Shabani Hamisi, Mume wa Zamaradi Mketema aliyemtishia mwenzake kwa bastola afikishwa Mahakamani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Shabani Hamisi ambaye ni mume wa mtangazaji na mmiliki wa Zamarad TV, Zamaradi Mketema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na mashtaka ya kumtishia Venance John kwa bastola.

=====

Aliyemtishia mwenzake na bastola aachiwa
43280836_2041779779210067_3689578870601367914_n1.jpg

JUMATATU , 4TH NOV , 2019
NA MWANDISHI WETU
Mwanaume aliyeonekana akimtishia mwenzake kumpasua na bastola, leo Novemba 4, 2019, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na kuachiwa kwa dhamana ya Shilingi Milioni 2 kutoka ka wadhamini wawili.


Mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Shaban Hamis, ambaye pia ni Mume wa mtangazaji Zamaradi Mketema, alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na kosa la kumtishia silaha, Dereva wa lori la mchanga Venance John.

Akisomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga, mbele ya Hakimu Mfawidhi, Frank Moshi, mtuhumiwa alikana shtaka hilo na inaelezwa kuwa mtuhumiwa inadaiwa kwa makusudi kabisa alimtishia Venance John, huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 30, 2019, maeneo ya Mbezi Mabwepande na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 13, 2019.
 
Mwenetu huyu Tumsamehe/
Awekwe ndani kwa siku 30 nadhani akitoka atakuwa na Ilmu mzuri kabisa.
 
Ndo mana mi ctaki kumiliki mguu wa kuku maana mie sijuagi mikwara mikwara eti nikutishie tishie mi nakutandika kweli ya ubongo then tunagawana majengo ya serikali we unaenda segerea mm mochwari!
Kabisa Mkuu, jamaa alipochukuwa pistol nilijua anamuwasha kweli. Unfortunately kumbe ana vi-element vya woga still . . .
 
Ndo mana mi ctaki kumiliki mguu wa kuku maana mie sijuagi mikwara mikwara eti nikutishie tishie mi nakutandika kweli ya ubongo then tunagawana majengo ya serikali we unaenda segerea mm mochwari!
Unamtandika anaenda Segerea wewe Mochwari au unajiua mwenyewe???😂😂😂😂

Au unampa akuue aende segerea wewe uende mochwari😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom