Sungurampole
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 984
- 205
Hakika hizo ni tungo za zamani sana na shairi hilo la nimeachiwa machela mimi na rafiki yangu lilitungwa na mshairi maarufu sana kutoka Ikwiriri Rufiji kwa jina ni al marhum SHAABAN MUSA MKADARU. Ni lilitoka katika gazeti la ngurumo la taarih 26 April 1968 na kisa hicho ndio kisa kilichochukua muda mrefu sana katika magazeti ya tanganyika na kilifungwa mwaka 1975.Ndugu zangu liko shairi moja niliwahi kusimuliwa zamani. Kwa bahati mbaya aliyekuwa anasimulia alikuwa mlevi mmoja na pia mimi nilikuwa mdogo sasa sikumuuliza jina la shairi wala mtunzi wake lakini atakuwa moja wa malenga wa siku nyingi.. Ninachkumbuka ni ujumbe wa shairi lile kuwa walikuwepo wavuvi wakivua wakaona watu wamebeba maiti na kama ilivyojadi ya waafrika nao wakajiunga ili kusaidiana kubeba baada ya kwenda muda wakibadilishana mara wakajikuta wako peke yao wavuvi na hawajui maiti ni ya nani, kafa na nini na wala anenda kuzikwa wapi? ..
Nimejitahidi kulitafuta sehemu nyingi lakini sijafanikiwa kulipata
naomba msaada wa yoyote anayelikukbuka - jina rasmi na/au mtunzi
Hakika hizo ni tungo za zamani sana na shairi hilo la nimeachiwa machela mimi na rafiki yangu lilitungwa na mshairi maarufu sana kutoka Ikwiriri Rufiji kwa jina ni al marhum SHAABAN MUSA MKADARU. Ni lilitoka katika gazeti la ngurumo la taarih 26 April 1968 na kisa hicho ndio kisa kilichochukua muda mrefu sana katika magazeti ya tanganyika na kilifungwa mwaka 1975.
Waliojitahidi kumpa majibu walikuwa pamoja na Sihiana Swalehe (madevu) wa Buguruni sokoni, Mzee Khalidi mtipa (ngondanee) wa Kibiti refiji, Shaaban Robert wa tanga, Saidi m Nyoka wa Tandika tambuka reli, Juma Maganga (Joka kuu) kutoka tabora, Saidi Sudi Andanenga (sauti ya kiza) wa kinondoni shamba na wengine.
Nataliweka jamvini mara nikinafasika inshallah
Ahsante Barubaru,Hakika hizo ni tungo za zamani sana na shairi hilo la nimeachiwa machela mimi na rafiki yangu lilitungwa na mshairi maarufu sana kutoka Ikwiriri Rufiji kwa jina ni al marhum SHAABAN MUSA MKADARU. Ni lilitoka katika gazeti la ngurumo la taarih 26 April 1968 na kisa hicho ndio kisa kilichochukua muda mrefu sana katika magazeti ya tanganyika na kilifungwa mwaka 1975........Waliojitahidi kumpa majibu walikuwa pamoja na Sihiana Swalehe (madevu) wa Buguruni sokoni, Mzee Khalidi mtipa (ngondanee) wa Kibiti refiji, Shaaban Robert wa tanga, Saidi m Nyoka wa Tandika tambuka reli, Juma Maganga (Joka kuu) kutoka tabora, Saidi Sudi Andanenga (sauti ya kiza) wa kinondoni shamba na wengine.....Nataliweka jamvini mara nikinafasika inshallah

Kwa hakika namelitafuta hapa katika maktaba yangu lakini silioni ila nimeagiza ahali zangu waliangalie huko Zanzibar kwenye mktaba yangu pia na nikilipata nitaliweka hadharani inshallah.

Ngojeni nikupe Beti chache ninanzoweza kuzikumbuka

1.Moja mbili tatu nne, namba tano siiioni,

Bwana mtengenezaji, nakuomba samahani,

Nipe kiliba cha maji, kinipooze kooni,

Tumeachiwa machela mimi na rafiki yangu.

2.Kwetu kumetungwa mila, tuseme au sheria,

Ukiyaona machela, Ni wajibu kupokea,

Huku ukijilamala, Na watu kusaidia,

Tumeachiwa machela, mimi na rafiki yangu.

.Si mgonjwa wakusema, Na wala si wa kupumua,

Kumbe yule ni maiti, Wenzetu wametuachia,

Tumeachiwa machela mimi na Hasani wangu.

Hizo ni baadhi tu (beti ya kwanza, pili na nyingine ambazo Marhum Shaaban Mussa Mkadaru wa Ikwiriri Rufiji alitunga.

Nitawaletea inshallah mara nitakapo zipata.

Dr Hamza Yousuf Al Naamaniy(Barubaru)

154/ martaj ,Umm Hays ,

Doha, Qatar
Ahsante Barubaru,
Umenikumbusha mbali na kunikumbusha kisa mimi kuwa mpenzi sana wa mashairi kwani watunzi hawa walikuwa wajuzi kwelikweli. Naona umetaja baadhi ya magwiji walomjibu, Je ulibatika kukutana au kufahamu baadhi ya hao magwiji?, Unajuwa nimekuwa najiuliza kutokana na mkabala wa dhiki na kubadika kwa mfumo wa kuwasilisha mashairi magazetini nahisi kama watunzi bora wengi ama wameamua kukaa kimya, au hawatumii vyombo vya habari kutoa tungo zao kama zamani. Pia vipindi kama mbinu za kiswahili, mashairi yetu nk vilikutanisha wengi kirahisi sana.