Share experience kama ulishawai kuuzwa na mwanamke wa mtandao Badoo,Facebook, insta n.k

TADPOLE

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
2,800
9,041
Siti ya Nyuma kabisa kwenye Costa ya Kibamba-Mwenge alikuwepo Mtu mmoja hivi,.a man with a very serious face,komwe la ukoo, akiwa amevalia Tshirt ya njano iliyochorwa Cheni kifuani, halafu kichwani ana kipilipili kilichokolea easy wave,....kwa kweli mtu huyo si Mwingine bali ni MIMI

Hapa ndani ya Gari akili yangu yote ilikuwa kwa Asunta Lovelicious,binti mrembo niliyemuona Instagram, kisha tukahamia Snap Chat kabla kupanga Appointment kupitia Watsapp...tafadhali Dereva tanua njia tuwahi nahitajika Best Bite Namanga!, " taimu iz makangabilite

Sasa wakati tumefika Kimara Stop Over kuna Mama mmoja wa Makamo hivi aliyekuwa amesimama ndani ya Daladala aliomba nimsaidie mtoto,,..nami nikamsaidia

MIMI: Halafu Mama yangu unafanana sana na yule Babu aliyeigiza filamu ya 'The god must be crazy"
YEYE :Kweli ee, Asante Mwanangu, wengi wanasema hivyo!..

Basi wakati bado tupo kwenye Foleni ghafla ndani ya gari kukaibuka harufu Mbaya sana,...abiria wote wakafungua vioo kuchungulia nje kama kuna Gari ya taka (BUDEGE) tulikodoa macho bila mafanikio!, hiyo gari haikuwepo!...sasa Abiria tulisha-panic kabisa!, Moyo ulienda mbio mpaka nikahisi Roho inataka ku-log out,...ndipo nikasikia dereva anasema

"Jamani Abiria Mkaguane, isije kuwa kuna mtu kaingia na Mzoga wa Paka Shume humu ndani"
Ukaguzi huu sasa ulifanywa na Kondakta, akipita katika kila siti,..sasa alipofika kwangu ndipo kidogo nizimie!, kumbe katoto nilikobeba hakakuwa hata Pampas aisee! mimi sikujua, ndiko Kalikoshusha Uharo, ..that Uharo umekwenda direct to My Savco Jeans!....Jeans lote linanata, uharo umeshuka mpaka kwenye kamba za viatu, katoto kanakoroma,halafu tunavyokanyanyu
a ndio kanazidi kutibua mambo!....Mama wee abiria wote wameshika pua! Wanawaka hatari!!

"Washusheeee!......Washusheeee
!......Washusheeeee!"

Yaani kwa hasira nimemrushia yule Mama mtoto wake kidogo niue, tayari nilisimama kwenye seat huku jeans yangu ya appointment ikiwa inanata uharo kama nta ya nyuki,....tumeshushwa pale pale Kimara wote wawili, yaani mimi na yule Mama, gari imeondoka abiria wengine wanazomea...wengine wanatukana,,,,wengine wanacheka!

Hapa Chini Stendi ya kimara napo watu wamejaa, huu ndio wakati sasa ninabwata kishenzi!!
"Yaaani Wewe Bibi Mchawi sana! natamani hata nikutandike Ngumi ya roho hakiyanani!, leo nilikuwa naenda kuonana na Mtoto Mzuri Asunta Lovelicious,Ush
aniharibia sasa!!"

YEYE : haaa!! Kumbe wewe ndiye Shomari Kipapai bwana yangu Mpya wa Instagram?,..Mi ndio Asunta Chabwede Lovelicious wa Kibaha Maili mbili, jamani Pole Baby wangu, basi Mbebe mwanao nichukue Nyonyo na Maboga kwenye Mkoba!..kana njaa kweli!
ngachoka kabisa kumbe hiki kibibi kinachofanana na yule jamaa wa kwenye The God must be crazy ndo mrembo Asunta lovelicious binti aliyeunasa moyo wangu niliyemuhisi mtamu kama asali itokayo tabora,kwa kweli hiki kibibi kikantia hasira maradufu zaidi anyway ngoja nkitoka lock up kwa dhamana ntawaambia nini kilitokea eneo hilo...
😂😂😂😂😂😂😂😂

Ndugu zangu hiko ni kisa cha kutunga tu ila kiukweli wanaume wengi humu wamewahi kuuzwa/kuingia chaka kwa kudanganywa na picha fake za kwenye mitandao ya kijamii..unakuta mwanamke mkalii dp yake picha iliyoenda shule anaonekana mrembo zaidi ya Beyonce lakini njoo live sasa wengi wao ukiwaona live unawakimbia na kuwakwepa na utakuwa unajiuliza hivi ni huyu huyu au mwengine muda huo sasa ndo mpo eneo la tukio la kukutania upo kwa mbali kidoogo unamchora kwanza kabla ya kujitokeza lakini unachokishuhudia sicho ulichokiwaza maana demu wa kwenye picha tofauti kabisa na huyu ambaye unaona dhairi mabega yanapiga cheers na mawingu,yaani shapeless, cuteless😂
wanaume wenzangu njooni mtupe experience kama kuna mtu imewahi kumtokea hii
 
haha ha hahaa haa haaaa haaaa
..

hahaaa haaaaa "", daaaahh JF aisee",... hii chai sio ya taifa hili" in short jamaa unakipaji cha uandishi
 
haha ha hahaa haa haaaa haaaa
..

hahaaa haaaaa "", daaaahh JF aisee",... hii chai sio ya taifa hili" in short jamaa unakipaji cha uandishi
😂😂 tunasubiri ushee nasi experience yako mkuu hii kitu haijawahi kukutokea?
 
hahaa huwezi kuwa addicted wa social network " then usikutane na hiyo kitu"Aisee
Ila mademu wanazingua nao! profile pic mtoto anaonekana mkalii wengi wao ngoja ukutane nao sasa utatamani ukimbie mkuu,unakuta demu ana chunusi kama chenga za togwa,miguu haina uwiano kama miti ya genge bhna😂😂
 
huyo wa chunusi " aisee niliwahi kukutana na manzi wa aina hiyo ".. aliniambia niende kwao " k.koo mitaa ya fire ""...tulikutana Fb mnamo 2011
 
binafsi sidhani kama kuna mtu mzima anaweza kumtoa mtu kwenye daladala et kisa mtoto amejisaidia na kuna harufu mbaya.
labla ulipanda gari la watoto wanuka mikojo wenzako mtoa mada.
 
Kuna demu nilikuwa tunapanga kuonana...yeye ndo alikuwa ananisumbua ili tuonane bahati mbaya mi nilikuwa mkoani....Nikaona isiwe kesi ile nimeingia Dar kumuona si akaingia mitini...HADI LEO HUWA ANAVIEW STATUS ZANGU ZA WHATSAPP KIMYA KIMYA...mi nacheka mpaka basi
 
binafsi sidhani kama kuna mtu mzima anaweza kumtoa mtu kwenye daladala et kisa mtoto amejisaidia na kuna harufu mbaya.
labla ulipanda gari la watoto wanuka mikojo wenzako mtoa mada.

bora jumatatu shule zifunguliwe watoto kama nyie ambao wengi wenu tunaweza kulala na mama zenu na mkapatikana nyie muende shule tu...hukusoma kama kuna sehemu imeandikwa hiki ni kisa cha kutungwa!? usikurupuke wewe siku utajikuta una ujauzito wa mtu usiyemjua yaani kizazi cha sasa cha jf kinaboa kinoma nina miaka zaidi ya mitano Jf ila mwaka huu ndo nimeshuhudia wazinguaji wengi na vilaza wengi kama wewe
 
ha hahaa haa
 
binafsi sidhani kama kuna mtu mzima anaweza kumtoa mtu kwenye daladala et kisa mtoto amejisaidia na kuna harufu mbaya.
labla ulipanda gari la watoto wanuka mikojo wenzako mtoa mada.
umefatilia vzr kwel alichoandika!? Keshasema iyo ni stori ya kutunga so jitahid kuelewa kwanza kilichoandikwa ndo ukomenti mkuu
 
binafsi sidhani kama kuna mtu mzima anaweza kumtoa mtu kwenye daladala et kisa mtoto amejisaidia na kuna harufu mbaya.
labla ulipanda gari la watoto wanuka mikojo wenzako mtoa mada.
we nawe " wataka shari tu " hapa .. Umeshaambiwa hiyo stori ni hekaya ". .. then unakuja kukosoa " Kama sio ugomvi ni kitu gani ndugu "....

ili kuwa nikujibu Utumbo mixer kinyesi " but I'd yako " imenisuta " maana design kama na ifahamu hivi ".
.
kuwa OG bwana "...
 
Back
Top Bottom