 
Nimesema wawe na ushirikiano, ushirikiano sio kuwa na group la whatsapp shekhe! Ushirikiano ninaomaanisha wawe wanapashana habari. Ni zaidi ya group la whatsap, jwani hata wanaweza kuanzisha forums, vikao mbali mbali pia kujadili mambo yanayowahusu waislam.
Hawajaamua lakini wanaweza na ni rahisi sana
 
Yemen na Saudia ni majirani wa mfano huo uliyoutoa lakini mwezi ukiandama Yemen Saudia haufuati.

Unasemaje katika hili?

Ajabu huyu huyu anayesema mwezi ni 1 popote ufuatwe, mwezi huu huu 1 ukipatwa hata huko wanapofuata kwenye vipindi vya radhamani na Eidi hawaufuati; Kwa maana hawaswali swala ya kupatwa kwa mwezi.
Suala la mwezi muandamo ni ngumu kulitatua kwa kutumia hoja ambazo zipo nje ya mwezi muandamo.

Kupatwa kwa mwezi ni jambo kando hasa na mwezi muandamo.

Ni mifano tofauti kwa sababu kupatwa kwa mwezi mwezi tayari upo pale siku nyingi tuu baada ya kuandama.

Haiji kutumia mfano huu kama hoja kwa sababu unalinganisha mambo tofauti.

Ni sawa na mtu analinganisha sala na mwezi muandamo.

Jana mufti alitangaza kuwa hapo comoro mwezi haukuonekana.

Sasa mkuu unadhani sisi na comoro mwezi wetu ni mmoja kwa mujibu wa mufti mpaka akatumia comoro kama reference ?

Lakini pia kenya na tanzania unadhani mwezi wetu ni mmoja ?
 
Lakini mbona funga ya beidh hamfuati mwezi huo wa kimataifa mnaousema? Kwa hili nalo pia wanajua wenyewe!
Mkuu mbona hili jambo wengi tunafuata kalenda iliyotangulia ndo tunafunga masiku meupe ?

Ama kuna watu unaishi nao huko pengine wanafanya kama ulivyojengea hoja hiyo haifanyi kuwa wote tunafanya kama wao hivyo sio sahihi kuifanya hoja kwa wote.

Sisi tunafata kalenda iliyotangulia hata masiku meupe tjnaingia humo sisemi kama hawapo wanaofata ya hapa.

Wapo pia lakini hawabebi sisi tusiofata.

Nimeona hili nikujulishe mkuu
 
Watakuwa wamemkera tu, ila Mataka ni msomi mzuri sana wa elimu dunia
Tatizo la wakristo wanajua msomi wa dini ya kiislamu hana uelewa wa mambo ya kidunia,wakati watu wanasoma fani mbalimbali kama...mantik(logic) na fani zingine humo humo katika elimu ya dini ya kiislamu...mnatakiwa msiwadharau masheikh kuna waliohitimu katika vyuo vikuu vikongwe kama azhar shariff wanafundisha dini na fani zingine...kuna masheikh na pia ni mainjinia,madaktari,n.k.
 
Hebu tutajie Sheikh wa hapa nchini ambaye ni Mhandisi, Mwanasheria au Daktari hata wa kusomea (PHd holder).

Nitajie wawili tu.
 
Sheikh Mattaka anasema mwandamo wa mwezi Duniani kote hutangazwa na mamlaka husika na hapa Tanzania mamlaka hiyo ni BAKWATA.

Mattaka anasema Mufti hutangaza mfungo au mfunguo baada ya mwezi kuonekana na kamati ya muandamo wa mwezi kujiridhisha.

Sheikh Mattaka, anasema BAKWATA hufuatilia pia muandamo wa mwezi kwa nchi za Zanzibar na Kenya, lakini huko pia mamlaka husika zimesema mwezi haujaandama.

Hata hivyo Sheikh anasema Waislamu watakaoswali Eid kesho ndio wengi na hapa Dar es Salaam waumini watajaa misikiti zaidi ya 300 tofauti na hawa wanaoswalia viwanjani leo ambao hutumia viwanja viwili vitatu tu.

Chanzo: Channel Ten

wengi kwa sababu mmepiga marufuku tv imaan kujitangazia idd waruhusu idd yao ya ansur sunna waitangaze kwenye ma tv uone
 
Uislamu unabaki kwa elimu kwa maana Dini ni elimu na hiyo (hii) elimu ndiyo dini.

Hivyo basi Uislam ukamtaka mtu kutokuingia kwenye masuala bila ya elimu nayo na kutoka kwenye masuala bila kuwa na elimu nayo! Tukatanguliziwa nukuu kuwa elimu kabla ya kunena na kutenda.

