Shamba la chumvi

fungafunga

Senior Member
Mar 30, 2010
116
155
Naomba msaada kwa mwenye uelewa wa mambo ya uwekezaji katika mashamba ya chumvi.

1. Yapi maeneo sahihi ya uwekezaji
2. Upatikanaji wa maeneo husika na garama zake
3. Changamoto za kilimo hiki (faida na hasara)
4. Soko la chumvi
5. Wapi au nani naweza mtembelea nikajifunza kwa vitendo
6. Jarida, kitabu au blog yeyote ninayoweza pata taarifa sahihi

Na taarifa yeyote utakayoona inanifaa. Tafadhali ninaomba msaada wenu!
 
Hii kitu nilishawahi kuonaga kwa mbali maeneo ya kunduchi kule karibia na bahari,Nakushauri kafanye reseachi maeneo ya kunduchi baharini utafaidika sana
 
Thanks Hajto!
Tatizo lililopo kunduchi yale ni mashamba ambayo yalifanya kazi zamani sana na sasahivi ni kama yameachwa flani hivi. Nilitaka nipate ambalo linafanya kazi ili nikajifuze kwa vitendo.
Ila nashukuru kwa kujali..
 
fungafunga,
Jina hili, 'Shamba la Chumvi' linamaanisha, kwa Kiingereza, 'Salt pans', na Wavunaji wa Chumvi huyaita "mabirika ya chumvi".

Uvunaji wa Chumvi unasimamiwa na Wizara ya Madini, ikimaanisha kuwa Chumvi ni moja ya madini yanayovunwa Tanzania.

Pamoja na ukweli kuwa Jukwaa la Kilimo siyo jukwaa sahihi kwa mada hii, ningependa, kwa ufupi kabisa, nielezee kidogo kuhusu Chumvi na Uvunaji wa Chumvi.

Madini ya Chumvi, nchini Tanzania, huvunwa katika mikoa ya Kigoma (Uvinza), Simiyu (Ziwa Natron), Ukanda wa Pwani, (Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara).

Matumizi ya Chumvi nchini Tanzania yanakadiriwa kufikia tani 500,000 kwa mwaka wakati uzalishaji hapa nchini ni tani 150,000 kwa mwaka.

Upungufu wa tani 350,000 kwa mwaka unajazwa na Chumvi toka Kenya.

Chumvi iliyoko madukani yenye nembo ya K-Salt au Malindi Salt inatoka Kenya.

Kenya inatulisha chumvi wakati sisi tuna uwezo wa kuzalisha chumvi MARA TATU zaidi ya Kenya kwa sababu Pwani yetu ya Bahari ya Hindi ni ndefu zaidi ya Pwani ya Kenya.

Pwani yetu, 'shoreline length' ni kilomita1424, wakati 'shoreline' ya Kenya ni kilomita 536 tu. Hapo bado tuna Simiyu na Kigoma.

Chumvi, pamoja na kutumika kama kiungo cha chakula cha binadamu na mifugo, hutumika pia katika viwanda vya minofu ya samaki, usindikaji wa nyama, usafishaji wa maji, utengenezaji wa karatasi, uchimbaji wa visima vya gesi na mafuta, na matumizi mengine mengi sana.

Chumvi inayotumika kama kiungo cha chakula hutakiwa kuwekewa Madini Joto, 'iodine' ambayo ni chanjo muhimu sana dhidi ya mtindio wa ubongo 'mental retardation' kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano.

Kwa kumalizia, Uvunaji wa Chumvi ni FURSA ya kipekee kwa sababu CHUMVI NDIYO MADINI PEKEE DUNIANI, AMBAYO KILA UKIYAVUNA, MWENYEZI MUNGU ANAKULETEA TENA UPYA, ili uendelee kuyavuna.

Kwa lugha ya wachimbaji Madini, "Chumvi ni makinikia pekee duniani, ambayo kila ukiyavuna, Mwenyezi Mungu anajazia upya pale ulipovuna".

Taratibu za "kilimo" hiki cha chumvi zinapatikana katika Ofisi za Madini (Regional Mines Offices- RMO's) katika Mikoa ya Kigoma, Simiyu, Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara.
 
Naomba msaada kwa mwenye uelewa wa mambo ya uwekezaji katika mashamba ya chumvi.
1. Yapi maeneo sahihi ya uwekezaji
2. Upatikanaji wa maeneo husika na garama zake
3. Changamoto za kilimo hiki (faida na hasara)
4. Soko la chumvi
5. Wapi au nani naweza mtembelea nikajifunza kwa vitendo
6. Jarida, kitabu au blog yeyote ninayoweza pata taarifa sahihi
Na taarifa yeyote utakayoona inanifaa. Tafadhali ninaomba msaada wenu!
Fungafunga, Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali linaweza kuwa sahihi zaidi kwa "Kilimo cha Chumvi" kuliko hili la Kilimo.
Mods ukiihamishia huko hii mada, Watanzania wengi watapata fursa ya kukijua "kilimo" hiki na kuchangia mawazo zaidi.
Mods, ikikupendeza zaidi, kwa heshima na taadhima, anzisha JUKWAA LA MADINI, na mada hii ya Fungafunga iwe ya kwanza.
 
Jina hili, 'Shamba la Chumvi' linamaanisha, kwa Kiingereza, 'Salt pans', na Wavunaji wa Chumvi huyaita "mabirika ya chumvi".
Uvunaji wa Chumvi unasimamiwa na Wizara ya Madini, ikimaanisha kuwa Chumvi ni moja ya madini yanayovunwa Tanzania.
Pamoja na ukweli kuwa Jukwaa la Kilimo siyo jukwaa sahihi kwa mada hii, ningependa, kwa ufupi kabisa, nielezee kidogo kuhusu Chumvi na Uvunaji wa Chumvi.
Madini ya Chumvi, nchini Tanzania, huvunwa katika mikoa ya Kigoma (Uvinza), Simiyu (Ziwa Natron), Ukanda wa Pwani, (Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara).
Matumizi ya Chumvi nchini Tanzania yanakadiriwa kufikia tani 500,000 kwa mwaka wakati uzalishaji hapa nchini ni tani 150,000 kwa mwaka.
Upungufu wa tani 350,000 kwa mwaka unajazwa na Chumvi toka Kenya.
Chumvi iliyoko madukani yenye nembo ya K-Salt au Malindi Salt inatoka Kenya.
Kenya inatulisha chumvi wakati sisi tuna uwezo wa kuzalisha chumvi MARA TATU zaidi ya Kenya kwa sababu Pwani yetu ya Bahari ya Hindi ni ndefu zaidi ya Pwani ya Kenya.
Pwani yetu, 'shoreline length' ni kilomita1424, wakati 'shoreline' ya Kenya ni kilomita 536 tu. Hapo bado tuna Simiyu na Kigoma.
Chumvi, pamoja na kutumika kama kiungo cha chakula cha binadamu na mifugo, hutumika pia katika viwanda vya minofu ya samaki, usindikaji wa nyama, usafishaji wa maji, utengenezaji wa karatasi, uchimbaji wa visima vya gesi na mafuta, na matumizi mengine mengi sana.
Chumvi inayotumika kama kiungo cha chakula hutakiwa kuwekewa Madini Joto, 'iodine' ambayo ni chanjo muhimu sana dhidi ya mtindio wa ubongo 'mental retardation' kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano.
Kwa kumalizia, Uvunaji wa Chumvi ni FURSA ya kipekee kwa sababu CHUMVI NDIYO MADINI PEKEE DUNIANI, AMBAYO KILA UKIYAVUNA, MWENYEZI MUNGU ANAKULETEA TENA UPYA, ili uendelee kuyavuna.
Kwa lugha ya wachimbaji Madini, "Chumvi ni makinikia pekee duniani, ambayo kila ukiyavuna, Mwenyezi Mungu anajazia upya pale ulipovuna".
Taratibu za "kilimo" hiki cha chumvi zinapatikana katika Ofisi za Madini (Regional Mines Offices- RMO's) katika Mikoa ya Kigoma, Simiyu, Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara.

Nakushukuru sana fundimchundo!
Nimepata pa kuanzia
 
Nakushukuru sana fundimchundo!
Nimepata pa kuanzia
Huu uzi wako Fungafunga, unaweza kufungua njia nzuri kwa wote walio na nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa chumvi.
Soko la ndani ni kubwa sana. Soko la nchi jirani ni kubwa zaidi.
Kizuri kuliko vyote ni kwamba mtaji unaohitajika ili kuanza uzalishaji wa chumvi siyo mkubwa.
Kwa kiwango kikubwa, uzalishaji wa chumvi nchini mwetu unafanywa na watu wa hali ya chini kabisa.
Chumvi ni madini namba moja kwa kuwawezesha Watanzania kuingia katika Tanzania ya Uchumi wa Viwanda.
 
Kuna makala moja niliiona kuhusu ziara ya tume ya madini katika Kampuni ya Neel Kanth Salt Ltd ambacho kipo Shungubweni wilaya ya Mkuranga. Kiwanda hiki kinaaziga asilimia 70 ya malighafi ya kuzalisha chumvi kutoka nje ya ya nchi kwa madai kwamba wakulima wa chumvi wa ndani ya nchi wavuna chumvi ambayo haijakomaa. Wanasema chumvi lazima itimize miezi mitatu kabla ya kuvunwa. Na mwenyekiti wa tume hiyo Profesa Idris Kikula akatoa miezi mitatu hali hiyo isiendelee,hivyo soko ni kubwa sana. Nenda mkuranga kuna mashamba ya chumvi.
Ila biashara hii inalipa sana ukiwa na elimu nayo.
 
Aiseee! Mi nikajua shughuli za ujasiriamali zishaisha, kumbe ziko nyingi tu!! 😂😂😂😂

Ngoja twende kwenye chumvi sasa kabla wahamasishaji (motivational speakers) hawajaanza kuwalisha watu sumu 😂😂😂
 
Kuna makala moja niliiona kuhusu ziara ya tume ya madini katika Kampuni ya Neel Kanth Salt Ltd ambacho kipo Shungubweni wilaya ya Mkuranga. Kiwanda hiki kinaaziga asilimia 70 ya malighafi ya kuzalisha chumvi kutoka nje ya ya nchi kwa madai kwamba wakulima wa chumvi wa ndani ya nchi wavuna chumvi ambayo haijakomaa. Wanasema chumvi lazima itimize miezi mitatu kabla ya kuvunwa. Na mwenyekiti wa tume hiyo Profesa Idris Kikula akatoa miezi mitatu hali hiyo isiendelee,hivyo soko ni kubwa sana. Nenda mkuranga kuna mashamba ya chumvi.
Ila biashara hii inalipa sana ukiwa na elimu nayo.

Asam unaweza nipa link ya hiyo makala?
 
Njoo na Manyara wilaya ya Hanang kuna ziwa ka chumvi kubwa tu chumvi ni ya kuchota kwa spades na mikokoteni huna haja na shamba maana yenyewe inatengenezeka tu.

Nilivuna miaka ya 2015 wakati wateja walikuwa wanatoka DRC,Burundi,uganda na sehemu mbali mbali kwani walikuwa wananunua kwa bei nzuri ila Ngosha alipoingia tozo ziliongezeka wakawa hawaji tena kununua chumvi yetu.
chumvi hii ni nyingi sana haiwezi kumalizika ziwani.
karibu ujifunze pia au nitafute kwa namba 0714144414
 
Back
Top Bottom