Shamba zuri linauzwa.

Tangazo limetulia ila Dah !!I wish na mimi ningekuwa na hiyo pesa ila gud luck..

Thanks mkuu. Zichange uwahi kuja kununua bado lipo mikoni mwangu!
 

Nina milioni 3.5 kwa hilo shamba. Ni Pm kama uko na moyo. ILA Turiani nasikia kuna wachawi sana!
 
Nina milioni 3.5 kwa hilo shamba. Ni Pm kama uko na moyo. ILA Turiani nasikia kuna wachawi sana!

Hamna uchawi mkuu hizo ni longolongo na hekaya za watu wavivu wa maendeleo.
Hela yako ni nzuri lakini haitoshi kwa thamani ya shamba hili.
Jikusanye mkuu unipe kitu kamili tajwa hapo juu tufanye mauziano!
 
Kaka ungetuwekea na picha ingekuwa poa sana, tunataka tuone hiyo tambarare unayosema
 
Kaka ungetuwekea na picha ingekuwa poa sana, tunataka tuone hiyo tambarare unayosema

Mkuu amini nilichoandika hapo juu. Ni bahati mbaya simu yangu haina uwezo wa kuapload picha humu. Ila hii haiondoi uhalali wa kununua shamba hili kama u mhitaji.
 
we nawe!hapa si inabidi awe na herikopta

Teh teh teh!
Ni haki yake lakini mkuu si unajua tena wengi wetu ni wajukuu wa Tomaso!
Ila kweli kitu cha herikopta kingefotoa aerial photograph!
 
Mkuu, bado lipo?

Bado lipo mkuu mbio zako tu! make ni wengi wamehamasika na kuahidi kuja kujionea ili twende hatua nyingine ya kuuziana.
Nakukaribisha sana mkuu na ikiwezekana nicheki kwaPM tuongee ndugu yangu!
 
Perfect.....

True that!
Nazidi kuwakumbusha wadau kuwa shamba bado lipo licha ya ahadi kedekede za kuja kuliona, lakini mwenye kisu ndio mla nyama.
Karibuni sana!
 
Hata mimi nauza ekari 30 zote zimepandwa mananasi na nimeshaanza kuvuna.kila ekari moja milion 3 liko rufiji km 120 kutoka dar.
 
Hata mimi nauza ekari 30 zote zimepandwa mananasi na nimeshaanza kuvuna.kila ekari moja milion 3 liko rufiji km 120 kutoka dar.

Madalali utawajua tu! yaani kuona tangazo tu mate yashaanza kukutoka! unahsi ninapga hela sana eee au nimekubania nafasi umekosa pa kutundika tangazo lako la udalali humu JF? MODs hamtanitendea haki kama hili jamaa hamtalipiga BAN.
Nahsi ulizoea kudesa tangu utotoni kwako ndiyo maana huna maarifa hata ya kuandika tangazo!
 
:smile-big::smile-big::smile-big: Mkuu kweli aisee mambo za kuchinjana si mazuri

Huku hakuna migogoro ya ajabu mkuu nimezungukwa na mashamba ya "Wenye Nchi" nisingependa kuwataja hapa. Huku sahau kuhusu migogoro kati ya mkulima na mfugaji.
Wafugaji huku mashambani tunawategemea sana make ndo wanaostablize uchumi na mzunguko wa hela. Hivyo tunajitahidi kujenga mahusiano mazuri ili kuwanufaisha wananchi wanaotuzunguka na hatimae kuchochea maendeleo.
Labda kwa kukusaidia tu ni kwamba mi ni good reconciliator wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Nashangaa Rais hajapitisha jina langu katika uteuzi wa wajumbe wa katiba!
 
 
Niko serious na ununuzi wa shamba hili naomba kujua haya:

Lina hati ya kijiji au?
Hayo maji ya mto ni throughout the year au?
Je wewe ndiye mmiliki halali au la familia?
Ni KM ngapi from main road
Kuna huduma gani karibu mf zahanati (Km ngapi, Ofisi ya serikali ya kijiji?)
Kuna majirani au ni mashamba tu?

Naomba majibu mkuu.
 

Nikatie 2 heka mkuu, npm tufanye biashara
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…