Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 256
USINGOJE SIKU MIA
1. Mara utapo apishwa, Rais Tundu wa Lisu,
Walaka wa kukumbushwa, na kupa pia na kisu,
Siku mia ukipishwa, za kuondoa kukusu,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
2.Watu wanaangamia, mifuko imetoboka,
Rushwa imetukalia, viongozi wanafoka,
Wawekezaji huria, wote wanataabika,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
3.Sijenge miundombinu, jenga afya za watu,
Uchumi sitwae kwenu, rudisha thamani zetu,
Wezi wote toka TANU, maridhiano ya watu,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
3.Wachunguze vyeti feki, wape na mafao yao,
Walitumika kwa haki, jali uzoefu wao,
Wape zao sitahiki, si mbwa ni watu hao!
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
4.Anza na rasmu yetu, katiba ya Warioba,
Mikoa wilaya yetui!!wafyeke wakuu baba,
Punguza wizara zetu, ata zikifika saba,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
5. Wafungwa wa kisiasa, nazo kesi za visasi,
Sheria zisizo sasa, fungua haki na nafsi,
Mafao wanasiasa, yapunguzeni kiasi,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
6. Usingoje Siku Mia, fungua ofsi nayo,
Wasomi wamepotea, warudishe wape moyo,
Sijenge kama kichaa, watuwo piga mihayo,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
7. Warueishie mapato, vijiji sio mijini,
Wakulima wape pato, wauze wawe peponi,
Kwa kipindi cha mpito, wazee wako motoni!
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
8. Ondoa mipango feki, rudisha miradi yetu,
Cheza kasi kama beki, na ongozeni kwa haki,
Usikivu ndio haki, shaurika kila kitu,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
9. Ushindi umeshapata, wasubiri kuapishwa,
Sahau yaliyopita, watesi wapo wawashwa,
Mungu mahala kipita, mwanadamu hupandishwa,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
10. Leta elimu taifa, ondoa elimu Kata,
Afya watu wakufa, matibabu wamefuta,
Yafatilie maafa, yote yaliyotukuta,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
11. Mazao ya biashara, yameibwa wazi wazi,
Wanakera wanakera, wanakera hawa wezi,
Tunga ya kilimo Sera, ondoa utandawizi,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
12. Wekezeni kwa viwanda, vya mazao wakulima,
Ukata tutaushinda, na wote twende kulima,
Watalima kwa kupenda, kiondoa takirima,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
13. Urejeshe uongozi, kwenye kanda na mapato,
Bila kufanya ajizi, mikoa ipige futo,
Wilayani pana wizi, uchawi, rushwa, fukuto,
Usingoje Siku mia, yaondoe haya Lisu.
14. Zipunguzeni nafasi, kazi za kugawiana,
Walopeana ofisi, watoe weka vijana,
Ondoani ukakasi, ajira kupatikana,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
15. TANU ilikuwa yetu, rudisha viwanja vyetu,
Rejesha ofisi zetu, tupeni majengo yetu,
Rudisha na tunu zetu, pia na mashamba yetu,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
16. Ulevi wa madaraka, viongozi vyeti feki,
Piga kazi kwa haraka, Uhuru utamalaki,
Wazee kuang'atuka, hawaiwezi mikiki,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
17. Tenda haki kwa walimu, ikubali taaluma,
Kriato waislamu, wapi haki si huruma,
Zivunje vunjeni timu, za CCM dhuluma,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
18. Nendeni kwenye wilaya, nafasi uzipunguze,
Acheni watu uriya, wangio uwapoteze,
Na viongozi wa kaya, na wazee uwapoze,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
19. Jenga kipato cha watu, reli haijengi mwili,
Jenga majengo ya watu,
Barabara sio dili,
Jaza mifuko ya watu, siwaibie kubali,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
20. Chunguza gereza zetu, zilizojaa mateso,
Kumbuka wafungwa wetu, mahakama utakaso,
Waenzi wahenga wetu, waliolionja teso,
Usingoje Siku Mia, yaondoe haya Lisu.
~Linaendelea~
Linaandikwa na S.M. P. Kijoka