Shamba Heka 50 Linauzwa Kibiti

Lady Ra

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
879
990
Wadau,
Natumanini mko poa na mnaendelea vizuri na maisha. Nisiwachoshe sana, Jirani yangu anauza Shamba lake na details zake alizonipa ni kama ifuatavyo,

1) Kuhusu Kufika Shamba
Liko kibiti, njia ya kwenda kusini (Kilwa road) umbali wa Kilometa 173 kutokea Ubungo Mataa. Umbali huo unahusisha Kilometa 152 za lami mpaka kibiti kituoni kisha ni rough road ya kilometa 21 kutoka kibiti kituoni mpaka shambani. Kwa wanaotumia daladala ukitokea Mbagala nauli mpaka kibiti kituoni ni kiasi cha Tshs 5,000/= na ukishuka kituoni pale unachukua bodaboda kwa gharama ya Tshs 8,000/= mpaka shambani.

2) Kuhusu Shamba Lenyewe
Shamba halijawahi kulimwa kabisa hivyo ni pori, na litahitaji kusafishwa. Shamba lina ukubwa wa heka 50, yaani Heka 5 x heka 10 au Mita 350 x mita 700. Eneo lililopo shamba ni maarufu sana kwa kilimo cha Mihogo na Ufuta, ingawa wenyeji wanasema na mazao mengine pia yanakubali. Serikali ya Kijiji inatambua uwepo wa shamba hilo na inatambua pia mmiliki wa shamba hilo, na mauziano ya hilo shamba yatafanyikia hapohapo serikali ya kijiji.

Mwenye-shamba ni mkazi wa DSM, hivyo mnunuzi mtarajiwa akihitaji kuliona atatakiwa kupanga siku ambayo atakua huru hivyo wataenda shambani kwa gharama zilizotajwa pale juu (#1)

3) Bei
Shamba hili lenye heka 50 linauzwa kila heka moja ni 90,000/= na linauzwa lote kama lilivyo (Tshs 90,000 X 50heka = 4.5 Mil), bei hii ni kwa mujibu wa Muuzaji mwenyewe hivyo pengine ukimpigia mkielewana inazungumzika (inapungua).
Contacts zake ni 0684 477 150

Mimi ni mjumbe tu, nimefikisha ujumbe kama nlivyotumwa, wala sio dalali.
 
Nimependa sana description ya mauzo ya shamba .... big up and wish you success
 
Nimependa sana description ya mauzo ya shamba .... big up and wish you success

Ahsante Mkuu,

Nimejaribu kadiri ya uwezo wangu ili kupunguza maswali mengi. Naamini mnunuzi mwenye taarifa kamili ya shamba anakua katika nafasi kubwa ya kufanya maamuzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom