Shairi; Kama mnataka mali mtaipata Shambani

Shairi; Kama mnataka mali mtaipata Shambani

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.


2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.


3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?


4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?


6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli...


" Kama mnataka Mali mtaipata Shambani".
 
Asante sana kwa hili shairi,binafsi umenirudisha nyuma na kukumbuka enzi hizo shule ya msingi,damn those were the good times...!!!
 
Hivi mashairi haya bado yanafundishwa mashuleni? Nakumbuka hadithi ya sungura sizitaki mbichi hizi,
 
Hivi mashairi haya bado yanafundishwa mashuleni? Nakumbuka hadithi ya sungura sizitaki mbichi hizi,

Asante sana kwa hili shairi,binafsi umenirudisha nyuma na kukumbuka enzi hizo shule ya msingi,damn those were the good times...!!!

Tuko pamoja waungwana, naamini wanafundisha ila sio kama kipindi chetu jinsi tulivyokuwa tunajifunz ahaya mambo....mnamkumbuka Manenge na Mandawa?
 
ila kwa sasa option za kupata mali ni nyingi iliyo ya fasta ni kuwa mwanasiasa
 
Hili shairi linahitaji remix maana mali hazipatikani tena shambani.

"Kama mnataka mali,mtaipata siasani /bungeni"
 
Inasemekana huyo baba anayezungumziwa humo ni msomi wa elimu ya juu aidha degree, masters au PhD na safari ya mbali inamaanisha safari ya kielimu takriban zaid ya maiaka 17 yupo darasan akiamin ipo siku elimu anayoitafuta itampa afuen ya kile anachokitaka lakin mwisho wa siku anaambulia patupu na kurudi hali yake ya zaman na hana kitu wakat alikuwa anaman kuwa na mali, na watoto humaanisha kuwa ndio sisi vijana ambao bado tupo chini na hatujawa na uzoefu wa kimaisha yalivyo huko mtaani, tumekaririshwa na wazaz wetu na jamii nzima kwa ujumla hasa wale ambao hawakusoma kuwa elimu ndio kila kitu ktk kufanikiwa maisha lakin aliyesoma anatuambia kuwa kama tunasoma kwa lengo la kuajiriwa ili kujiokoa kimaisha basi tunajidanganya tu isipokuwa mali inatokana na juhudi binafsi zaid huku ukishirikiana na watu. Shamba limekusudiwa mambo mawili tu, moja ni biashara ya jumlajumla na pili ni kipaji, hivyo kwa yule anayetaka mali basi hatoipata kamwe isipokuwa awe na kipaj au awe mfanya biashara wa jumlajumla au vyote kwa pamoja, mshair kazungumzia pia pori nene akiwa na maana changamoto za kuipata mali mitaani ni kubwa mno kuliko zile za shulen ambazo wakat mwingne unasoma msosi unakuta tayar umeshapikiwa na kuandaliwa lakin mtaaninni pagumu zaid kuliko huko shulen coz huli mpaka uwe umepata kitu vinginevyo unashinda na njaa tu. Hali aliyo nayo mgonjwa ni hali ngumu kimaisha na sio ugonjwa na ndo maana akasema hata kama akivhanjwa haiyoki homa kali, akiwa na maana kuwa hata kama ataajiriwa leo kamwe umasikin alio nao hautaisha isipokuwa atakufa maskin tu. Ili na sisi tuondokane na hiyo hali ndio mana akatupa kauli, yan ushauri kuwa mali haipatikana isipokuwa kwa kufanya kazi kwelikweli na kwa ushirikiano sio kama mashulen mitihan inatufundisha ubinafsi na anayepata maswali mengi zaid ndiyo anaonekana ana akili nying sana kuliko wengine wakat mtaani anayepata mafanikio ndiyo mtu wa juu kiheshima.
Naaam mkuu nakubali
 
Tuko pamoja waungwana, naamini wanafundisha ila sio kama kipindi chetu jinsi tulivyokuwa tunajifunz ahaya mambo....mnamkumbuka Manenge na Mandawa?
Dah mtoa mada kumbe alifariki? Asante sana kwa huu wimbo. Pumzika mahala pema kamanda.
 
Back
Top Bottom