Kisima
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 4,438
- 5,441
- Thread starter
- #41
Niko serious na ununuzi wa shamba hili naomba kujua haya:
Lina hati ya kijiji au?
Hayo maji ya mto ni throughout the year au?
Je wewe ndiye mmiliki halali au la familia?
Ni KM ngapi from main road
Kuna huduma gani karibu mf zahanati (Km ngapi, Ofisi ya serikali ya kijiji?)
Kuna majirani au ni mashamba tu?
Naomba majibu mkuu.
Mkuu samahani sana kwa kuchelewa kujibu maswali yako.
1) Shamba hili ni mali yangu mwenyewe nililipata kwa kununua kwa mtu na manunuzi yalifanyika rasmi kwa ushuhuda na usimamizi wa serikali ya kijiji. Hivyo utakaponunua, pasipo kukiuka maelezo ya tangazo hili pia ntakukabidhi rasmi mkataba wa mauziano ya awali wa shamba hili(shfting of ownership property)
2) Maji niya uhakika mwaka mzima.
3) Kutoka barabara kuu ni km5 na limezungukwa na mashamba makubwa ya miwa na watu ni wengi tu(sio porini)
4) Huduma ya Zahanati ipo km2 kutoka shambani pia huduma nyingine za kijamii zinapatika kirahisi kabisa.
Nakukaribisha sana mkuu tuongee kuhusu manunuzi.