kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 735
___________________
Habari za kifo cha muigizaji Shahrukh Khan zilienea kwa kasi mapema wiki hii na kusababisha wasiwasi miongoni mwa mashabiki wake duniani kote.
Hata hivyo taarifa hiyo imethibitishwa kuwa ni uongo na hivi karibuni habari nyingi za bandia kwenye mitandao ya kijamii zimekuwa zikizusha taarifa za kifo cha msanii huyo.
Alhamisi (Mei 18) ripoti iliyotoka jana ilithibitisha mwigizaji huyo hajafa yu hai.Mwigizaji huyo ameingia kwenye orodha ya watu mashuhuri wanao zushiwa vifo kwenye mitandao ya kijamii.
Baadhi ya mashabiki wake wamesikitishwa na taarifa hiyo ya uongo na huku wengine wakisema hii inaonyesha umaarufu wake uliokithiri duniani kote.
------------------
Je ni move gani ya star huyu wa Kuch Kuch Hota Hai uliyotokea kuipenda zaidi au unamjuaje huyu star katika industry ya filamu india na ulimwenguni kote...