Shehe Yahaya angekuwepo ningemuuliza kama alikosea ama bado Iko vile vile

Shehe Yahaya angekuwepo ningemuuliza kama alikosea ama bado Iko vile vile

Lee Van free

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2024
Posts
2,246
Reaction score
7,111
Al maruhum Sheikh Yahaya Husein alitusimulia maono yake kua,baada ya JMK atakuja mtu mweusi,mchapa kazi halafu mchekeshaji.

Huyu atamaliza dakika arobaini na Tano za kwanza,lakini arobaini na Tano za pili hatazimaliza.

Katika maono yake alisema atakuja Malkia,na baada ya Malkia itaingia timu Mpya kabisa kutokea mbali huko.

Vitu ambayo ingemuuliza Al maruhum ni
Huyu malikia atacheza dakika zote tisini?

Maana naona Malkia ameshaanza kufanya jaramba licha ya timu moja kusema inapendekeza mabadiliko ya kanuni za ligi.

Nilimwamini yahya aliposema mchapakazi na mchekeshaji hata maliza zote tisini na hakumaliza.

Hivyo ningemuuliza ni wakati Gani malikia atawakabidhi kikombe timu nyingine?

Maana mchezaji wao na nahodha wao tayari kapewa kadi nyekundu,Sasa atawezaje kukabidhiwa kikombe wakati Yuko nje kwa kadi nyuekundu?

Ningemuuliza shehe,je
Hatamaliza Arobaini na Tano za kipindi Cha kwanza au baada ya za kipindi Cha pili?

Ukweli ningemuuliza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom