Shairi: Nimeachiwa machela...

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Ndugu zangu liko shairi moja niliwahi kusimuliwa zamani. Kwa bahati mbaya aliyekuwa anasimulia alikuwa mlevi mmoja na pia mimi nilikuwa mdogo sasa sikumuuliza jina la shairi wala mtunzi wake lakini atakuwa moja wa malenga wa siku nyingi.. Ninachkumbuka ni ujumbe wa shairi lile kuwa walikuwepo wavuvi wakivua wakaona watu wamebeba maiti na kama ilivyojadi ya waafrika nao wakajiunga ili kusaidiana kubeba baada ya kwenda muda wakibadilishana mara wakajikuta wako peke yao wavuvi na hawajui maiti ni ya nani, kafa na nini na wala anenda kuzikwa wapi? ..

Nimejitahidi kulitafuta sehemu nyingi lakini sijafanikiwa kulipata

naomba msaada wa yoyote anayelikukbuka - jina rasmi na/au mtunzi

Sungurampole

Na mimi niliwahi kusimuliwa ila nimesahau jina na mtunzi lakini nakumbuka jibu la kitendawili chenyewe. Nitajaribu kuulizia zaidi. Ni muda mrefu sijafuatilia habari za washairi lakini nadhani kina Koja Kuu, Sauti ya Kiza, Udogo si Hoja, Yoba kama bado wapo wanaweza kutusaidia.

Mwanangu

ndumbayeye, mwnangu na maelenga shukhrani vipi tunaweza kupata beti zake? - mimi lilinikonga moyo sana nilipokuja tafakari nikiwa mtu mzima

Ndugu zangu liko shairi moja niliwahi kusimuliwa zamani. Kwa bahati mbaya aliyekuwa anasimulia alikuwa mlevi mmoja na pia mimi nilikuwa mdogo sasa sikumuuliza jina la shairi wala mtunzi wake lakini atakuwa moja wa malenga wa siku nyingi.. Ninachkumbuka ni ujumbe wa shairi lile kuwa walikuwepo wavuvi wakivua wakaona watu wamebeba maiti na kama ilivyojadi ya waafrika nao wakajiunga ili kusaidiana kubeba baada ya kwenda muda wakibadilishana mara wakajikuta wako peke yao wavuvi na hawajui maiti ni ya nani, kafa na nini na wala anenda kuzikwa wapi? ..

Nimejitahidi kulitafuta sehemu nyingi lakini sijafanikiwa kulipata

naomba msaada wa yoyote anayelikukbuka - jina rasmi na/au mtunzi
Hakika hizo ni tungo za zamani sana na shairi hilo la nimeachiwa machela mimi na rafiki yangu lilitungwa na mshairi maarufu sana kutoka Ikwiriri Rufiji kwa jina ni al marhum SHAABAN MUSA MKADARU. Ni lilitoka katika gazeti la ngurumo la taarih 26 April 1968 na kisa hicho ndio kisa kilichochukua muda mrefu sana katika magazeti ya tanganyika na kilifungwa mwaka 1975.

Waliojitahidi kumpa majibu walikuwa pamoja na Sihiana Swalehe (madevu) wa Buguruni sokoni, Mzee Khalidi mtipa (ngondanee) wa Kibiti refiji, Shaaban Robert wa tanga, Saidi m Nyoka wa Tandika tambuka reli, Juma Maganga (Joka kuu) kutoka tabora, Saidi Sudi Andanenga (sauti ya kiza) wa kinondoni shamba na wengine.

Nataliweka jamvini mara nikinafasika inshallah

Mkulu Br,
ukiliiweka weka na majibu aliyopewa na Hasa ya SHABAAN ROBERT na SAUTI YA KIZA tafadhali

wakuu wangu nashukuru sana kwa majibu nasubiri kwa hamu nilipate kwa ukamilifu wake..juhudi zangu za siku nyingi zitakuwa zimezaa matunda

Kwa hakika namelitafuta hapa katika maktaba yangu lakini silioni ila nimeagiza ahali zangu waliangalie huko Zanzibar kwenye mktaba yangu pia na nikilipata nitaliweka hadharani inshallah.

