Sheikh Alhad Mussa Salum(Dar) ashauri Viongozi wa dini kuacha siasa misikitini, kanisani

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Points
2,000

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 2,000
MWENYEKITI wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Shehe wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum amewataka viongozi wa kidini kuacha siasa za chuki dhidi ya viongozi wa kitaifa katika majukwaa yao ya ibada.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Shehe Alhad alisema siku za hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya viongozi wa kidini kutoa kauli mbalimbali zenye lengo la kuwachonganisha wananchi na viongozi wakuu wa kitaifa akiwemo Rais John Magufuli, suala alilodai halina budi kukemewa kwa kuwa sio mahali pake.

Alisema viongozi wa kidini wana nafasi kubwa katika jamii na kutokana na nafasi hizo pia wanazo fursa mbalimbali za kuwasilisha mawazo yao bila tatizo lolote kwa kufuata utaratibu unaoeleweka, ila siyo kwa kusimama mbele ya waumini wao wakati wa ibada na kutoa kauli za kisiasa zinazolenga kuvuruga amani.

“Sisi viongozi wa kidini tumepewa wigo mkubwa sana wa kufikisha mawazo yetu, siyo kwamba tunakatazwa kuikosoa serikali kwa jambo lolote…hapana, hiyo ni haki yetu ila hapa ni utaratibu upi tunautumia kufikisha kile tunachokiona hakiendi sawa,” alisema Shehe Alhad.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imefanya kazi nzuri na kubwa ikiwemo ya kukomesha ufisadi, rushwa, unyonyaji, nidhamu kazini, kudhibiti mapato na mengine, huku ikipiga hatua katika kuongeza kasi ya maendeleo, jambo alilosema ni vyema kama litapokewa kama sehemu ya kujivunia kwa viongozi hao na taifa kwa ujumla.

Alisema tangu serikali hiyo iingie madarakani miaka miwili iliyopita, Rais Magufuli pamoja na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wamekuwa mstari wa mbele kutembelea makanisa mbalimbali na misikiti na kuzungumza na waumini pamoja na viongozi wao, na kuhoji iweje sasa kwa viongozi hao wanageuka tena na kuanza kuwavuruga.

“Utaratibu sahihi upo na wa nidhamu kwa viongozi wetu ndiyo pekee unaowezesha kulinda amani na utulivu kwa taifa hili, lakini siyo kwa kukosoana kwenye nia ya kuchochea waumini wachukie viongozi wao pasipo sababu, leo kiongozi wa dini anasimama na kukosoa, kesho msemaji wa serikali akisimama na kujibu mwisho wa siku linakuwa siyo jambo la busara, kikubwa ni kwa viongozi wenzangu wa dini kuwa na staha,” aliongeza.

Aidha, kuelekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, Shehe Alhad amewaomba Watanzania wote pasina kujali itikadi zao za kidini, kuzidi kuliombea Taifa ili lizidi kwenda katika njia sahihi kama ambavyo dalili zimejionesha ndani ya kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismasi na katika miaka miwili chini ya Rais Magufuli. Alisema ushirikiano baina ya wananchi na viongozi wao wa ngazi zote ndiyo jambo pekee litakalowasaidia kuvuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika njia sahihi za mafanikio.
 

jumamwaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
236
Points
250

jumamwaki

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
236 250
:D:D:D:D Amenifurahisha kuchomekea sindano ya Ganzi kwa watawala ili wasimbughudhi kaweka mistari ya kufagilia wanaopenda kufagiliwa tu hapo huwezi shangaaa ni majukwaa yale yale yanayopingwa ila ukiingiza mistari kadhaa ya kusifia watawala basi wazee wale wenye nyota nyota hutua silaha chini wakiendelea kukusikiliza kama itajitokeza mistari ya kukrash :D:D:D:D:D:D:D dah naipenda sana Nchi yangu,Naipenda sana Jamii forums
 

malisoka

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2012
Messages
1,818
Points
2,000

malisoka

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2012
1,818 2,000
Sijui ni kusahau au ni kwa makusudi kwa kuwa mkuu ameambiwa atubu madhambi yake?

Nina Uhakika Mkuu ni Mkatoliki na kila jumapili huwa tunatubu!


Pili, Moja ya kazi ya kueneza dini ni

Kwanza: Kufundisha watu maadili mazuri (pamoja nakuheshimu serikali iliyopo)

Pili: Kuonya, Kukemea, Mienendo mibaya na maovu yanayofanyika.

Tatu: Kuwafanya watu waishi maisha yanayo mpendeza Mungu bila kujali ni rais au waziri au diwani au Mbunge.


Sasa Mimi ninajiuliza Huyu Mkuu wetu Ni MUNGU kwamba hatakiwi kuambiwa na kurekebishwa.

Mwalimu Nyerere alikuwa akionywa na hata kwenye hotuba zake ameonyesha kwamba wakati mwingine viongozi wa dini walikuwa wakimkosoa, na hakuwatukana na wala hakuwatishia kufunga makanisa yao.

Shime, hakuna aliye mkuu kama Mungu aliye juu, Mungu mmoja aliyeumba mbingu na nchi. wote tuliobaki ni Uchi, masikini, Ovyo, takataka.
 

Kambaku

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2011
Messages
2,929
Points
2,000

Kambaku

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2011
2,929 2,000
Na wao wana siasa wanapotaka kuombewa je mbona wanachanganya na dini huo usiasa wao?

Hivi hatukuona mmoja hapa aliombwa vyeti akakimbilia kanisani kuomba msaada tena kwa machozi kabisa? Kwanini sasa alipeleka malalamiko yake ya kisiasa kanisani?

Yule kaka mkubwa mara ngapi tumeona anaomba watu wa Mungu wamuombee maana anapata shida sana katika siasa zake? Tena anatumia msemo huo huo 'mniombee sana', sasa sisi na viongozi wa dini tumuombee wapi kama sio kwa Mungu huyu huyu anaesisitiza kutubu dhambi mara kwa mara?

Polisi TZ, CCM na kaka mkubwa, hakuna binadamu asiyekosea na hakuna binadamu anayepata amani moyoni kama akitubu na kuamini kasamehewa dhambi zake. Viongozi wa dini kutukumbusha kutubu ni sehemu ya kazi zao.
 

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Messages
1,457
Points
2,000

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2016
1,457 2,000
Baada ya vyuma kukaza, makanisani hakuna sadaka, wachungaji wanahaha, kakobe analia na Rais, Walokole hawataki kusikia jina Magufuri. Ni balaaa

Kakobe tubu wewe, yule Nyoka madhabauni mwako ni wanini, husipokuwepo wewe mwingine hapandi madhabauni y??? tubu wewe
 

Gideone

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2017
Messages
509
Points
1,000

Gideone

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2017
509 1,000
Shehe alhad ameongea Vyema sana Hakuna kiongozi wa Dini atataka kuonana na Rais azuiwe kwa Muda mrefu Yani aki propose appointment within a short time anapewa nafasi, Uongozi Huu umewapa sana Heshima viongozi hawa wa dini bila kujali imani Ni Mara nyingi tunamuona Mhes JPM yuko na mashekhe pamoja na wachungaji na maskofu, Uhuni aliofanya kakobe ni wakukemea kabisa, Hakuna aliemzuia kuingia magogoni kuonana na Rais na kushauri
 

Gideone

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2017
Messages
509
Points
1,000

Gideone

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2017
509 1,000
nasikia huyu anaingiaga mpaka kanisani kusali. huyu sheikh alishapotoka kitambo....
Wewe ndio umepotoka Hujui ata kuwa Dini si lolote si chochote, Ziletwa kwa nia ya kututawala mimi hapa pia sina Dini Ila Popote pale naweza kuunga na Watanzania wenzangu na Kufanya ibada Iwe kanisani au msikitini Sina ule udini udini na misimamo mikali ambayo ni Ujinga tu.
 

Forum statistics

Threads 1,392,174
Members 528,565
Posts 34,100,930
Top