Shakassaling Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shakassaling Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlenge, Mar 27, 2010.

?

Unadhani ni ipi hasa sababu ya JK kupembejea EAC?

Poll closed Apr 26, 2010.
 1. Sababu A: Hajui atendalo

  0 vote(s)
  0.0%
 2. Sababu B: Schadenfreude

  0 vote(s)
  0.0%
 3. Sababu C: Anajua mwenyewe

  0 vote(s)
  0.0%
 4. Sababu D: Hakuna sababu

  0 vote(s)
  0.0%
 5. Sababu A: Hajui atendalo

  0 vote(s)
  0.0%
 6. Sababu B: Schadenfreude

  0 vote(s)
  0.0%
 7. Sababu C: Anajua mwenyewe

  0 vote(s)
  0.0%
 8. Sababu D: Hakuna sababu

  0 vote(s)
  0.0%
 1. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Comrades & compatriots,

  What questions would you ask our beloved President, Jakaya Kikwete, if you would get a rare opportunity for one-to-one interview?

  JK is one of the most important presidents Tanzania had had. His speech to parliament kickstarting his presidency was a masterpiece. He won many accolades, including mine, for that speech, saying "at last, Tanzania have got the president Tanzania needs." There is nonetheless one issue that remains unclear.

  Attached is the questions I would ask Hon. Kikwete, if I had one-on-one interview.

  Regards,

  Mlenge

  NB: Your thoughts?
   

  Attached Files:

 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kumshakasali Kikwete
  

  Mwaka mmoja au miwili hivi tangu uwe Rais, Jakaya Kikwete ulihojiwa na Shaka Ssali, wa
  Sauti ya Marekani, ambaye alikuwa ziarani Tanzania. Mahojiano hayo yalirushwa na televisheni
  za Tanzania. Baada ya mdajala wa muda, Shaka Ssali alikuuliza Rais Kikwete utaje jambo moja
  tu la maana kuliko yote ulilolifanya ndani ya huo muda uliokuwa madarakani.
  Hapo Rais Kikwete ukaanza kutaja orodha ya ‘mafanikio', lakini Shaka Ssali akakwambia
  hahitaji kile alichokiita kwa Kingereza, "shopping list" ("Kiswahili mrefu") ya hayo ‘mafanikio',
  bali umtajie jambo moja unaloona utawala wako umelifanya mpaka muda huo.
  Ilibidi Mheshimiwa Kikwete utaje jambo moja kubwa unaloona utawala wako umelifanya, na
  utakumbukwa na kupata heshima kwa hilo toka uingie madarakani.
  Ujenzi wa sekondari za kata ndio jambo la maana kuliko yote Rais Kikwete na serikali yako
  ilikuwa imefanya mpaka mnaenda mitamboni, ndilo jambo ulilolisema kwa Shaka Ssali.
  Suala muhimu hapa ni kwamba mahojiano hayo uliyafanya na mtu wa televisheni ya nje, na huyo
  alipata fursa ya kukuhoji Rais ‘mtu kwa mtu'. Fursa hiyo adhimu na adimu ni vigumu kupatikana
  kwa kina sisi Waandishi ‘chinga' tuitwao pia ‘makajanja'; vigumu pia na hata kwa wale
  ‘wenyewe', mradi tu ni wa vyombo vya habari ‘madafu'.
  Ndio maana hapa pa kufikirika nakuuliza Rais Kikwete masuali yafuatayo. Najua tofauti na
  Shaka Ssali aliyepata majibu yake palepale, sitarajii kupata majibu ya haraka, ila ni muhimu kwa
  vile punde si punde utamaliza muda wako wa kuwako madarakani (miaka kumi?), kwa hiyo
  utataka ukumbukweje?
  Maswali yatakayotumika ni ya mfumo wa shakasali -- : Jibu moja tu -- bila shopping list

  ("Kiswahili mrefu") kwa kila suali, katika masuali yafuatayo yaliyokolezwa wino:
  1. Kwa mujibu wa hotuba zako Rais Kikwete unataka Tanzania iwe chini ya Shirikisho la Afrika
  Mashariki. Kisha umesaini mikataba ya kuidhinisha hilo. Ni kwa sababu ipi moja
  inayokufanya uamue hivyo, na si kuamua kuitoa Tanzania kwenye EAC ili iendelee kuwa
  huru na kuendelea kuwa ni Jamhuri?

  [Ili kuhakikisha jibu lako linakuwa bayana, jibu hilo haliwezi kuwa ‘wananchi walitaka baada ya
  kuwauliza kwa kutumia Tume ‘ya Wangwe'. Jambo hili ni lako wewe mheshimiwa Rais. Kwa
  hili tutakuvika medali ya pongezi, iwapo ni jambo jema kama unavyosisitiza mara kwa mara, au
  tutakunanga kwa nyimbo na misemo ya kukusimanga ikiwa litakuwa jambo baya kama
  tunavyoona sisi wananchi. Ikiwa si sisi, basi ni historia itakayafanya hivyo.]
  2. Mojawapo ya sababu zinazotolewa kana kwamba ndio sababu ‘halisi' ya Tanzania kupelekwa
  kwenye EAC ni kwamba kwenye moja ya zile awamu zilizopita, ufisadi ulikithiri, kwa hiyo njia
  mojawapo ya kunyamazisha kelele hizi za ufisadi dhidi ya taifa, ni kulifuta hilo taifa lenyewe.
  Sababu nyingine inayotolewa ni kwamba awamu yako inaendeleza hayo kwa vile wewe lengo
  lako lilikuwa ni kwamba siku moja uwe Rais. Ushakuwa Rais. Mwisho wa reli. Ndio maana
  unasaini mikataba ya kulifuta taifa ambalo bila hilo huwezi kuwa Rais, au basi huwezi kuwa
  Rais mwenye madaraka yaleyale kama vile kwenye taifa (vyama vya wanafunzi, vya michezo, na
  vinginevyo, navyo pia vina ma-Rais, lakini hawana madaraka kama uliyokuwa umekabidhiwa).
  Ni sababu ipi moja ambayo inakufanya usaini mikataba ya EAC ambayo inakupunguzia
  madaraka wewe (Rais wa Tanzania), Bunge na Mahakama vilivyo chini yako, madaraka
  ambayo ulisubiri muongo mzima na zaidi ili kuyapata?
  3. Moja ya mambo ambayo yanaleta taabu kuyaelewa ni kwamba uamuzi huo wa kuipeleka
  Tanzania EAC iwapo unatokana na wewe Rais Kikwete, pamoja na serikali yako, Chama Tawala
  CCM, na watu wako wa karibu, kwamba hamuelewi mnachokisaini, wala mnachokipembejea.
  Mnadhani EAC ni ‘mbuga' nyingine ya ‘ulaji', ambayo watu waliokosa ‘ulaji' majimboni mwao
  wanaweza kujipatia ulaji huo huko EAC. Hamjui kwamba hili ni tanuri, mtego wa panya kuingia
  aliyekuwemo na asiyekuwemo. Hii tuiite "Sababu A". Ikiwa si sababu "A", inatatanisha kujua
  kwamba iwapo basi itakuwa ni kwamba wewe Rais wetu Kikwete, unajua fika madhara, madhila
  na mateso unayotuletea Watanzania kupitia EAC. Kwa inda, chuki na jinsi usivyotupenda wala
  kutujali Watanzania tuliokuchagua uwe Rais wetu, umeamua ‘kututosa‘ kwenye mateso ya EAC
  unayojua vema yatatokea. Unajua kwamba wewe na watu wako wa karibu hamuezi kuathirika.
  Kwa roho mbaya tu umeamua kutusaliti Watanzania. Hii ni "Sababu B". Utaona mheshimiwa
  Rais, kwamba, inatuwia vigumu kukubali "Sababu A", kwa vile hotuba zako ni nyingi, ndefu,
  ambazo unasifia EAC. Zinakuwa vigumu kuamini kwamba unazisoma tu kwa vile zimeandaliwa
  na wasaidizi wako, pasi na wewe kuelewa na kukubaliana na yaliyomo. Wakati huohuo wengine
  wanasisitizia kwamba "mtu mwenyewe anachekacheka tu, si ndio hayo anawachekea hata wale
  wanaochukua madaraka yake mwenyewe kupitia EAC! Mkwere yake kucheza ngoma tu, na
  ‘Uswahili', vitu vya msingi kama kutetea taifa hata kama wale wengine watanuna, hawezi!". Hao
  wanaleta utani wa kikabila kwenye masuala nyeti ya taifa. Tunawapuuza. Kwa upande wa
  "Sababu B" napo tunashindwa kuamini. Uliingia madarakani ukitaka "maisha bora kwa kila
  Mtanzania". Ungekuwa hutupendi, unatuchukia, ungegombea kwa kampeni ya "Bora maisha
  kwa kila Mtanzania". Kwa hiyo hii "Sababu B" nayo tunaipuuza. Tuambie basi mhe. Rais ni
  nini hasa sababu moja ya wewe binafsi kuchukua hatua ya kuipeleka Tanzania hatimaye
  kwenye EAC. Hii ndio "Sababu C", sababu halisi, ambayo itaondoa ‘manenomaneno'
  (Sababu A na Sababu B).

  Natanguliza shukrani.
  Ndimi,
  mfuasi wako mtiifu,
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mr President, how do you live with yourself?
   
Loading...