Hazina faida yoyote ile kwa nchi, zaidi ya kuwa sifa ya mtu binafsi. Mchango wa mtu fulani katika jamii, na pia utambulike mbele ya taasisi fulani yenye hadhi na kuaminika, huwa ni kitu cha faraja kubwa kwa muhusika.
Ila yule anayezipata kwa njia ya mchongo huwa anajidanganya yeye mwenyewe, ingawaje zina faida kubwa sana ndani ya CCM. Mtu akiipata tu huesabika kuwa naye yumo kwende kundi teule la "elites" wachache ndani chama.
Madaktari wa aina hii hupata ujiko mkubwa katika kutambulishwa kwenye hafla maalum iliyoandaliwa na CCM, na pia ni rahisi kwao kupata "connection" za maana kupitia maisha yao ya ki-"fake".