Shahada za vyuo vya Kitanzania hatarini kupuuzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shahada za vyuo vya Kitanzania hatarini kupuuzwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Sideeq, Jun 22, 2012.

 1. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Baada ya lile sakata la NECTA ambalo limenyakwa hata na vyombo vya habari vya nje, mabadiliko na uboreshwaji wa Baraza ambayo yamechukuliwa na Serikali hayatangazwi sana na vyombo vya habari! hii inaviweka katika hatari vyuo vya Tanzania kuonekana katika uoni wa macho ya nchi za nje kuwa untrustworthy! vyombo vya habari tafadhalini tangazeni mabadiliko na uboreshwaji wowote ule uliotokea NECTA baada ya lile sakata ili isije ikawakuta Watanzania yale yanayowakuta wasomi waliosomea Russia ambapo vyeti vyao havithaminiwi kabisa katika nchi za Magharibi.
  Mod please usiubanie huu uzi kwa sababu ni ushauri tu kwa vyombo vya habari ambao ninaamini utasaidia sana wasomi wa Kitanzania.
  Not coded message trust me!
  Nawasilisha.
   
 2. B

  Bob G JF Bronze Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kama ukiamua kutotaka kuelewa ni tatizo lako. waalimu wa kiislamu waliitwa NECTA wakaeleweshwa na wakaelewa na wakaamini ilikua bahati mbaya na haikua makusudi, issue waambieni hao walimu wakiislamu wawaeleweshe waumini wenzao ambao wanatumia NECTA kwa malengo yao wakati mambo yalishawekwa sawa na NECTA
   
 3. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa skendo kama ile, aidha "bahati mbaya" au si bahati mbaya mabadiliko, uboreshwaji na uwajibikaji ni lazima Mkuu!
   
 4. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kulingana na 'tatizo' wewe unashauri mabadiliko yapi yafanyike, na uboreshwaji upi ili utusadie sisi wafanya maamuzi ili tuweze kufanya maamuzi magumu
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  duh, NECTA wanatoa degree!!! thread yako ni upup.u mtupu
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Narubongo,
  Umeweka picha ya Lameck Airo mbunge wa Rorya, hivyo mimi nilitegemea kwamba wewe ni yeye au jamaa zake wa karibu au iliyokuwa timu yake ya kampeni. Lkn kila ninaposoma mchango wako hapa JF naona kabisa uwezo wako wa kung'amua mambo ni mkubwa kuliko Lameck Airo ambaye yuko likizo ya miaka 5 bungeni akifanikisha mambo yake ya kibiashara.

  Sasa mimi nina swali moja tu kwako, je ni kitu gani kinahokuvutia kwa Lameck Airo mpaka umeamua kutumia picha yake? tafadhali naomba unijibu.
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mkuu, jukwaa langu kuu JF ni "Business & Economic Forum & Ujasiriamali" ukienda huko utakuta michango yangu mingi sana (karibu sana) na utaweza kunielewa vizuri.

  - Kanda ya ziwa inajulikana kwa kuwa na wasomi wengi kama master, PhD holders & PROFs

  - Kanda ya ziwa inajulikana kwa kutengwa na govt, angalia jiji la mwanza ambalo 97+% limejengwa na watz

  - Angalia ktk hizo 97+% master, PhD holders & PROFs wanamiliki % ngapi (Nipe jina la msomi mmoja mwenye investment kubwa pale mwanza)

  - Wenye primary/secondary education ndio wanamiliki sekta ya usafiri, uvuvi, mijengo yote ya pale mjini pamoja na viwanda na mahoteli makubwa etc (kina diallo, kitana, charles, gachuma, ... kishimba na wengine kibao...) na hawa wasiosoma ndio wamewajiri maengineers & other graduates kwenye viwanda vyao na biashara nyingine

  - sasa mkuu, ukiangalia hayo makundi je? ni kundi lipi ambalo linafaa kuigwa na kuwa mfano bora wa kunitimizia malengo yangu ya kuwa mmoja wa wawekezaji wakubwa wazawa na kuja kutoa ajira badala ya mimi mwenyewe kutegemea kuajiriwa?

  ...fuata nyukiule asali
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana ndugu yangu. Na mimi ni wa huko huko. Naamini tutaongea mengi ndugu yangu na hakika nititembelea hiyo forum ya business, kwani ndilo enero langu pia japo katika angle nyingine ya training na research. Ahsante sana kwa hiyo taarifa.
  TELO.
   
Loading...