Shairi: Utenzi wa Waliobaki. Subirini huko huko Mlioenda

Shairi: Utenzi wa Waliobaki. Subirini huko huko Mlioenda

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,418
Reaction score
23,471
Utenzi wa Waliobaki. Subirini huko huko Mlioenda

Sisi tuliobaki, kura tutahakiki
Wizi hatutaki, uhuni hatubariki
Kura ni yetu haki, mashetani hatuwataki

Mitandao tutaitumia, habari kuwatumia
Hatutaki watu kuumia, haki kupigania
Matukio tutawarushia,habari kuwafikia
Nchi tutapigania, haki kujipatia

tuliobaki mtandaoni,tawaletea ya mtaani
Kila linalojiri nchini, tutawarushia hewani
Kutoka kila sehemu duniani, VPN kutusaidia
Habari kuwafikieni, mtandao mkirudishiwa

Tutatumia kwa nia njema, kuwapasheni habari
Kuwaletea yalo mema, na yale ya hatari
Akina baba na akina mama,tuwape habari.
Nchi imeinama, kukaribisha hatari.
 
Back
Top Bottom