Shairi: Kwanza kaleta ndege, sasa meli

Bin Eifan

New Member
Sep 22, 2018
3
5
Hotuba yake ya Mwanza, ya Raisi Magufuli,
Ndege ameleta kwanza, sasa ataleta meli,
Hakujali kila kinza, Raisi katawakali,
Kwanza ndege sasa meli, Raisi twampongeza.

Raisi twampongeza, daima kwenye shughuli.
Nchi ameiangaza, tunaona hadi mbali,
Jua limeshachomoza, mwangaza kila mahali,

Meli zitaleta kheri, na kupunguza ajali,
Zitaondoa hatari, mizigo zitahimili,
Shida zote za safari, watu walistahamili,

Chato imeleta mwana, mwana usiku halali,
Mwana huyu kakazana, ili iwe nzuri hali,
Mwana kaweka bayana, kwamba nchi ina mali,

Tanzania ni tajiri, tazama maliasili,
Mengi yameshadhihiri, yalofungiwa kufuli,
Rais mwenye dhamiri, katuongeza akili,

Nchi inayo madini, tena madini asili,
Yenye bei duniani, na thamani iloghali,
Vipi nchi masikini, nani atajibu swali ?

Tunangojea treni, Rais katoa kauli,
Mzee hana utani, amefanya jedwali,
Hata hao wapinzani, wengi wameshakubali,

Tunaona madaraja, hayakuwepo awali,
Itakua ni faraja, kwa magari ni sahali,
Hakuna cha ngojangoja, Magufuli ni mkali,

Nyerere alitabiri, kuja kwa Msema kweli,
Sote sasa tunakiri, huyo mtu kawasili,
Jina lake mashuhuri, John Pombe Magufuli,

Kimasomaso mwanangu, Atakulinda Jalali,
Watakufa kwa uchungu, mahasidi majahili,
Hapa ndio mwisho wangu, chereko kila pahali,

Abdallah Bin Eifan (Kinyamkera)
Jeddah, Saudi Arabia,
 
Weekend njema mkuu
 
Back
Top Bottom