Shaffih Dauda angalia utachanika msamba, Msafiri Mgoyi na Almas Kassongo hawakutakii mema hao!

kapellen

New Member
Mar 19, 2017
4
2
Baada ya tuhuma za rushwa kule Mwanza, ukatangaza kwenye media kama umeamua kujitoa kwenye mchakato wa uchaguzi wa TFF lakini baada ya wapambe wako Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kassongo na Mwenyekiti wa Kigoma Msafiri Mgoyi kukwambia usiandike barua ya kujitoa, ukaamua kukaa kimya na kusubiri taarifa ya Takukuru mkiamini utakuwa salama na kuendelea na kampeni zako kimya kimya na sasa Takukuru wameshusha rungu kama wewe na wenzio mnaogombea ujumbe wa kamati ya utendaji akina Lugora, Mwanjala na Majige hamfai kugombea.
Msafiri Mgoyi na Almasi Kassongo wamebeba dhamana ya kuandika rufaa ya wewe urudishwe kwenye mchakato wa uchaguzi kwa mantiki ipi? Mgoyi anataka akutumie kwa manufaa yake lakini uchunguzi wa Takukuru umeshakwisha? Hao wanakulia pesa zako unazopata kwenye Ndondo Cup na mwisho wakumwage! Endelea na rufaa yako lakini ujue huko mbele utalia na kusaga meno utakapopelekwa kwenye kamati ya maadili na kwa taarifa mtizame mwenzio Hassan Hassanoo
 
Huyu Dauda huwa anajifanya kuponda wenzake wee huku na yeye anamendea kupata nafasi ya ulaji, unafiki mtupu
 
Shaffih...kama hukujihusisha na rushwa uchune tu...! Lakini kama ulidhubutu kuingia huko kwenye mkumbo...imekula kwako.
 
Kwa jinsi ulivyoamdika inaonyesha na wewe unagombea au kuna mgombea unampigia upatu.
 
Shafii kujifanya much know wa kila kitu

Sasa kwenda mbele kwenye TV kutangaza kajiondoa kumbe fix

Mnamsababishia ally mayai apigiwe kura za hasira kwasababu ya magundu yenu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Ningekuwa Ruge huyu jamaa kwanza ningemtoa kwenye vipindi vya michezo. Wangempa uhuru afanye mambo yake Binafsi maana kwa doa hili alilojitia bila shaka itakuwa dhahir CMG wapo nyuma yake na wangemsupport kwa hali yoyote wahakikishe anashinda..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakukua na haja ya kuja na ID Mpya...wanaume tunaambiana ukweli..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom