Shamba Huko Usambara Lushoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shamba Huko Usambara Lushoto

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Jan 2, 2010.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Hello wana JF,

  Happy New Year!

  Kuna rafiki yangu yuko nje ya nchi anataka Shamba kama Heka 20 kwa ajili ya kujenga Lodge huko Lushoto Usambara.

  Naomba kujua itakuwa bei gani kwa hekari moja. Au naomba kujua ni vijiji gani au tarafa gani yenye mashamba.

  Je nikienda huko nimwone Afisa mtendaji Kijiji Au katibu Tarafa?

  Kutoka Tanga mpaka Lushoto ni km ngapi
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  nenda kwanza TIC Tz investment centre wana maeneo wameyainisha karibu nji nzima kwa ajili ya uwekezaji naamini na lushoto ni mojawapo, usipo ridhika nao nenda wizara ya utalii Mpingo house idara ya tourism development na wao watakupa maelezo ya kutosha na ya uhakika, ukienda huko kutana na serekali ya Kijiji na uwe makini usije ukalizwa

  good lack
   
 3. S

  Selungo JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa ningekushauri kuhangaika na upatikanaji wa ardhi kabla ya kwenda kuwaona jamaa wa TIC. Nijuavyo mimi Lushoto ni kati ya maeneo yanayokabiliwa na ufinyu wa maeneo ukilinganisha na idadi ya watu. Hivyo TIC lazima watakuuliza "Je, unalo eneo?".

  Ki jiografia Lushoto ni kati ya sehemu nzuri kuwekeza katika shughuli za utalii ila tatizo kubwa ni upatikanaji wa eneo linalotosha kwa shughuli kama hizo. Hii ni kwa sababu si rahisi kumpata mtu mmoja mwenye eneo la ekari 20, na aliye tayari kuliuza. Hivyo ili kupata eneo la kiasi hicho, ni lazima utafute watu tofauti na wenye maeneo yaliyo sehemu moja ili upate jumla ya hizo ekari. Kwa maana hiyo hata bei kwa ekari ni lazima zitatofautiana, kulingana na aina ya mimea iliyopo kwa kila eneo.

  Kama utafanikiwa kupata eneo, kabla ya makubaliano ya kuuziana; Ni jambo la lazima kwanza kukutana na "BARAZA LA ARDHI LA KATA", ambalo hili litaagiza serikali ya kijiji husika kuchunguza endapo hakuna mgogoro wowote unaohusu umiliki wa eneo husika. Ikidhibitika hakuna (kimaandishi), basi endelea na taratibu za ununuaji wa eneo ukuhusisa wataalam wa sheria, ikiwa ni pamoja na mahakama katika eneo husika.

  Umbali kutoka Dar hadi Lushoto mjini kwa basi ni wastani wa saa 6. Na kutoka Lushoto mjini hadi huko vijini inategemea unakwenda kiji gani.

  Vile vile ningekushauri ukaangalia uwezekano wa kufanya shughuli hiyo USAMBARA MASHARIKI na hasa eneo la AMANI. Usambara Mashariki ni among WORLD HOTSPOT AREA interms of rich in biodiversity na ndipo ilipo NATURE RESERVE ya kwanza kwa Tanzania. Na pia ni one of the MAN AND BIOSPHERE RESERVE ambapo sasa wanakamilisha taratibu za eneo hili kuwa moja ya "WORLD HERITAGE". Yapo maeneo mengi pale Amani ambayo baadhi ya vijiji wanahitaji wawekezaji wa aina yako. Mfano vijiji vya Mgambo, Ubiri, Kwemwewe, Misalai na n.k. Umbali kutoka Dar hadi Muheza ni saa 4.


  Eneo la Amani lipo karibu sana na Pangani ambapo utalii wa fukwe za bahari unakuwa kwa kasi kubwa sana. Upande wa mashariki wa Amani ipo Saadan National Park, na upande wa kaskazini ipo Mkomazi National Park pamoja na Umba river game reserve. Mashariki ni visiwa vya Unguja na Pemba, ambapo watalii wengi huja na kuondoka kwa kutumia uwanja wa ndege wa Tanga au Pangani (Mwera air stip). Ni mwendo wa chini ya masaa mawili toka Pangani na ni chini ya saa moja kutoka muheza mjini.

  Kama lengo ni kujishughulisha na wageni watalii ni vyema kuzingatia "Combination of tour Packages" eg beach, wildlife, scenary, ecotours, culture, fevarouble weather n.k. East Usambara is an Ideal Place. Na hii itawapunguzia gharama watalii na hivyo wewe kuwa katika nafasi ya kupata wageni wengi.

  Nakutakia uwekezaji mwema.
   
 4. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Dear Prodigal Son and Selungo,

  Happy New Year!

  Very Thanks for useful information.

  I will go there and search a land.
   
Loading...