Umeandika mengi kuhusu kadhia ya mwezi. Narudi kwenye madhumuni yangu; Umesoma dini?
Unakumbuka Miiraj ilikuwa ni siku gani? Kama hufahamu katafute Miiraj ilikuwa siku gani then uje na jibu hapa Eid ni lini. Elimu ya dini ni pana zaidi ya unavyofikiria. Na mwaka wa Hijiriyya kila mwaka unapungua kwa siku 11 dhidi ya Miladiyya. Chukua hiyo.
Hii JF wengi wengi hatuoneshi uhalisia wetu kwa kujificha nyuma ya keyboard.
Na pia kwenye upungufu wa siku 11, jaribu kupitia mwaka jana mwandamo wa mwezi ulikuwa ni tar ngapi then relate na upungufu wa siku 11 ndipo uje na jibu
Elimu ya dini ni pana sana, Pia subiria leo jioni INSHALLAH, kisha uangalie mwezi uje na jibu je ni mwezi mosi au mwezi pili.
 
Katika historia leo kwa mara ya kwanza nimetizama swala ya Eid mnaz mmoja kwa kweli kabisa imedoda sana mpaka waziri mkuu anaomba sana watu wajitokeze kwenye baraza la Eid wakifanya mchezo wataanza kuwachukuwa watu kwa magari kujaza. Hili fundisho kwa Bakwata na kwa kuwa wameanza na hizi kauli sisi wengi tutajaza basi ujue limewapata, kwani nani alisema haya mashindano ya kujaza watu kama Chadema na CCM. kila miaka inavyokwenda Bakwata wanapoteza wafuasi kuliko hao wapinzani wao, wale walianza wachache lakini kila mwaka wanakusanya vijiji. Bakwata hawana mamlaka yoyote na baada kuona mwezi jana utasema jua ni wazi mwezi wa juzi sasa wamenza defensive statement. acheni kutugawa PM anainuka anaomba jamani mje kwa wingi baraza la Eid ujuwe something wrong.
 
Mimi nadhani kundoa ubishi huu, Jana tumeuwona mwezi mimi nimeuwona. Je ni kweli ule mwezi wa jana? tuongee haki kwa kugopa Allah. ile mwezi wa juzi kwa maoni yangu. mwezi wa siku ya kwanza unakuwa mdogo sana na kama macho yako zio mazuri unaweza kuonyeshwa kwa kidole na ukahangaika kuona. wa jana ni mkubwa toa maoni ulichoona jana basi wewe mwenyewe sio kuambiwa.
 
NAWAKUBALI SANA NDUGU ZETU WAISLAM WANAOHESABU SIKU BADALA YA KUSUBIRI KUONA MWEZI KWA MACHO YAO.

NIONAVYO BAKWATA NI CHOMBO au WING mojawapo ya Serikali, haipo kwa ajili ya maslahi waislamu.
Science imekuwa watu wanaona tusiyoyaona leo, wanasema kabisa chance ya kuonekana mwezi tarehe hii ndogo ila saa na dakika hii utatoka na kupotea kwa seconds elimu imekuwa lakini kuna watu wanataka tuishi kama miaka 600 nyuma.
 
nimeona mwezi mkubwa jamani
Suala la mwezi mkubwa sio ishu na halina shida kabisa.

Mimi nimekula jana na kuna watu walinilalamikia kuwa ule mwezi wa jana sio wa leo na wao wanafungua kesho,sikutumia upenyo huo kuwavuta kwenye msimamo wangu wa mwezi popote,badala yake nikawaambia tu kuwa ule mwezi hapa tulipo sio wa jana kwa sababu hyo jana haukuonekana.

Almuhimu haya mas'ala sio ya kuvutana,tukiendelea kuvutana jambo litakuwa kubwa.

Lakini tukichukuliana uzuri na kupeana nyudhuru jambo hhili litaisha lenyewe tu.
 
Nakubaliana na wewe kuna baadhi ya family yangu pia hawakula jana lakini nikajibu kwa uzuri sababu nilihisi kama wanataka kuchokosa hisia zangu lakini busara ikaja hivi nikawajibu hakuna shida ukila Ijumaa hata ukitaka Jumamosi shauri yenu wala sio issue wakakaa kimya ni kama walitaka kuona nitajibu nini msg yao lakini nikawa soft tu baada ya msg yangu wakaa kimya tu. Ila nimetoa ushuhuda wangu mwezi jana nimuona mkubwa sana kwa haki kabisa.
 
Sheikh Mattaka anasema mwandamo wa mwezi Duniani kote hutangazwa na mamlaka husika na hapa Tanzania mamlaka hiyo ni BAKWATA.

Mattaka anasema Mufti hutangaza mfungo au mfunguo baada ya mwezi kuonekana na kamati ya muandamo wa mwezi kujiridhisha.

Sheikh Mattaka, anasema BAKWATA hufuatilia pia muandamo wa mwezi kwa nchi za Zanzibar na Kenya, lakini huko pia mamlaka husika zimesema mwezi haujaandama.

Hata hivyo Sheikh anasema Waislamu watakaoswali Eid kesho ndio wengi na hapa Dar es Salaam waumini watajaa misikiti zaidi ya 300 tofauti na hawa wanaoswalia viwanjani leo ambao hutumia viwanja viwili vitatu tu.

Chanzo: Channel Ten
Hivi lile jukwaa la dini lilienda wapi?
 
Back
Top Bottom