Shairi: Uwaneni

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
UWANENI

Uwaneni!
Chinjanen!
Chukianen!
Amani tena ya nini?.

Piganeni!
Shindaneni
Mwende vitani?
Nawasemesha wahuni.

Wamarekani!
Pia Irani!
Ni mashetani?
Mliopo duniani

Yenye amani
Tatizo nini?
Majukwaani
Mwaharibu amani.


Vingi vijembe
Vya wala sembe
Nyinyi mang'ombe?
Ziacheni zenu bangi.

Tushikaneni
Tuwaueni!
Kwani amani
Dawa yake ni upanga?.



SHAIRI-UWANENI!
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com

Saluti fasihi.
 
Waache wauwane bata,watakula mbatata!
Sisi tutawaweka kwapa,watashindwa kutapa

Wakikwea utata,watapata pakacha
Kisu kilichowakata,daima hawatakipata.
 
Waache wauwane bata,watakula mbatata!
Sisi tutawaweka kwapa,watashindwa kutapa

Wakikwea utata,watapata pakacha
Kisu kilichowakata,daima hawatakipata.
Kisu kilichowakata,daima hawatakipata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom