Shakira bado hajasema, na atasema, yaani mpaka aseme

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
26,091
68,365
Kweli mapenzi hayana cha ustaa wala umaarufu yakiamua kukunyoosha yanakunyoosha bila kujali ni mtu wa aina gani.

Ni wazi bado mwanamama Shakira anateswa na zimwi la penzi la Gerald Pique, kuzidi kumuongelea mara kwa mara kwenye interviews inadhihirisha bado anamuelewa sana mwamba, sijui mwanasoka huyu alimpa nini Shakira licha ya umaarufu wake.

Nachomkubali Pique ni mkimya, nampongeza kwa hilo ni tabia ya kiume haswa, tangu watengane 2022 Shakira ndio kinara wa kuyaongelea mahusiano yao. Shakira anadai penzi lake na Gerlad Pique limemfanya kumrudisha nyuma na kumuumiza vibaya kimapenzi pia hatamlipizia kisasi kwa kumuongelea kwenye nyimbo zake kama ambavyo amefanya kwenye nyimbo zake zilizopita.

G. Pique yeye hupenda kuongelea zaidi kuhusu watoto wao akihojiwa kuhusu mahusiano yake na Shakira.

Wanawake mkipenda sana ndio mnakuwa kama Shakira?


FB_IMG_17114650118301907.jpg

licensed-image.jpeg
 
Back
Top Bottom