Shaka: Upinzani usimtafute mchawi, ujitafakari na kujipanga upya

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Morogoro kimevitaka vyama vya upinzani kujipima kisiasa, kutafakari na kujitathmini hatimaye vibaini mapungufu yao na kujua kwanini wanachama na viongozi wake wakiwemo wabunge na madiwani wanavihama vyama hivyo na kurudi CCM.

CCM kimesema dawa ya vyama hivyo si kulalamika, kumtafuta mchawi na kutunga uongo, bali vichemshe bongo na kutazama mahali walipojikwaa badala ya pale wanapodondokea.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu wakati akimkaribisha mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa kuwapokea na kuwakabidhi kadi viongozi na wanachama wa chama vya upizani waliojiunga na CCM wilaya ya Ulanga Mkoani hapa.

Shaka alisema CCM kilitumia muda mwingi kutafakari, kujitathmini na kujipima kwanini kumekuwepo na shutuma dhidi ya serikali na watendaji wake hatimaye kikapata majawabu ambayo yakawafanya wajipange, kutekeleza na kuchukua hatua.

Alisema kazi ya chama chochote makini cha siasa ni kujikita kufanya uchambuzi, tathmini za kitaalam, tafiti za kiuchumi na kijamii ili kuona kama bado kinakubalika , kinashambuliwa au hakitimizi wajibu wake kwa umma.

"Yapo mambo CCM iliyabaini na kuanza kuchukua hatua haraka .Tuliona kuna ombwe la kukosekana tunu ya utendaji na ufanisi. Kulikithiri vitendo vya rushwa na ubadhirifu. Mmongonyoko wa maadili, ufisadi na kupungua nidhamu ya kazi " Alisema Shaka

Alisema CCM haikutafuata mchawi wala viongozi wake kunyoosheana vidole vya lawama , badala yake iliposema ni lazima tukubali kujikosoa, kujivua gamba, kukomesha ufisadi, rushwa na usaliti , wapo walioona mambo hayo yasingewezekana lakini yakafanyika kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM 2015/2020.

Katibu huyo wa CCM alisema wananchi walishachukizwa na kukithiri ufisadi, kuzorota kwa huduma bora za kijamii, kuchomoza maonevu , manyanyaso pia kukosekana kwa kwa haki kwenye baadhi ya vyombo za kisheria na kimamlaka.

Aidha alisema ujasiri wa Rais Dk John Magufuli katika kusimamia kwake utelelekezaji wa ilani ya CCM , kumekisafisha chama na serikali ambapo wananachi wamejenga matumaini mapya kwa ccm huku upinzani ukikosa hoja na mashambulizi.

"Upinzani ni hoja na si mashambulizi dhidi ya wanaotawala. Kama malalamiko ya wananchi yanafanyiwa kazi, ufanisi unaaonekana huku sheria zikifuatwa na watendaji, ni lazima upinzani ufilisike na viongozi wake warudi CCM " Alisisitiza Shaka.

Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa Morogoro Sudi Mhando , aliwataka watendaji wa serikali katika vyombo vya dola na watumishi wa umma kwenye halmshauri za wilaya mkoani humu kutimiza wajibu wao ipasavyo kabla hawajawajibishwa.
IMG-20181121-WA0848.jpeg
 
Chapa kazi kijana, watasema sana wapinzani, kipigo uchaguzi serikali za mitaa 2019 kipo pale pale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom