Shairi: Kumbe ndoto

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
Kumbe ndoto

Naona Afrika, yatoka gizani
Nuru ikiwaka, tokea angani
Tukinawirika, hadi mashavuni
Ghafla nashituka, he ! kumbe ni ndoto.

Tunafaidika, toka migodini
Yazidi uzika, yetu madini
Miji yajengeka, hata vijijini
Nafungua macho, he ! kumbe ni ndoto.

Tunafurahika, Kuona amani
Inaongezeka, twapanda imani
Vita vya toweka, vile vya zamani
Nasikia pu pa, he! kumbe ni ndoto.

Yanaongezeka, majengo shuleni
Ina imarika, elimu nchini
Nasi yatoweka, huzuni rohoni
Mara watu wewe, he! kumbe ni ndoto.

Inapeperuka, bendera hewani
Madege yaruka, mengi angani
Nauli yashuka, asomudu nani
Hadi masikini, he! kumbe ni ndoto.

Una sahulika, ha umasikini
Njaa yafutika, hadi mitaani
Inaongezeka,ajira kazini
Mambo ni moto, ha!kumbe ni ndoto.

SHAIRI - KUMBE NDOTO.
MTUNZI - Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Brother mambo vp?mi nina mashairi yangu yakimapokeo(mavina)tunafanyaje ili ikiwezekana tutengeneze japo kitabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom