Fikra Angavu
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 301
- 105
Nina uhakika nina gundu,
Haifichiki kama nundu,
Wazi wazi bila ukungu,
Hii ya leo ni kali, nimechoka paka basi.
Nilikua daladalani,
Mtoto mzuri pembeni,
Anasimu kiganjani,
Hii ya leo ni kali, nimechoka paka basi.
Nikamuuliza,
Dada habari yako,
Za huko utokako,
Umependeza naomba namba yako,
Nasema,
Hii ya leo ni kali, nimechoka paka basi.
Dada alitabasamu,
Chombezo lilimmaliza hamu,
Sauti masikioni ilihatamu,
"Sawa hamna shida, na wewe ni hendisamu"
Hii ya leo ni kali, nimechoka paka basi.
Jamani nawachukia mateja,
Narudia ninaugomvi na mateja,
Walichonifanyia ni zaidi ya jecha,
Hii ya leo ni kali, nimechoka paka basi.
Mrembo kwa mapozi kama jini,
Kalegeza mkono tena dirishani,
Kumbe teja yu mawindoni,
Jamani,
Hii ya leo ni kali, nimechoka paka basi.
Kesha chukua namba,
Na nimeshajivua gamba,
Sitaki tena misamba,
Teja kapita kama mamba,
Hii ya leo ni kali, nimechoka paka basi.
Teja kakwapua simu jamani,
Teja kaitia simu kwapani,
Machozi kulia natamani,
Najikaza mrembo asinione hayawani,
Na sina kitu mfukoni,
Aaah.
Hii ya leo ni kali, nimechoka hadi basi.
Jamani pole,
Kaka hujaumia vidole?
Dada aniulizia wangu udole,
Simuelewi na zake pole,
Nikashuka pale pale,
Kachukuaje yangu kaacha ya yule?
Hii ya Leo ni Kali, Nimechoka hadi basi.