Shairi ya Harusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shairi ya Harusi

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by eRRy, Mar 8, 2011.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wapendwa JF! Asalam Aleykum... Bwana Asifiwe!Kuna Rafiki yangu anafunga pingu za Maisha mwezi huu wa sita. Anahitaji shairi! Nisaidieni kwa hilo plz!:help:
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ulimkubalia nini wakati uliona ww huwezi kumtungia?? ni vema umwambie mapema kuwa umeshindwa!!
   
 3. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,602
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Nafumbua macho yangu, kukuangaza Kipenzi
  Waridi la moyo wangu, daima nitakuenzi
  asante kwa kuja kwangu, na kunipa lako penzi
  KARIBU mpenzi Wangu.Karibu moyoni mwangu

  Ni moyo wa namna gani, shujaa alokuwa nao
  Ule usiotamani, kupendwa na wapendao
  Mgumu Kiasi gani?, Usivutwe na Sumaku
  Nguvu Ilo Mapenzini, aijua hata Kuku
  SEMBUSE MIMI KABWELA, MTOTO WA KITANZANIA?.

  Uzuri wako Kipenzi, Mithili ya mbalamwezi
  Kwako nimeshikwa ganzi, kwa hakika sijiwezi
  Kwangu ondoa Simanzi, usihofu laazizi.
  Karibu Mpenzi wangu, Karibu Moyoni Mwangu

  Tumuombe Mwenyezi Mungu, ndoa atie baraka
  Atwondoshee Ukungu, Atujalie fanaka
  Niwe wako uwe wangu, siku zote kwa hakika!
  Karibu Mpenzi wangu, Karibu Moyoni Mwangu


  Mpenzi niko tayari, KWANI SABABU NINAYO!
  Mpenzi Sitahayari, KWANI NIA NINAYO!
  Na Tuianze Safari, KWANI UWEZO NINAO!
  Karibu Mpenzi wangu, Karibu Moyoni Mwangu


  Hilo Shairi ukilitumia Ukipata Mijihela yoyote huko ya Kutuzwa , Ukipenda Unikumbuke Mwanao. hahahah!
   
 4. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  GLN. ulikuwa umejiandaa nini?
  naomba unitungie la talaka
   
 5. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  AAh Susy! Mi nilimkubalia Kujitahidi Kuitafuta. Sikumpa Uhakika!
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  He dawa ya Babu haijafanyakazia BW unataka talaka. Tafadhali bana eehhh
   
 7. HARUFU

  HARUFU Platinum Member

  #7
  Jan 15, 2015
  Joined: Jan 21, 2014
  Messages: 24,740
  Likes Received: 27,744
  Trophy Points: 280
  Limetulia sana litawasaidia na wengineo watakaotaka shairi
   
 8. ladyfurahia

  ladyfurahia JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2015
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 13,648
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  mwambie kuwa hapa ndo kesha fika shairi tu atalipata aonane nami kwani anakiasi gani cha malipo ya hilo shairi?  kingine mwambie kuwa mm ni mama shughuli yaani MC kwenye sherehe mbalimbali na vileviile natengeneza keki na kadi za harusi asinikose kwenye hizo huduma pls usisahau mkuu
   
 9. ladyfurahia

  ladyfurahia JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2015
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 13,648
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  [h=3]shairi la harusi[/h]
  1.
  Msigeuze harusi, zikawa ni kivumbasi,
  Isirafu damisi, kwa shehe na makasisi,
  Mjukuu Ibilisi, kisirani na nuksi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  2.
  Ndoa ibada halisi, walisema waasisi,
  Jambo lataka kiasi, si kushibisha nafusi,
  Haliafiki Qudusi, mwingi wa kutanafusi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  3.
  Nikahi ni fahirisi, utangulizi hukisi,
  Lakudumu majilisi, pasiwe na wasiwasi,
  Kaskazi au kusi, vyote kupata nemsi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  4.
  Ikifanywa kwayo kasi, ya riha na anisi,
  Hutia doa jeusi, katika moyo mkwasi,
  Na kuleta uyabisi, kila kiungo kuhisi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  5.
  Harusi kama libasi, wawili ni mahsusi,
  Huleta hawa fususi, ya woto na utesi,
  Hawapendwi maharusi, kipendwancho ni harusi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  6.
  Hili lataka kiasi, hakika si wasiwasi,
  Isirafu si nemsi, muulize Abunuwasi,
  Na vitabu kadurusi, uone yake nakisi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  7.
  Harusi si kiharusi, jasho na wingi kamasi,
  Lataka bora ususi, mambo yenu kuasisi,
  Yasiyoleta nuksi, balaa nayo mikosi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  8.
  Harusi kitu halisi, hakichanganywi najisi,
  Haumo kwenye kamusi, uchafu nao utesi,
  Vinginevyo wasiwasi, na mgeni Ibilisi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  9.
  Haitaki kandarasi, kuufanya uhandisi,
  Huumeza ubinafsi, jumuiya kuasisi,
  Ikawa yenye wepesi, umoja na urahisi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  10.
  Humkataa chunusi, anayezusha mikosi,
  Huyakimbia maasi, kwa mbio zake farasi,
  Ili kutunza asasi, na kumkana ibilisi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  11.
  Huchongwa moja libasi, ya kukaa maharusi,
  Hawa zikatanafusi, huba ikawa msosi,
  Pendo kuwa ni hadithi, simulizi kila mosi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
  12.
  Ila ikiwa najisi, haitokwisha mikosi,
  Yatazidi na maasi, kusambaratika nafusi,
  Ndoa ikawa nuksi, na familia kuhasi,
  Harusi kama hadithi, huishia muflisi.
   
 10. ladyfurahia

  ladyfurahia JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2015
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 13,648
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  kwani kuna mtu anaweza kutunga shairi la talaka ndugu yangu?
   
Loading...