Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani
_96038895_ransomware.png

Haki miliki ya pichaWEBROOT
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika baadhi ya kompyuta wakati wahalifu wa mtandao walipotekeleza shambulio
Sambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia utumizi wa vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.

Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.

Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi nchini China.

Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.

BBC inaelewa kwamba takriban mashirika 40 na huduma kadhaa za matibabu ziliathirika huku operesheni na mikutano ikifutiliwa mbali.

Programu hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.

Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.

Idadi kubwa ya kampuni kubwa ikiwemo Telefonica ,kampuni ya umeme ya Iberdrola na ile ya Gesi asilia pia ziliathirika huku kukiwa na ripoti kwamba wafanyikazi katika kampuni hizo waliagizwa kuzima kompyuta zao.

Raia walipiga picha za kompyuta zilizoathirika katika mtandao wa Twitter ikiwemo mashine ya kukata tiketi za safari ya reli nchini Ujerumani pamoja na maabara ya kompyuta nchini Italy.chanzo.Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani - BBC Swahili
 
Kitu kingine nilichojifunza ni kwamba hii Ransomware ina affect Windows 7 ambazo hazijawa Updated ku Fix ile SMB Vulnerability ilokua revealed sometimes na Wikileaks ikihusisha NSA na Shadow Blockers!

Kwa watumiaji wa Windows 10 ambako Regular Updates hauwezi zi switch off na watumiaji wengine ambao hufanya Regular Updates za Windows zao ni vigumu kushambuliwa na wadudu kama hawa!
 
Hii kitu imeshamalizwa na malware tech mwenye umri wa miaka 22. Msiwe na hofu kuhusu computer zenu.
 
Yote kwa yote hawa jammaa (hackers) wanajua kutumia vizuri RAT (remote access tool), ambayo ikitumika ipasavyo ni ngumu sana kuwatrace
 
Hii kitu imeshamalizwa na malware tech mwenye umri wa miaka 22. Msiwe na hofu kuhusu computer zenu.
Version 2 yake ilishatoka na hiyo sio Ransomware ya kwanza kuna Member hapa JF mafile yake yaliwai fungwa na mdudu kama huyo nafikiri ni mda watu kujua jinsi hao wadudu wanavyo sambaa, sana sana nimeona njia inayokua quoted ni ile kuisambaza kupitia documents na attachments za email!
 
Hii kitu imeshamalizwa na malware tech mwenye umri wa miaka 22. Msiwe na hofu kuhusu computer zenu.
unafkiri ni rahisi hivyo? na hio sio issue ya kwanza wala sio ya mwisho, solution ni kuwa na os ambayo ipo up to date, kila siku ni windows xp na 7 ndio wanaoathirika tu.
 
Hii nyuz ina 9 replies na hii ni ya 10 ni page 2. Ila uzi ungekuwa "jinsi ya kumfikisha kileleni bibi..." nina hakika tungekuwa reply ya 159...tz nchi ya viwonder!!
 
Hii kitu imeshamalizwa na malware tech mwenye umri wa miaka 22. Msiwe na hofu kuhusu computer zenu.
Ni kweli lakini bwana mdogo mwenyewe anasema hana uhakika kuwa hiyo itakuwa ni suruhisho la kudumu!
 
Au na Mimi wamenidukua maana kila Nikingia internet naambiwa your connection is not secure
 
Back
Top Bottom