Shairi - Nimekufa

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,904
2,000
NIMEKUFA
Masikio yameziba, sisikii na sioni
Shingoni yamenikaba, nimelegea moyoni
Ni nani wa kunibeba, nyota ipo ukingoni
Nimekufa nimeoza, nasubiria kunuka.

Niache niwe mtumwa, penzi lake ni kifani
Hata kama nitasemwa, simwachi yeye jamani
Hata mate nikitemwa, namganda kifuani
Nimekufa nimeoza, nasubiria kunuka.

Mapenzi yake matamu, sijaona duniani
Wala haliishi hamu, ni kama nipo peponi
Hadi zaruka fahamu, pindi nipo nae ndani
Nimekufa nimeoza, nasubiria kunuka.

Nahisi ni malaika, amaetoroka mbinguni
Maana navyoridhika, yeye moto mimi kuni
Tena sitohangaika, kitu nakivuta ndani
Nimekufa nimeoza, nasubiria kunuka.

Jamani kupendwa raha, huyu si mweki shakani
Nala bata kwa furaha, na kuku kwenye sahani
Nitanunua silaha, nikate watu shingoni
Nimekufa nimeoza, nasubiria kunuka.

SHAIRI-NIMEKUFA
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom