Shamhuna aapa kulinda mafuta ya Z`bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shamhuna aapa kulinda mafuta ya Z`bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Majoja, Jul 13, 2011.

 1. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimemsikia Ndugu Shamhuna akilieleza Baraza la Wawakilishi Zanzibar , kuwa suala la mafuta ni la uchumi wa zanzibar na halina uhusiano na muungano.
  Kwa hiyo litatolewa katika shughuli za muungano.
  Kimsingi sipingi kujiondoa Zanzibar katika muungano lakini, najiuliza ikiwa suala la mafuta si la muungano je ni kwa nini Serikali ya Muungano kupitia TANESCO wanaendelea kusaidia uchumi wa Zanzibar kwa kuwapa umeme wa BURE!
  Haya matamshi ya Shamhuna yana dalili za kihuni tu ndani yake, Zanzibar kama serikali itoe tamko tu la kujitoa muungano tujue moja , si haya matamshi yasiyo na mbele wala nyuma.
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=2][/h]


  Na Charles Mwankenja  13th July 2011Waziri wa Maji, Ardhi na Nishati wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna  Waziri wa Maji, Ardhi na Nishati wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna, jana aliibua tena hoja za kuhoji Muungano aliposema Katiba ya Zanzibar na ya Muungano zote zina matatizo na ndio chanzo cha mgogoro unaoendelea juu ya umiliki wa mafuta na gesi visiwani hapa.

  Shamhuna, ambaye ni waziri mwandamizi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, alisema wakati umefika kwa Tanzania Bara kuwaachia wananchi wa Zanzibar haki ya umiliki wa rasilimali hiyo.

  Waziri Shamhuna alitoa kauli hiyo wakati anafanya majumuisho ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2011/12 katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.

  Alisema suala la umiliki wa mafuta katika bahari kuu ya Zanzibar lipo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na haoni sababu kwa nini wawakilishi wanalijadili katika kikao cha baraza.

  "Mwaka 2009 Baraza la Wawakilishi lilipitisha uamuzi wa kuondoa mafuta katika orodha ya mambo ya Muungano," alisema Shamhuna.

  Alisema kwa uamuzi wa baraza hilo, hatua inayofuata ni kwa serikali ya Muungano kupeleka muswada wa sheria bungeni utakaoliondoa suala hilo katika mambo ya Muungano.

  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wanahoji umiliki wa mafuta na gesi visiwani kuwa chini ya mambo ya Muungano, wakati rasilimali hiyo ni mali ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria iitwayo Mining Decree ya mwaka 1951 ya Zanzibar.

  Akifafanua zaidi, Shamhuna alisema kwa kuwa baraza hilo lilipitisha uamuzi wa kuondoa mafuta katika orodha ya mambo ya Muungano mwaka 2009, na Baraza la Mapinduzi lilitoa baraka zake juu ya uamuzi huo na aliahidi kuwa atasimamia kikamilifu kuhakikisha sekta hiyo inabaki chini ya umiliki wa Zanzibar.

  Hata hivyo, alisema kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na nchi mbili, (Zanzibar na Tanganyika) kumesababisha Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, zote kuwa na matatizo katika mambo mengi, yakiwemo ya uchumi, kisiasa na kisheria.

  "Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, zilizoundwa baada ya nchi mbili kuungana, zote zina matatizo, lakini wenzetu hawataki kuyaondoa," alisema Shamhuna.

  Alisema suala la haki kwa Zanzibar kumiliki sekta ya mafuta visiwani, litapatiwa ufumbuzi wa kudumu, kisheria kupitia Katiba mpya inayoendelea kuandaliwa.

  "Muswada wa mapitio ya Katiba mpya utakapoanza kutolewa maoni, naomba wawakilishi na wananchi, ajenda yetu namba moja iwe ni kupata Katiba itakayotoa haki kwa Zanzibar kumiliki mafuta visiwani," alisema.

  Baraza la Wawakilishi lilipitisha bajeti ya wizara hiyo bila mabadiliko yoyote.  CHANZO: NIPASHE

   
 3. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hivyo ndivyo wafanyavyo baada ya KUAPA kuilinda KATIBA ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.....
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wacha mafuta, hata Zanzibar yenyewe italindwa isichukuliwe kimzobamzoba na Tanganyika.


  “[President Nyerere] managed half the work of a python… He swallowed Zanzibar all right but he did not crush its fighting force first. The live animal is a long time digesting, and its kicks are being felt hurtfully, and possibly even fatally, deep inside Tanganyika’s body politic.”

  - ‘The Perils of Nyerere’ in The Economist of June 1964
   
 5. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yale yale matusi. Nakuomba utoe hoja tu na usitukane watu. Shamhuna ni Waziri wa SMZ, kumwita muhuni si ustaarabu.

  Hilo unalosema sio deni, bali ni rushwa yenu kwa SMZ ili huo "muungano" wenu feki usivunjike.

  Ondoeni majeshi yenu ya uvamizi kwanza, utavunjika tu.
   
 6. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ni akili iliyolala tu! Mafuta siyo malighafi katika dunia ijayo ila bado wamelala
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Shamhuni huyo.....
   
 8. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mliolala ni nyinyi mnaouza nchi yenu kwa magabachori kila siku.

  Nchi tajiri, watu wake maskini.

  Hayo ni matokeo ya kuendekeza pombe na ufisadi.
   
Loading...