Shaka kwa usalama wa vyakula Arusha

Shaka kwa usalama wa vyakula Arusha

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
858
Reaction score
131
0,,16164289_401,00.jpg

mbunge wa Ujerumani Ute Koczy

Kwa habari zaidi tembelea web WD chini


Shaka kwa usalama wa vyakula Arusha | Masuala ya Jamii | DW.DE | 09.11.2012

Kuna habari za kutia wasi wasi kwamba baadhi ya wakulima nchini Tanzania wanatumia vumbi la madini ya uraniumu ili kuhifadhia mazao yao kama vile nafaka na matunda. Kwa mujibu wa mbunge wa Ujerumani Ute Koczy .Mbunge huyo wa chama cha kijani nchini Ujerumani Ute Koczy ametahadharisha kwamba matumizi ya vumbi la madini ya Uranium kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya kilimo yanaweza kusababisha hatari kubwa kwa wakulima.
Kutokana na hatari kubwa iliyopo mbunge huyo amesema pana haja kwa serikali ya Tanzania kuchukua hatua, angalau kwa ,kutoa habari kwa ukamilifu, "Sisi tunaona pana umuhimu mkubwa kwa serikali ya Tanzania na taasisi mbalimbali kulishughulikia suala hilo.Serikali na taasisi zinapaswa kutoa habari kwa ukamilifu ili watu wajue ni nini kinaweza kutumika na nini kinapaswa kuachwa."
0,,4450469_4,00.jpg
Mkulima mkoani Arusha
Kwa muda wa miaka mingi mbunge huyo wa Ujerumani Ute Koczy ambae ni msemaji wa wabunge wa chama cha kijani juu ya masuala ya maendeleo amekuwa anafuatilia kwa undani shughuli zinazohusu uzalishaji wa madini ya uranium nchini Tanzania. Na hivi karibuni alikuwaa nchini Tanzania ambako aliweza kuijionea mwenyewe shughuli zinazohusu uzalishaji wa madini ya uranium . Kutokana na hatari ya vumbi la madini hayo linalotumiwa na baadhi ya wakulima nchini Tanzania, mbunge huyo ameandika barua kwa Shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia, na pia kwa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania. Jee ni nini hasa anata katika barua alizoandika? "Nionavyo mimi pana mambo ya kichini chini yanayotokea. Tunaingiwa wasiwasi tunaposikia kwamba wakulima nchini Tanzania wanaanza kutumia vumbi la madini ya uranium ili kuhifadhia mazao yao.Sasa tunaanza kujiuliza jee kinatokea nini nchini Tanzania? alisema mbunge huyo.
Mbunge huyo wa Ujerumani bibi Ute Koczy aliongeza kusema ni hatari kubwa kwa wakulima na kwa watu wengine nchini Tanzania kukaribiana na vumbi la madini ya uranium.
Aidha alisema mpaka sasa hakuna data na takwimu zinazofahamika juu ya viwango vya miali inayoweza kuwa hatari.Kuna habari zinazopingana juu ya hayo. Kutokana hali iliyopo mbunge huyo anataka kupigwa marufuku kabisa kwa matumizi ya vumbi la uranium nchini Tanzania.
Hata hivyo ni vigumu kwa mbunge huyo kusema ni kiasi gani cha vumbi la uranium kinachohusika kwa jumla. Lakini amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yameteoa tahadhari na shirika la nishati ya kiatomiki la Tanzania pia limethibitisha habari hizo.
Mwandishi:Mtullya abdu/Mahojiano Schmidt Andrea.
Tafsiri:Mtullya abdu.
Mhariri:Abdul-Rahman
 
Mimi nasema sio usalawa wa vyakula kwa watu wa Arusha tu, ni wasi wasi wa Taifa zima la Tanzania na watu wake, tunaweza kuasirika na kupata maradhi mabaya na uwezo wa kutibiwa ikawa hatuna.

Kumufuma kwa maradhi mabaya ndio hukuu , Watanzania tunakufa kwa mambo mengi tukiashilia janja la Umaskini wakupindukia , basi hufa kwa mavyakula mabovu na madawa mabovu yaingizwayo nchini bila ukaguzi wwte ule.

Hivi kweli tuna serekali sisi au tuna genge la mafisadi na wajilimbikiziaji wa mali na rasilimali za Umma?
hivi sasa Watanzania tatizo sio siasa ni hilaki ya maicha yalivyo tunamia.

Panapokuwa na maisha bora basi siasa huingia mitini, lakini hivi sasa watanzania tumenamiwa na maisha magumu imekuwa mfano wa harka ya kimbunga au mawimbi ya Bahari likitoka hili linakuja kubwa jingine.

viongozi wetu wao hutugawa kwa njia za kisiasa lakini yao na familia zao yanawaendea ,wenye kula hilaki ni sisi raia wakawaida, jikoni kalala Paka.

Imefika hadi wasio watanzania wanatupigia kelele kuhusu asari za afya zetu lakini viongozi wetu kimya , ama kweli samani ya raia wako viongozi wetu hawaijuwi wala kuiheshimu.
 
Hilo vumbi la Uranium wanalitowa wapi?
 
Kuna kaharufu kaujasusi wa kibiashara na kuharibiana soko la mauwa yanayokwenda ulaya.

Siiamini hii habari kuwa ni ya kitafiti.

Huyo mbunge usikute ana maslahi na kuagiza mauwa ya kenya na au anatumiwa. Wazungu wanakuchekea tu usoni lakini ni hatari kweli kweli inapokuja kwenye kulinda maslahi yao.

Haijanikalia sawa hii habari. Mpaka sasa siiamini.
 
Uranium ni radioactive element na wakati inapo under go half in tend ku emit mionzi ambayo ni hatari kwa afya kwa kuwa mionzi hii inaweza kusababisha kansa na pia inaweza kushambulia DNA na kubadili coding yake na kusababisha madhara kama Albinism na matatizo mengine! cha kushangaza ni kuwa haya mabaki ya uranium yanafika mikononi mwa watu wa kawaida? na uchimbaji upo safe kiasi gani? kama upo holela kiasi hiki kuna wasiwasi wa madini haya kuangukia mikononi mwa magaidi waktumia kutengeneza bomu la nuclear! hatari kwa taifa, hatari kwa dunia!
 
Je ni wakulima wote wa Tanzania au wa mikoa gani ya nchi? Nadhani kuna kitu kinapigiwa debe hapo.
 
Uchakachuaji ni mbaya hasa kwenye masuala ya chakula mimi nimenunua sembe imeandikwa japa ya nguvu processed by Monaban trading company ltd ila unatoa mbovu sana na pia hauna ladha kabisa.
 
Back
Top Bottom