Share Nasi Hapa Cheat Code Ya Mazoezi Yoyote

Vyakula vifuatavyo vinaboost testosterone.

-Mbegu za maboga
-Tangawizi
-Tikiti maji
-Vyakula vyenye asili ya baharini mfano samaki, pweza, papa, ngisi n.k

Kwa anayefanya mazoezi (mwanaume) anapokula vyakula hivi hufanya mwili kuendelea kutoa hiyo homoni ambayo huhitajika na mwili katika kuutanua, nguvu na kukuza misuli.

Up side ni kua inakuongezea na libido.
 
mtoa mada mi nimeanza juzi kukimbia kuzuka uwanja bt mapaja yote yanauma hatari VIP hii hali unaweza isha baada ya siku ngapi
Endelea kufanya zoezi pataacha kuuma kwasababu mazoezi ni mazoea so pindi unavozid kulifanya ndivyo mwili unapoizoea hiyo hali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
d0ccf4ac584366359629e7e838ce83fd.jpg
34d037a4306c861bcad3236aecbdc4df.jpg
34279a9afa7889c53f40182bd05b786a.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya push ups hizi.

Pushap na magoti yamegusa chini. Seti tatu kila seti iwe na raundi 20.
Kupumzika kati ya seti ma seti iwe sekunde 20.

Pushap magoti juu ya benchi (unaweza ukaweka kitandani). Seti tatu kila seti moja iwe na raundi 20. Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 20.

Pushap miguu juu ya benchi. Seti tatu kila seti moja iwe na raundi 20. Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 20.

Pushap za kawaida. Seti 3, raundi 20, kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 20.
Ila kupumzika kwako usitoke kwenye mkao wako wa pushap, utabaki umeganda hivyo hivyo sekunde 20 za kupumzika zikiisha unaanza tena.

Halafu njoo na feedback
 
niliwahi kufanya hii ya kunyanyuka na vitu vizito baada ya muda nikaanza kuhisi kiti kama mshipa kwenye scrotum(testis)
Inaonekana ulikua unapiga squats, pia inaonyesha ulikua unatumia uzito mkubwa mno.
Kama uzito ulikua ni saizi yako basi ulikua haukai kwenye mkao unaotakiwa wa squats.
Au ulikua unaenda raundi nyingi kushinda uwezo wako.

Hua inashauriwa kitu kizito mfano beseni la maji tukitaka kulinyanyua tusilinyanyue huku tumeinama badala take tuchuchumae ili kuepuka tatizo kama hilo.

Haya niliyoyaweka hapa unakua unanyanyua mwili wako mwenyewe na kwa mkao wake hayawezi kukusababishia mshipa.
 
castr nina siku nne natumia stendi ya push up nipe hasara na faida tafadhali
Kama nakumbuka vizuri stand ulishanionyesha kwenye uzi fulani hivi.
Kama ni zile mimi hua situmi zile, kuna zingine hua natumia.

Hua natumia nikiwa nataka kukigawa kifua, yaani kuuleta ule mstari wa katikati.
Faida yake ni kwamba ina ufanisi mkubwa katika kutimiza hilo.

Push ups zote hasara zake ni kama usipokaa vizuri kupata maumivu ya maungio ya mikono au kushtua mikono
 
Kitu chochote kizito, hata beseni la maji, ukiwa unanyanyua bila mkao stahiki utapata ngiri.

Katika mazoezi zoezi ambalo linaweza kukupa ngiri ni squats, hivyo kifua na mengine hayana athari hiyo.
dah mkuu castr kumbe squat yaweza kuleta ngiri dah me wakati fulani huwa napata maumivu ya scrotum inabidi nipunguze squat au niache kabisa
 
dah mkuu castr kumbe squat yaweza kuleta ngiri dah me wakati fulani huwa napata maumivu ya scrotum inabidi nipunguze squat au niache kabisa
Angalia uzito umaotumia, idadi ya reps na kama hua unakaa jinsi squat inavyotakiwa kukaa ukiwa unaifanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom