saitama_kein
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 981
- 100
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hilda Gondwe anadaiwa kuomba auziwe kwa Sh6 milioni gari la serikali aina ya Toyota Landcruiser VX lililonunuliwa miaka mitatu iliyopita kwa Sh96 milioni.
Mwishoni mwa mwaka jana, gari hilo lenye namba za usajili STK 1867 lililokuwa likitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (RC), Monica Mbega lilikarabatiwa na kampuni ya Toyota ya jijini Dar es Salaam kwa Sh11 milioni.
Kwa kawaida magari ya serikali huwa hayalipiwi kodi, lakini kama gari hilo lingenunuliwa kwa bei ya soko, kuingizwa nchini na kulipiwa kodi mbalimbali ikiwamo ile ya 0ngezeko la Thamani(VAT), lingekuwa na thamani ya Sh155.7 milioni.
Shangingi lenye bei kama hiyo likiingizwa nchini linatakiwa kulipiwa Sh24 milioni kama kodi ya uagizaji (Import duty), Sh23.7 milioni kama VAT na Sh12 milioni ambazo ni kodi ya ushuru wa forodha.
Source: Mwananchi