Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
CHETI MWATAKA CHA NINI
1)Ingelikuwa elimu,iwekwe karatasini.
Ingelikuwa si ngumu,watu shindwa maishani.
Ingelikuwa ni sumu,ung'atwapo unyayoni. mwataka cheti cha nini,ndicho kifanyacho kazi ?
2)ingelikuwa ni cheti,chafanya kuwa imara.
Ingelikuwa bahati,wala siyo masikhara.
Isingetia vidoti,na kuharibu taswira.
mwataka cheti cha nini,ndicho kifanyacho kazi ?.
3)ingelikuwa uwezo, unapimwa wa shuleni.
Ingekuwa hamnazo,wameishia shimoni.
Ingekuwa si katazo,sote tuvijaze ndani.
Mwataka cheti cha nini,ndicho kifanyacho kazi.
4)ingelikuwa si unga,hivi mngesema nini.
Ingekuwa kujidunga,kuna tija duniani.
Ingekuwa ni mpunga,upikwao baharini.
Cheti mwataka cha nini,ndicho kifanyacho kazi ?
Shairi=CHETI MWATAKA CHA NINI ?.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arumeru.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com