Sheikh Alhad Mussa Salum(Dar) ashauri Viongozi wa dini kuacha siasa misikitini, kanisani

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imefanya kazi nzuri na kubwa ikiwemo ya kukomesha ufisadi, rushwa, unyonyaji, nidhamu kazini, kudhibiti mapato na mengine, huku ikipiga hatua katika kuongeza kasi ya maendeleo, jambo alilosema ni vyema kama litapokewa kama sehemu ya kujivunia kwa viongozi hao na taifa kwa ujumla.

Kwa hiyo ukisifia utendaji kazi wa raisi unakuwa hufanyi siasa, ila ukiukosoa ndo hapo siasa inakuwa imefanyika..! Ust'adh anajidhalilisha huyu..
 
MWENYEKITI wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Shehe wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum amewataka viongozi wa kidini kuacha siasa za chuki dhidi ya viongozi wa kitaifa katika majukwaa yao ya ibada.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Shehe Alhad alisema siku za hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya viongozi wa kidini kutoa kauli mbalimbali zenye lengo la kuwachonganisha wananchi na viongozi wakuu wa kitaifa akiwemo Rais John Magufuli, suala alilodai halina budi kukemewa kwa kuwa sio mahali pake.

Alisema viongozi wa kidini wana nafasi kubwa katika jamii na kutokana na nafasi hizo pia wanazo fursa mbalimbali za kuwasilisha mawazo yao bila tatizo lolote kwa kufuata utaratibu unaoeleweka, ila siyo kwa kusimama mbele ya waumini wao wakati wa ibada na kutoa kauli za kisiasa zinazolenga kuvuruga amani.

“Sisi viongozi wa kidini tumepewa wigo mkubwa sana wa kufikisha mawazo yetu, siyo kwamba tunakatazwa kuikosoa serikali kwa jambo lolote…hapana, hiyo ni haki yetu ila hapa ni utaratibu upi tunautumia kufikisha kile tunachokiona hakiendi sawa,” alisema Shehe Alhad.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imefanya kazi nzuri na kubwa ikiwemo ya kukomesha ufisadi, rushwa, unyonyaji, nidhamu kazini, kudhibiti mapato na mengine, huku ikipiga hatua katika kuongeza kasi ya maendeleo, jambo alilosema ni vyema kama litapokewa kama sehemu ya kujivunia kwa viongozi hao na taifa kwa ujumla.

Alisema tangu serikali hiyo iingie madarakani miaka miwili iliyopita, Rais Magufuli pamoja na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wamekuwa mstari wa mbele kutembelea makanisa mbalimbali na misikiti na kuzungumza na waumini pamoja na viongozi wao, na kuhoji iweje sasa kwa viongozi hao wanageuka tena na kuanza kuwavuruga.

“Utaratibu sahihi upo na wa nidhamu kwa viongozi wetu ndiyo pekee unaowezesha kulinda amani na utulivu kwa taifa hili, lakini siyo kwa kukosoana kwenye nia ya kuchochea waumini wachukie viongozi wao pasipo sababu, leo kiongozi wa dini anasimama na kukosoa, kesho msemaji wa serikali akisimama na kujibu mwisho wa siku linakuwa siyo jambo la busara, kikubwa ni kwa viongozi wenzangu wa dini kuwa na staha,” aliongeza.

Aidha, kuelekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, Shehe Alhad amewaomba Watanzania wote pasina kujali itikadi zao za kidini, kuzidi kuliombea Taifa ili lizidi kwenda katika njia sahihi kama ambavyo dalili zimejionesha ndani ya kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismasi na katika miaka miwili chini ya Rais Magufuli. Alisema ushirikiano baina ya wananchi na viongozi wao wa ngazi zote ndiyo jambo pekee litakalowasaidia kuvuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika njia sahihi za mafanikio.
Embu afungue mdomo kwanza amtake huyu Sheikh anae dai jerusalemu ni halali ya Israeli
7706d6480105d043d9dd755ff5b19d32.jpg
awache siasa ndio nitajua sio Shehee ubwa ubwa .
 
Wewe ndio umepotoka Hujui ata kuwa Dini si lolote si chochote, Ziletwa kwa nia ya kututawala mimi hapa pia sina Dini Ila Popote pale naweza kuunga na Watanzania wenzangu na Kufanya ibada Iwe kanisani au msikitini Sina ule udini udini na misimamo mikali ambayo ni Ujinga tu.
Dini ni nini? Na ziko ngapi mkuu?
 
Dini ni nini? Na ziko ngapi mkuu?
Dini ni Ways of people life ni kama utamaduni wa Watu zipo aina nyingi sana za Dini kutegemea na jamii, Jamii zilizokuwa Firm na Bold ndio zimejitahdi kutapakaza tamaduni zao maeneo mengi, mfano wa Tamaduni hizo ni Uislamu na Ukiristo na budhasim kwa mbali. Jamii nyingi zili ignore tamaduni zao either kwa kuwa na mapungufu or kwa kuzidiwa akili na Wanatamaduni wengine.
 
Dini ni Ways of people life ni kama utamaduni wa Watu zipo aina nyingi sana za Dini kutegemea na jamii, Jamii zilizokuwa Firm na Bold ndio zimejitahdi kutapakaza tamaduni zao maeneo mengi, mfano wa Tamaduni hizo ni Uislamu na Ukiristo na budhasim kwa mbali. Jamii nyingi zili ignore tamaduni either kwa kuwa na mapungufu or kwa kuzidiwa akili na Wanatamaduni wengine.
Kwahiyo zipo 3 tu mkuu?
 
Siasa za chuki nani katoa siasa za chuki aisee mbona huyu jamaa anataka kuniangusha wakati ndiye niliyekuwa namuona kichwani yupo sawa sawa?yale maneno yalikuwa yanafafanuliwa kutoka Bible hakusimama tu mtu akayatoa kichwani mwake.ule ulikuwa ufafanuzi tu ila ujumbe wote ulishaandikwa kabla hata hiki kipande cha ardhi haijajulikana kama kitakuja kuitwa Tanzania.
 
Basi zisome zote uzielewe zote mkuu.
Mkuu kuna ambazo zinazunguka wana jamii wenzangu au Watanzania hizo nazifahamu basics zao mfano wa Christian au muslim mimi sio miongoni wa mdini niko neutral na siwezi Kumchukia mtanzania mwenzangu kisa tu imani ambayo haina muda mrefu tangu iletwe, Ukiristo na uislamu umetukuta hapa Tanzania tukiwa wamoja tu kwanini leo vitugombanishe
 
Back
Top Bottom