Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,405
KILE KITU CHA USIKU.
1) Mchana kinalegea, nguvu usiku chapata,
Kama vile chabembea, ajabu kukikamata,
Taratibu chasogea, mwendo wa pole wa bata,
Kile kitu cha usiku, hata mchana si kipo?
2) Tena kipo katikati, umbole kama duara,
Ni kama nusu chapati, kinapotoa taswira,
Hakilengwi kwa manati, usilete masikhara,

3) Kama ndani kina kitu, lakini kimejificha,
Wanakitumia watu, usiku usipokucha,
Na hakina ukurutu, hapo utani naacha,

4) Msitu wakizingira, pori linawaka waka,
Waliopoteza dira, njia walipoanguka,
Kilikuwa barabara, yasafari kufikika,

Mtunzi: Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
Simu: +255624010160
Email: iddyallyninga@gmail.com