Shambulizi la Westgate shopping mall Nairobi 2013

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,881
30,226
1547615994970.png


Marie Aude mama wa Kifaransa Mkurugenzi wa French- Institute for Research in Africa (IFRA) Nairobi alinialika mkutano Nairobi na ‘’theme’’ ya mkutano ule ilikuwa miaka 50 ya kuwakumbuka mashujaa waliopigania uhuru katika nchi za Afrika Mashariki lakini historia imewasahau.

Marie Aude alikuja hadi Dar es Salaam kunialika na kunitaka niandike paper. Mkutano huu ulikuwa tarehe 23 na 24 Septemba, 2013.

Nyakati za mchana siku ya safari zikaingia habari katika TV na mitandao ya kijamii kuwa kumekuwa na shambulizi la kigaidi Nairobi Westgate Shopping Mall wakishukiwa Al Shabab.

Hii hii mall kubwa iko Westland na ikipendwa sana na wenye uwezo wao.

Tumetua Niarobi na Kenya Airways kiasi cha saa 11 jioni na kitu cha kwanza nilichokutananacho ni kutokuwapo kwa watu ambao kwa kawaida huwa nje ya milango kupokea wageni ndani ya uwanja.

Badala yake pote pale nje peupe hakuna mtu hata mmoja wametanda askari na silaha na watu wako mbali kabisa barabarani nyuma ya vizuizi vya chuma.

Hapo ndipo walipokuwapo wapokeaji na madereva wa teksi.

Nilikuja kupokelewa na wakati napelekwa hotelini katikati ya mji niliona mji wa Nairobi umejiinamia, watu na magari pia yamepungua barabarani. Nairobi kwa kawaida ni mji wenye pilikapilika nyingi hasa wakati zile za ‘’rush hour,’’ watu wanarejea majumbani wakitokea makazini kwao, foleni ya magari na ‘’matatu,’’ yaani daladala huwa ndefu.

FM station ndani ya gari ikawa haina habari ila habari za Wasomali waliovamia Westgate Mall na haijulikani watu wangapi wamepoteza maisha.

Kwa kweli kwa mbali nilianza kuwa na hofu na kujiuliza nini kimenileta mji huu wakati kama ule.
Kwa kawaida nina hoteli yangu huwa napenda kwenda kula chakula cha usiku niwapo mji ule lakini ile hali iliyokuwapo haikunitia moyo kutoka nje ya hoteli na baada ya muda ikaanza kunyesha mvua nah ii ikazidisha hali ya kukumbuka nyumbani

Kwenye kongamano chumba kizima Muislam peke yangu ukitoa ndugu zangu wa wawili wa Kiismalia.

Mmoja ni mama mtu mzima aliyejitambulisha kwangu kama mhariri wa jarida la Nawaz ambae alikuwa na kijana kutoka ofisini kwake (Nawaz walichapa papaer yangu).

Watoa mada wenzangu wote Wakristo pamoja na waliohudhuria.

Bahati yangu mbaya ni kuwa nikizungumza iwe Kiingereza au Kiswahili ‘’accent,’’ yangu mara moja nafahamika kuwa ni Mswahili tena wa Tanzania.

Najitahidi kujibanza lakini inakuwa shida kidogo maana dada yangu Marie Aude mtayarishaji wa Kongamano anahisi mimi mgeni wake tena isitoshe jina langu kapewa na mtu ambae yeye anamheshimu sana, Ahmed Rajab, heshi kutaka kunichangamsha kwa hili na lile na hii ikawa inafanya nionekane.

Nahisi alikuwa anaona kuwa mimi nimejikuta bila ya kutegemea niko katika ‘’kambi ya adui,’’ Waingereza wanasema, ‘’enemy’s camp.

KIjana mmoja kutoka Chuo Kikuu Cha Nairobi Idara ya Historia anatoa mada ya Bi. Titi Mohamed na aliponitambua akaniuliza kama nikimjua Bi. Titi.

Namjibu lakini sina raha ya mazungumzo.

Hapo tulipo na Westgate Mall ni jirani sana kiasi cha labda kilomita moja hivi na zikawa zinasikika sauti za risasi kuashiria kuwa kuna mapigano yanaendelea.

Katikati ya kongamano akasimama mtu kuomba tusimamishe mjadala yafanyike maombi. Jina la Yesu linasikika kila mlipuko ukisikika hasa kutoka kwa wanawake.

Macho ya wenzangu wote kwangu kama vile mimi ndiye niliyewatuma Al Shabab kuvamia Kenya.
Kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu sana.

Zamu yangu ya kuzungumza imefika na Marie Aude kanitambuilisha. Chuki na ghadhabu katika sura za wasikilizaji wangu zilikuwa dhahiri.

Projector imeweka kwenye screen picha ya Abdul Sykes, Nyerere, Dossa na Lawi Sijaona. Niliipuuza ile picha kama vile haipo pale.

Nilianza kwa kutoa pole kwa msiba uliowafika watu wa Kenya.

Kisha nikaeleza mafunzo ya Uislam vipi Allah anakataza kuua nafsi pasi na haki.
Nikazungumza kama dakika mbili hivi.

Ilisaidia sana nilihisi ile ‘’tension,’’ iliyokuwapo kama inashuka taratibu.

Siku ya pili walipokuja kunichukua asubuhi kunipeka Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta nilishukuru kuwa naondoka Nairobi salama.

Leo mchana nilipoona mashambulizi mengine Nairobi, fikra zangu zikanirudisha tena kwenye kumbukumbu ile ya mashambulizi ya Westgate Shopping Mall miaka mitano iliyopita.
 
Mohamed Said, uandishi wako huwa unamchukua anayesoma makala yako kwenye tukio husika na baada ya simulizi kuisha, anayesoma hurudi alipo.

Ubarikiwe sana. Mimi ni mkristo na mara zote huwa ninasema siwezi kumchukia mtu ambaye hamwamini Mungu wangu.

Nitakachofanya ni kumwelezea uzuri wa Mungu wangu. Hayo mengine Mungu wangu atapambana naye.





Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom