kinyangesi
JF-Expert Member
- Jul 15, 2012
- 247
- 86
Nalieleza hili kwa ushairi, nashindwa kulala ndani, kushinda pia ni kazi, anijeruhi moyoni, nimuonapo siwezi, namtamani yakini, awe kwangu mpaka mbali, anachonishinda huyu, ni dada wangu wa kazi. Anavyojua kupika, chakula chake kitamu, mkate wake kupaka, tena autia jamu, mke wangu hajafika, kiwango chake timamu, anachonishinda huyu, ni dada wangu wa kazi.
Azifanya zote kazi, mke wangu amelala, ni wa watoto mlezi, mkengu angoja kula, ninabaki bumbuazi, akikileta chakula, namuona anifaa, kuliko wangu mwandani. Ana kitu kafungasha, nyuma anaponipita, moyo autetemesha, nashindwa kufukuta, analo jema bashasha, mke hawezi mkuta, tatizo ni moja tu, ni mdada wangu wa kazi.
Atandika na kitanda, kitanda changu chumbani, jicho langu likiganda, pale kwake maungoni, hapo nabaki nadunda, moyo wangu tafrani, tatizo lake moja tu, ni daada wangu wa kazi. Umbo lake lavutia, kuliko la mke wangu, jinsi anavyonukia, mke wangu pale pungu, jinsi anavyotembea, napata kizunguzungu, Tatizo ni moja tu, Ni Dada wangu wa kazi.
Napenda kutoka nae, kulito mama watoto, ninapenda niwe nae, hata nkenda maliwato, hapo ninachoka mie, kwa umbo lake mtoto, sasa mke ni wa nini, wakati kazi hafanyi? Kazi yake ya chumbani, na tena sio mmanyi, akifanya anihini, anihini nammanyi, sasa mke wa nini, wakati kazi hafanyi?
Nguo zote anafua, pasi ananipigia, tai ananifungia, mkoba aniandalia, chai aniandalia, kikombe anikorogea, sasa mke wa nini, wakat kaz hafanyi? Anazo busara njema, mke wangu yupo nyuma, ana maamkizi mema, akiniona huchutama, kwa uzuri yu salama, mashallah yuko vyema, kama bado urijali, lazima utetemeke.
Sasa nataka muoa, nimuoe awe ndani, mke nataka timua, hanayo kazi nyumbani, kwani kashindwa kujua, nikitakacho mwandani, beki tatu ataweza, yoote nitakayo. Ushauri niambieni, huyu kama atafaa kuwekwa ndani, au atakuja jutia, niingie harusini, au nibaki tulia?
Naomba ushauri wenu wandugu
NAMPENDA HOUSE GIRL