Shamba Kwa mwenye Mahitaji ya Kujiendeleza (Kigamboni) Bure!!

Shamba Kwa mwenye Mahitaji ya Kujiendeleza (Kigamboni) Bure!!

Kitope

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
236
Reaction score
58
Habari waungwana wote!Ngoja kwanza nianze kwa kutoapole na mihangaiko ya kuzungusha gurudumu la maendeleo kwa wale wanaojitumakila kukicha kwa kutafuta riziki. Sio siri ya kwamba humu ndani wengi huwawanatoa changamoto za kila mtindo, kuna wale wanaochangia hoja tofauti, wapowanaotoa ushauri wa biashara, kilimo, ufugaji na kadhalika za kila mtindo. Wapopia wale wanaopita tu hata kama ushauri wao unaweza usitumike sana ila nimijadara ambayo pia huweza kuendelezwa kwa wale wenye enterprenueral skills. Kwanikuna faida katika kila hoja iwapo mtu ataangalia kwa njia ya positive. Anyways, Leo hii nimeamuakujitolea jambo moja na kabla ya yote wacha nijitambulishe kwa kujua mimi humusio mchangia hoja za kila siku, hivyo sio wengi wanitambuao.Kitope ni jina kama la watu wote wanavyotumiahumu ’’Nicknames’’ kwa kuepuka jambo moja ama jingine. Professional:- A business consultant in an international level mostly Europe –Africa. Maritualstatus: Ndoa na watoto watatu (nashukuru mungu kwa kweli)Financialcapacity : hii inategemea ni vipi tunaichachambua lakini nashukuru mungu piamkate haupigi chenga = kwa wale wanadini na wana busara itakuwa wanaujua uleusemi wa kwamba ukitaka kushukuru mungu angalia aliye chini yako na sio wale wajuu. Experience: 15 years in my professionNationality: Mbantu born and raised.Preferencein business environment : honesty and commitments to achieve the intended goalsand time saving.Sasabasi! Kutoka hapo juu ni imani yangu kuwa wale watakao wasiliana nami kuhusuhii post wataweka utani na mashaka ya kijinga pembeni. Although!!! Maswali yakila namna yanakaribishwa iwapo yatahusiana na hichi ntakachokitoa chini hapo.Ninaumiliki wa kashamba kasichozidi ekari 8 katika maeneo ya kigamboni km takribani10 kutoka Dar-es-salaam Zoo kwa wale wafahamu wa maeneo hayo. Kutokanana shughuli zangu za kila siku haziniruhusu kujishughulisha sana na kilimo amaufugaji ! Leo hii nimeamua kuyatoa mashamba haya kwa mjasilimali yeyote mwenyenia ya kujiendeleza na kujikwamua katika mitihani ya maisha. Kama mtu ana ideayake ya kilimo ama ufugaji na tatizo ni sehemu ya kufanyia shughuli hizo, Leohii ni nafasi ya kufuta tatizo ilo na kuangalia vikwazo vingine vitakavyomzuia.
  • Awemtu mwenye nia ya kujiendeleza
  • Awena mawazo ya kibiashara ambayo yatamnufaisha kujijenga
Shambalina uwezekano wa maji kwa ajili ya matumizi ya shambani bila matatizo. Hakuna bandalakini hili ni jambo linaloweza kutatuliwa bila matatizo. Rutuba ya kutosha,mara ya mwisho palilimwa matikiti maji na matokeo yake watu walishindwa kuvunakutokana kwa wingi na kutokutayarishwa kwa wateja kwa wakati muafaka. Kwa ujumlashamba ni zuri kwa kilimo na ufugaji wa mitindo tofauti.
  • Natoanafasi hii ya shamba bila gharama za aina yoyote ile
  • Niana madhumuni kwa kile ninachokipata mimi ni kwamba shamba litakuwa na shughulihivyo pana ulinzi na utunzaji wa aina Fulani. Kama tunavyojua hapa kwetu kamahakuna uangalizi mengi yanaweza kutokea.
  • Kukihitajikaushirikiano wa aina yoyote, mtu asisite kuwasiliana nami ili kuangalia nininitaweza kujihusisha,, ila kama nilivyosema hapo juu muda wangu si mwingikwenye fani hizi. Ingawaje ningependa kujishirikisha kwa kilimo na ufugaji pia.
  • Kuondoautata ni kwamba Shamba haliuzwi kwa hiyo hakuna haja ya kufikiria kwamba hiloni jambo la kujadili.
Uwezekanoni mkubwa sana kwamba hapo juu sijaweka maelezo ya kutosha, Tafadhali usisitekuwasiliana nami kwa majadiliano ama maswali yoyote kuhusu sehemu iyo. Kwaufupi ni hivi.
  • Ninashamba ambalo mimi mwenyewe siwezi kutumia kwa muda huu
  • Nahitajimtu wa kutumia shamba hilo bila kumchaji gharama zozote kwa sababu nitapataulinzi wa aina Fulani
  • Nimeonabora kutoa kwa mtu mwenye nia ya kujiendeleza na itakuwa nimetoa msaada kwawale wasio na uwezo wa kukodisha ama hakuna sehemu ya kukodisha (najitolea tu)
  • Siuzikwa sababu nina mipango ya miaka ya mbele kupaendeleza kwa kile nilichonachoakilini mimi mwenyewe ama possibly kushirkiana na atakae kuwepo hapo baada yakuona juhudi zake.
  • Mwishositoweza kuweka picha na Ni nia yangu kuchangia.
Maswali,ushauri, mawazo, hoja na changamoto Zinakaribishwa.
Asanteni sanawanajamiiKitope.
 
Naomba mawasiliano yako ya simu, nina uhahitaji sana wa shamba lenye sifa hizo!
 
Kwanza nikushukuru kwa moyo wako wa ukarimu kwa maana wenye roho kama yako ni vigumu kukutana nao kwa dunia hii ya leo!
 
Tunakushukuru sana mkuu kwa moyo wako huu. Tunaomba tusaidie mawasiliano yako ili atakayeweza afike na kuanza kujitafutia riziki. Natanguliza shukrani!
 
Ni vizuri kuona Kuna wakuu wenye Nia na Madhumuni !! Ningeomba Kitu kimoja tu kama inawezekana! Labda ni vizuri mtu Akijitambulisha kwa ufupi kwenye PM kama nilivyojitambulisha mimi. na akaeleza ama kuuliza maswali yake kabla hatujabadilishana namba za simu kwa mawasiliano zaidi. Jambo moja nilisahau kuliweka hadharani! Katika biashara zote ambazo watu wangekuwa na mawazo ya kufanya ningeomba Biashara ya kitimoto isiwemo. hii ni kuheshimu majirani na pia mimi mwenyewe nisingependelea.
Asanteni tena na kama mwenye idea zake asisite kuwasiliana nami kwa PM. itakapobidi kubadilishana namba zasimu pia tutafanya hivyo. naomba tu wale walio serious only na tayari kufanya shughuli ili tusije kumpa mtu nafasi kisha miezi miwili baadae tuweke post tena kwa sababu aliyepewa hakuonekana. 🙂
 
Kwanza nikushukuru kwa moyo wako wa ukarimu kwa maana wenye roho kama yako ni vigumu kukutana nao kwa dunia hii ya leo!

Shaka ondoa mkuu! Ingekua vizuri kama ungefafanua kidogo zaidi kama una maswali ama mawazo kabla atujabadilishana namba za simu 🙂
 
dunia hii!! uwe na mikataba ya ki wanasheria ndugu unless!! "ooh tumekaa hapa miaka mitano sasa itakuwaje" mara ohh tulipe fidia zetu! >>ni utu mwema<< but mtu asiweke makazi labda ulinzi tu!
 
Mitanzania mivivu, watataka uwape na mtaji na kisha wasifanye lolote. Utanambia.

Watakuja na porojo kibao.

Nakushauri, weka banda zuri la kuishi familia. Nenda India au Egypt utapata wakulima tena walio somea kilimo, unamuajiri mmoja anakuja kuwa General Manager wa hilo shamba. Gharama yako ni mazao ya mwanzo tu au mwaka wa mwanzo, baada ya hapo shamba litajiendesha lenyewe.

Watanzania nuksi, watakuja hata kukurekebisha kusema ni lao.

Ukweli ubaki kuwa ukweli ingawa ni mchungu.
 
Najua wangu, sio kazi ndogo

Akili za mafisadi utazijua tu. Mwenzako anajaribu kusaidia his/her fellow countrymen /countrywomen bila hata chembe ya ubinafsi, wewe unamletea hadithi za kuleta foreigners. Hivi hamuoni aibu au dhambi jirani zenu wanapokosa hata hela ya mkate kwasababu ya ufisadi wenu?

Shame on you.
 
Kwa kuwa mimi ni mtanzania, na kwakuwa wewe umeamua kututuka watanzania wote kwa ujumla..... Basi na mimi ninakutukana kimoyo moyo. Tena tusi baya kabisa. Nimechukia. Nakutukana tena! Dada nimekutukanatusi zito sana...nisamehe... Tusi jingine hilo!
 
Kumleta foreigner ni ufisadi? 😕
 
nilitaka kukupa likes 10 nimeshindwa yaani huyu mtu FOX NI.....!
 
Na kama hk8,unaonaje kama ungetoa mwanya kwa walau watu zaidi ya mmoja!!!.
 
Kumleta foreigner ni ufisadi? 😕

Context is everything. Kama umesoma mada, hakuna sehemu yoyote ambayo bw. Kitope amesema anataka kutengeneza hela kwa namna yoyote ile. Kama nimemwelewa vizuri, nia yake ni kusaidia mtu ambaye amekwama kwa sababu hana resource ya kukodisha shamba.

Huyo mtetea mafisadi anakuja na akili zake za kifisadi. Btw, nimependa jinsi Kitope alivyomjibu.
 
Taratibu waungwana, maneno makali hayatotusogeza mbele bali kutukwamisha tulipo na kuzua malumbano ambayo yanaweza kutunyima nafasi ya kujadili yaliyo ya msingi. kukosea kumo haliyakuwa sisi sote ni binadamu na kasoro ni moja ya sifa tulizoumbwa nazo.
Asanteni kwa michango ya mawazo na hakuna litakalopuuzwa na tutaweka uangalifu kwenye kuchagua yepi ya kutumia.
shukrani kwa wote
 
Uwezekano upo, Mimi sitozuia watu ushirikiano ila waliotangulia watawajibika na ni yupi wa kumshirikisha. ofcourse nipo mwenyewe kwenye ku approve watu.

Na kama hk8,unaonaje kama ungetoa mwanya kwa walau watu zaidi ya mmoja!!!.
 
Mitanzania mivivu, watataka uwape na mtaji na kisha wasifanye lolote. Utanambia.

Watakuja na porojo kibao.

Nakushauri, weka banda zuri la kuishi familia. Nenda India au Egypt utapata wakulima tena walio somea kilimo, unamuajiri mmoja anakuja kuwa General Manager wa hilo shamba. Gharama yako ni mazao ya mwanzo tu au mwaka wa mwanzo, baada ya hapo shamba litajiendesha lenyewe.

Watanzania nuksi, watakuja hata kukurekebisha kusema ni lao.

Ukweli ubaki kuwa ukweli ingawa ni mchungu.

Wewe ni mshirikina wala siyo bure.
 
Akili za mafisadi utazijua tu. Mwenzako anajaribu kusaidia his/her fellow countrymen /countrywomen bila hata chembe ya ubinafsi, wewe unamletea hadithi za kuleta foreigners. Hivi hamuoni aibu au dhambi jirani zenu wanapokosa hata hela ya mkate kwasababu ya ufisadi wenu?

Shame on you.

Sikiliza kijana, nimeiona dunia, Tanganyika ni kwetu na Tanzania ndiyo usiseme.

Hapo kuna mutual benefit, si tu anataka kusaidia bali na yeye anataka kusaidiwa ulinzi wa bure ili shamba au eneo lake la shamba lisivamiwe na pia lisiwe msitu na awe ana save pesa za kufyekesha na au kulimisha msitu mara kwa mara, a atarudi kuwa kwa arrangement hii eneo lake litakuwa katika hali nzuri wakati wote.

Hapo hakuna msaada wa usamaria mwema, hapo kuna "scratch my back I'll scratch yours", na wala sio siri, labda hujamsoma vizuri, rudia tena kumsoma.

Mimi yangu ni maoni tu, tena maoni yangu yapo wazi kabisa, mwisho wa siku hanijuwi simjuwi, si yeye si hao anaopenda kuwasaidia.

Tanzania hii tuna safari ndefu sana ya kwenda.
 
Back
Top Bottom