Shairi: Afya ya uchumi

Shairi: Afya ya uchumi

Makungu Joshua

New Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Habari yenu jamii, mko salama jamani,
inaniuma namimi, twapotea hasirani,
twakosa tiba kwanini, nchi ni yako namimi,
leo nahitaji nipate, afya ya uchumi.

watu wanahangaika, ajira zionekani,
serikali kutoweka, fursa kazi hadharani,
watu kazi wanataka, huishia wizi mtaani,
kwanini ajira hazipo, na taifa ni tajiri.

Mikoani Tanzania, watu wengi uhugua,
matibabu yapungua, ata kwa sio jiweza,
uwe na pesa hakika, ndio tibiwa waweza,
na masikini jamani, wanahitaji uhai.

uchumi wazidi panda, watu wote lalamika,
sio kwamba twapenda, au ni kwamba twataka,
mashamba yetu twapanda, pesa ndogo tunapata,
uchumi mgumu jamani, utaisha lini hakika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom