Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Salamu kwenu,

Kumekuwa na kelele nyingi kuwa ndege zetu hazina maana yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Watu wanaenda mbali zaidi kuhoji ikiwa flyovers za Dar es Salaam zina umuhimu wowote kwa watanzania waishio vijijini, mikoani huko.

Ukiangalia hizi hoja, unapata picha mbili. Ya kwanza ni kuwa ni kweli hawajui umuhimu wake na picha ya pili ni kuwa wanajua ila wameamua kupotosha. Picha zote mbili zinao wahusika, yaani wapo wasiojua na wapo wanaojua ila wameamua kupotosha. Kwa faida ya wote tuchambue kama ifuatavyo:

Utangulizi
Kujenga uchumi imara sio kazi rahisi. Ni kazi inayohitaji weledi na uwekezaji janja (smart investment) pamoja na mazingira wezeshi kiuchumi. Kufikia uchumi mzuri sio kazi ya muda mfupi ingawa matokeo chanya yanaweza kuonekana ndani ya muda mfupi Kama miaka mitano hivi. Haya yanakuwa ni viashiria kuwa tupo kwenye mstari sahihi (right track).

Kwanini watu huona kuwa flyovers na ndege haziwasaidii chochote?
Wanadamu tuna asili flani ya ubinafsi. Unataka uone wewe Kama wewe umefaidikaje. Aidha ukiacha ubinafsi, Ni kweli kuwa kwa macho ya kawaida, mfanyakazi atataka kuona mshahara mnono, mkulima atataka pembejeo, barabara ya uhakika ya kusafirisha mazao yake na soko la uhakika. Mwanafunzi atataka elimu Bora, vifaa vya kujifunzia na mazingira bora ya kujisomea. Watu wanataka huduma bora za afya kwa kuwa na vituo vya afya karibu yao, hospitali nzuri zenye vifaa na wataalamu wa kutosha. Hivyo matarajio yao Ni hivyo vitu kutimizea, na kwa hakika hivyo ndivyo serikali inapaswa kufanya.

Kwanini flyovers na ndege ni muhimu kwa watanzania wote hata kwa wale waishio nje ya Dar es Salaam na vijijini?

1. Flyovers
Dar es Salaam ni mji wa kibiashara na ndio mji wenye watu wengi zaidi Tanzania. Dar es Salaam ndio mji iliko hospitali ya taifa. Kila siku maelfu ya magari huongia Dar es Salaam kuleta wafanyabiashara wa ndani na nje, wagonjwa walioshindikana huko mikoani, watalii hasa wa ndani na bidhaa za mashambani.

Unapokuwa na msongamano mkubwa barabarani ni kuwa unapoteza muda mrefu kupeleka bidhaa sokoni, mgonjwa hospitalini na kuwahi kazini kwaajili ya kuwahudumia watanzania. Unapoondoa kero hiyo unakuwa hujamsaidia tuu mtu aishiye Dar Bali umemsaidia mkulima aliyeleta mazao yake manzese au kariakoo aharikishe biashara yake, mgonjwa aliyetoka mkoani kuwahi hospitali na mfanyakazi kuwahi kazini. Hapa utaokoa gharama za mafuta, muda na maisha ya mgonjwa. Pia utaongeza vivutio vya utalii na kupendezesha mji.

Ndege
Ndege zinarahisha usafiri wa ndani ya nchi. Unafika popote nchini ndani ya muda mfupi. Bibi akiumwa na kuzidiwa kule ikungi, mnachangishana anaenda sehemu ndege inapotua, huyoo anawahishwa hospitalini.

Uwepo wa usafiri wa ndani was uhakika unawafahya watalii waongezeke na hivyo Kukuza pato la taifa. Kuwa na ndege yenu (national carrier) inayofanya safari za nje inachangia sana kuongeza pato la taifa kwani watalii watalipa nauli jwa fedha za kigeni ambazo zitaingia Tanzania na watalipa fedha za kigeni wanapoingia hapa kufanya utalii. Hiyo itakuza ajira nchini kwa waongoza watalii, madereva, wenye hoteli, migahawa na orodha inaendelea.

Mazingira hayo yanatengeneza kipato cha uhakika ambacho kitakuwezesha kulipa watumishi mishahara mizuri zaidi, kujenga shule nyingi zaidi zenye ubora, hospitali zenye ubora zaidi, kutoa ruzuku kwa wakulima na orodha inaendelea.

Hongera Rais Magufuli kwa kufanya uwekezaji janja, hongera CCM, hongera Tanzania. Msioelewa sasa muelewe Rais anaposema tuko kwenye right track anamaanisha Nini.

Unaweza kuona nimetaja punje tuu ya mambo yaliyofanyika yenye lengo la kutufikisha mbali kiuchumi.

Fuatilia
Ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere
Ujenzi wa barabara
Uwekezaji kwenye madini
Ununuzi wa meli na vivuko

#2020 kura yangu kwa John
 
hazina umuhimu wowote kwangu
Wewe shida yako ni moja, hutaki kuelewa siku ukitaka kuelewa utaelewa. Ujumbe huu ni mahususi kabisa kwa mtu Kama wewe. The bottom line ni kuwa Kama unaishi Tanzania haijalishi umetaka au haujataka, inakusaidia
 
Hizi ndege hazina msaada hata kwa mtu anayeishi Dar. Mkuu fly over zinasaidia kuokoa muda wa kukaa barabarani, Ila ili uone unapoteza muda ni lazima kwanza uwe na kitu Cha kufanya, katika Tz ya Magu ambayo ukosefu wa ajira upo 200% na ugumu wa kufanya biashara kuwa 300% flyover is nothing maana watu wengi hawana shughuli za kuwaingizia kipato hivyo muda kwao is not an issue
 
Yaaani Vinachekeshaga sanaaa...

