Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Kufuatia shamba la mahindi zaidi ya hekari mbili kufyekwa wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi, Mkuu wa wilaya hiyo, Jamila Yusuph amesema mahindi hayo yalipandwa kinyume cha sheria.
Amesema kulingana na sheria ndogo za manispaa hiyo, hakuna mwananchi anayeruhusiwa kupanda mazao yanayovuka urefu wa goti katikati ya mji kwani ni kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Licha ya sheria kukataza hivyo, mkulima ambaye mahindi yake yamefyekwa, amerudia kosa alilotenda mwaka jana na kusamehewa, huku akitakiwa kulipa faini lakini mwaka huu tena amerudia kosa hilo.
Mwananchi