Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Viongozi wa dini mkoani Katavi wamekutana katika kikao maalum kujadili hali ya amani na mshikamano wa Watanzania, wakitoa wito kwa wananchi kuendelea kudumisha umoja na amani, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Wakizungumza kwa pamoja, viongozi hao wamesema kila Mtanzania ana jukumu la kuilinda tunu ya amani iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakisisitiza kuwa uchaguzi usiwe chanzo cha mgawanyiko au vurugu.
“Amani ndiyo nguzo ya maendeleo. Hakuna maendeleo bila amani, hivyo tuilinde kwa maneno na matendo yetu,” amesema Sheikh Kakulukulu.