Sasa Mtu Anapoitumia Huduma Ya Serikali Mfano Barabara,Flyovers,Shule,Zahanati,Viwanja vya michezo....

Kote huko inakuwa Ni KODI YAKE TU iliyotumika KUYAWEKA HAYO?!!!

Jamii Nikutegemeana Maana Ninavyopenda KULA UBWABWA wa Kutoka Mbeya Haina Maana nimekula PESA YANGU....yaani ile NOTI NYEKUNDU ya buku 10 iweze kuyeyushwa na kunyonywa na PARIETAL cells za UTUMBO WANGU MDOGO?!!!
 
Lazima ubalance maendeleo ya vitu na watu!Watumishi wamepigwa pini,ajira hakuna kwa wahitimu,mzunguko wa fedha umeshuka!Taarifa za mabank zinaonesha kuwa uwezo wa wajasiriamali kukopa na kurejesha mkopo umepungua kutokana na mzunguko kuwa mdogo!

Kikwete angefanya kama JPM hali ya watumishi ingekuwa mbaya sana lakini pia mzigo wa graduates wasio na ajira ingekuwa balaa wakati JPM anapokea nchi!

Huyu JPM yeye na miundombinu tu huku hali za watu zikizidi kuwa mbaya!
 
Hizi ndege hazina msaada hata kwa mtu anayeishi Dar.Mkuu fly over zinasaidia kuokoa muda wa kukaa barabarani,Ila ili uone unapoteza muda ni lazima kwanza uwe na kitu Cha kufanya,katika Tz ya Magu ambayo ukosefu wa ajira upo 200% na ugumu wa kufanya biashara kuwa 300% flyover is nothing maana watu wengi hawana shughuli za kuwaingizia kipato
Mkuu Sijijui ni kuwa huna hoja ila una vioja. Najua unajua ila tuu basi ni kusudi umeamua kupinga ni Kama vile viongozi wenu wanavyopinga kila kitu
 
Orodha ya alivyovifanya ni kubwa Sana. Kwa uchache wa yaliyofanyika rejea
post yangu

Kumrudisha Rais Magufuli sio kupoteza kura bali ni kuitendea haki
Kwa hiyo hayo mengi aliyofanya ndo yamepelekea kuongeza only USD 100 kwenye GNI na kuvuruga kabisa market systems za mazao ya korosho,kahawa,mbaazi na tumbaku huku ukuaji wa uchumi ukiongezeka kutoka 7% hadi 4% si ndiyo mkuu?
 
Mkuu Sijijui ni kuwa huna hoja ila una vioja. Najua unajua ila tuu basi ni kusudi umeamua kupinga ni Kama vile viongozi wenu wanavyopinga kila kitu
Mkuu kwa hiyo wewe hapo ndo umetoa hoja? I thought unakuja na hoja ya namna flyover inavyomsaidia mtu asiye na kazi ya kumuingizia kipato kuingiza pesa
 
Lazima ubalance maendeleo ya vitu na watu!Watumishi wamepigwa pini,ajira hakuna kwa wahitimu,mzunguko wa fedha umeshuka!Taarifa za mabank zinaonesha kuwa uwezo wa wajasiriamali kukopa na kurejesha mkopo umepungua kutokana na mzunguko kuwa mdogo!
Kikwete angefanya kama JPM hali ya watumishi ingekuwa mbaya sana lakini pia mzigo wa graduates wasio na ajira ingekuwa balaa wakati JPM anapokea nchi!
Huyu JPM yeye na miundombinu tu huku hali za watu zikizidi kuwa mbaya!
Na hii ndo imeua biashara nyingi, purchasing power ya watu imepungua hivyo kupunguza kasi ya mzunguko wa pesa huku Kodi zikiwa za kukomoana.Ila malengo yake ya kuwafanya watu waishi Kama mashetani yametimia
 
Hivi kwa akili tu ya kawaida huu uchumi wetu wa kuvuta na kamba Mtu anasifia kununuliwa ndege kwa cash??..

By the way maendeleo ni hatua kwa hatua hata ww ipo siku ubongo wako utaendelea na utausoma huu Uzi wako tena, ninaamini utajidharau sana na utajiona mjinga kwa kutetea mambo unayodhania kuwa unayajua kumbe hujui.
 
Bavicha wako kundi la pili. Wanajua umuhimu wa hivyo vyote ila wanaamua kubeza na kudhihaki. Huenda wako sahihi kwa maslahi yao ya kisiasa ila wanapoharibu ni kutaka kumuaminisha kila mtu awe na mtazamo sawa na wa kwao.
 
Lazima ubalance maendeleo ya vitu na watu!Watumishi wamepigwa pini,ajira hakuna kwa wahitimu,mzunguko wa fedha umeshuka!Taarifa za mabank zinaonesha kuwa uwezo wa wajasiriamali kukopa na kurejesha mkopo umepungua kutokana na mzunguko kuwa mdogo
Mafanikio makubwa yanagharama zake. Mwaka huu mshahara umeongezwa. Kuhusu ajira ni lazima ujue haiwezekani kila mtu akaajiriqa na serikali. Serikali inatengeneza mazingira mazuri kupitia PPP na huko ajira rasmi na zisizo rasmi hutokea.

Ajira za walimu zimetangazwa. Najua bado eneo hilo lina changamoto ila tutafika pazuri zaidi
 
Back
Top Bottom