M-bongotz
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,734
- 405
Yule kiongozi wa kikundi cha UAMSHO Z'bar na wenzake leo wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi na kusababisha vurugu ambapo hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amewanyima dhamana mpaka Alhamisi kwani kuna vipengele ambavyo mawakili wao walivipinga kikiwepo cha kila mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja wao ni lazima awe mtumishi wa serikali.
Wao wanapinga kwamba serikali ndio iliyowashitaki sasa iweje waambiwe walete mdhamini ambaye ni mtumishi wa Serikali.
Hakimu atatoa maamuzi ya hoja hizo Alhamis hivyo viongozi wa UAMSHO wamekwenda rumande.
Wao wanapinga kwamba serikali ndio iliyowashitaki sasa iweje waambiwe walete mdhamini ambaye ni mtumishi wa Serikali.
Hakimu atatoa maamuzi ya hoja hizo Alhamis hivyo viongozi wa UAMSHO wamekwenda rumande.
Kesi imefikishwa leo Mahakama kuu ya Zanzibar na Imeahirishwa hadi Alhamisi.
Mashtaka yanayomkabili Sheikh Farid na wenzake;
KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI
KUSABABISHA VURUGU ZILIZOTOKEA MIEZI MIWILI NYUMA.
Mawakili wake walilamika kuwa upande wa serikali umeshindwa kuwapatia order paper ya washtakiwa.
Vile vile walilalamikia Jinsi Jeshi la polisi wanavovunja sheria kwa Kuwazuwia Mawakili hao kuonana na wateja wao ambao jambo ambali=o ni kinyume cha sheria.
Ugumu wa Dhamana:
Mawakili imetaka mahakama kuondoa baadhi ya vipengele vya DHAMANA ikiwemo kuwepo kwa barua ya sheha kwani masheha wakifatwa hujifanya wana vikao na hawataki kutoa.
Vile vile kuondoa kipengele cha kuwepo mdhamini mmoja ambae ni mfanyakazi wa serikali. Wanasheria hao wamesema haiwezekani ikawa serikali ndio inawashataki halafu lazima awepo mdhamini ambae anafanya kazi serikalini.
Baada ya makubaliano hayo Jaji ambae aliepangiwa kesi hiyo amesema kutokana na ugumu wa kesi hiyo ameiahirisha mpaka siku ya ALHAMISI wiki hii.