Ngojeni nikupe Beti chache ninanzoweza kuzikumbuka

1.Moja mbili tatu nne, namba tano siiioni,
Bwana mtengenezaji, nakuomba samahani,
Nipe kiliba cha maji, kinipooze kooni,
Tumeachiwa machela mimi na rafiki yangu.

2.Kwetu kumetungwa mila, tuseme au sheria,
Ukiyaona machela, Ni wajibu kupokea,
Huku ukijilamala, Na watu kusaidia,
Tumeachiwa machela, mimi na rafiki yangu

.Si mgonjwa wakusema, Na wala si wa kupumua,
Kumbe yule ni maiti, Wenzetu wametuachia,

Tumeachiwa machela mimi na Hasani wangu.

Hizo ni baadhi tu (beti ya kwanza, pili na nyingine ambazo Marhum Shaaban Mussa Mkadaru wa Ikwiriri Rufiji alitunga.

Nitawaletea inshallah mara nitakapo zipata.

Dr Hamza Yousuf Al Naamaniy(Barubaru)
154/ martaj ,Umm Hays ,
Doha, Qatar

Hakika hizo ni tungo za zamani sana na shairi hilo la nimeachiwa machela mimi na rafiki yangu lilitungwa na mshairi maarufu sana kutoka Ikwiriri Rufiji kwa jina ni al marhum SHAABAN MUSA MKADARU. Ni lilitoka katika gazeti la ngurumo la taarih 26 April 1968 na kisa hicho ndio kisa kilichochukua muda mrefu sana katika magazeti ya tanganyika na kilifungwa mwaka 1975........Waliojitahidi kumpa majibu walikuwa pamoja na Sihiana Swalehe (madevu) wa Buguruni sokoni, Mzee Khalidi mtipa (ngondanee) wa Kibiti refiji, Shaaban Robert wa tanga, Saidi m Nyoka wa Tandika tambuka reli, Juma Maganga (Joka kuu) kutoka tabora, Saidi Sudi Andanenga (sauti ya kiza) wa kinondoni shamba na wengine.....Nataliweka jamvini mara nikinafasika inshallah
Ahsante Barubaru,

Umenikumbusha mbali na kunikumbusha kisa mimi kuwa mpenzi sana wa mashairi kwani watunzi hawa walikuwa wajuzi kwelikweli. Naona umetaja baadhi ya magwiji walomjibu, Je ulibatika kukutana au kufahamu baadhi ya hao magwiji?, Unajuwa nimekuwa najiuliza kutokana na mkabala wa dhiki na kubadika kwa mfumo wa kuwasilisha mashairi magazetini nahisi kama watunzi bora wengi ama wameamua kukaa kimya, au hawatumii vyombo vya habari kutoa tungo zao kama zamani. Pia vipindi kama mbinu za kiswahili, mashairi yetu nk vilikutanisha wengi kirahisi sana.

Kwa hakika namelitafuta hapa katika maktaba yangu lakini silioni ila nimeagiza ahali zangu waliangalie huko Zanzibar kwenye mktaba yangu pia na nikilipata nitaliweka hadharani inshallah.

Ngojeni nikupe Beti chache ninanzoweza kuzikumbuka

1.Moja mbili tatu nne, namba tano siiioni,

Bwana mtengenezaji, nakuomba samahani,

Nipe kiliba cha maji, kinipooze kooni,

Tumeachiwa machela mimi na rafiki yangu.

2.Kwetu kumetungwa mila, tuseme au sheria,

Ukiyaona machela, Ni wajibu kupokea,

Huku ukijilamala, Na watu kusaidia,

Tumeachiwa machela, mimi na rafiki yangu.

.Si mgonjwa wakusema, Na wala si wa kupumua,

Kumbe yule ni maiti, Wenzetu wametuachia,

Tumeachiwa machela mimi na Hasani wangu.

Hizo ni baadhi tu (beti ya kwanza, pili na nyingine ambazo Marhum Shaaban Mussa Mkadaru wa Ikwiriri Rufiji alitunga.

Nitawaletea inshallah mara nitakapo zipata.

Dr Hamza Yousuf Al Naamaniy(Barubaru)

154/ martaj ,Umm Hays ,

Doha, Qatar

hongera sana kwa kumbukumbu nzuri ulizotupatia wengi wao hatukuwepo katika zama hizo kwani umri ulikuwa hauturuhusu...

Asante kwa muadhama, barubaru ninakupa
Kwa kazi iliyo njema, na kumbukumbu kutupa
Utatukuka daima,ni heshima ninazokupa
Aliyeachwa machela,katupa kisa kizuri

Ahsante Barubaru,

Umenikumbusha mbali na kunikumbusha kisa mimi kuwa mpenzi sana wa mashairi kwani watunzi hawa walikuwa wajuzi kwelikweli. Naona umetaja baadhi ya magwiji walomjibu, Je ulibatika kukutana au kufahamu baadhi ya hao magwiji?, Unajuwa nimekuwa najiuliza kutokana na mkabala wa dhiki na kubadika kwa mfumo wa kuwasilisha mashairi magazetini nahisi kama watunzi bora wengi ama wameamua kukaa kimya, au hawatumii vyombo vya habari kutoa tungo zao kama zamani. Pia vipindi kama mbinu za kiswahili, mashairi yetu nk vilikutanisha wengi kirahisi sana.

Hakika mimi ni mmoja wa wapenzi wakubwa sana wa mashairi tokea nasoma darsa la tisa(form1) nilianza kutunga mashairi na hao niliokutajia wote nawajua.

Na Huyo Marhum Shaaban Mussa Mkadaru nimefika mpaka kumzika kwao huko Ikwiriri km takriban 200 kutokea dar es Salaam njia kuelekea Mtwara.

Nimezika akina Said Nyoka wa tambuka reli na wengine ninawasiliana nao mpaka leo. Kwani mie ni mmoja wa walezi wa chama cha washairi Tanzania.

Nitaliweka hilo shairi pindi nikilipata.

Assalaam Alaykum,
Mimi ni mgeni katika jamiiforums. Nilijiunga majuzi. Nilifurahi sana kuona wadau wa mashairi na mimi pia napenda mashairi na pia ni mshairi. Shairi hilo la Machela nalikumbuka vizuri sana na pale alipohojiwa redioni kuhusu shairi hili.
Watunzi wa zamani bado tunawakumbuka. Nilisoma Dodoma Secondary School na kumaliza Form IV mwaka 1964. Dodoma nilisoma na watoto wa Mshairi maaruf marehemu Mahmood Hamdouny (Jitukali) na kutoka kwake nilijifunza kutunga mashairi kwa vina na kwa mizani.
Shairi langu la kwanza kwenda hewani ilikua katika mwezi wa Ramadhani 1962 (KARIBU MWEZI WA TOBA, MTUKUFU RAMADHANI). Halafu nikaondoka Tanzania 1965 kuja huku Arabuni na mpaka leo naishi hapa Jeddah. Nimerudia kutunga mashairi na kupeleka TBC . Shairi langu la kwanza mwaka huu redioni ni kuhusu URAIA PACHA na mengine mengi.

Zamani nakumbuka mashairi mazuri sana kama lile la marehemu Khamis Amani (Nyamaume) MKOKO MTI WA KALE. Mashairi mengine ya watu wengine ni URUDI KWAKO TUNDUNI, MBAYUWAYU NDEGE WANGU,

KIUMBE NIPE NIKUPE, HICHO JAMAA KITU GANI, MUNGU TUMEKOSA NINI, VIUMBE WA USUMBURA, n.k.

Ndugu yenu,
Abdallah Bin Eifan (Kinyamkera).
Jeddah, Saudi Arabia.

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom