Anayedaiwa kumng'oa mkewe jino kwa plaizi na kumtoboa jicho afikishwa Mahakamani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
kizimbani-pic.jpg

Isack Robertson (45) mkazi wa Sombetini jijini Arusha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha akikabiliwa na kosa moja la shambulio la kudhuru mwili.

Mshitakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Mei 31, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Jenipher Edward.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 80/2023 Wakili wa Jamhuri Charles Kagirwa alimsomea mshitakiwa huyo kosa moja la shambulio la kudhuru mwili.

Alidai Mei 23 mwaka huu saa tano usiku, Osunyai alimjeruhi mkewe Jackline Mkonyi (38) kwa kumng'oa jino, kumpiga na mkanda usoni, mgongoni na maeneo mengine ya mwili na kumsababishia madhara ikiwemo kushonwa nyuzi nane chini ya jicho.

Baada ya kumsomea kosa hilo, mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa jamhuri ulieleza kuwa upelelezi umekamilika na kumsomea maelezo ya awali.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Mei 23, 2023 mwathirika alikuwa nyumbani na watoto wake na alisikia honi ya gari nje ya geti ambapo alikuwa anajiandaa kwenda kufungua, alikuta mtoto wao mkubwa ameshaenda kufungua.

Alidai kuwa mshitakiwa alipoingia ndani hakutoa salamu kwa mke wake na badala yake alielekea chumbani na mwathirika aliamua kumfuata chumbani. Mtuhumiwa alimvuta hadi sebuleni na kuanza kumpiga mateke, kumpiga kwa mkanda wake wa suruali maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumng'oa jino kwa kutumia plaizi jambo lililomfanya mwathirika atokwe na damu nyingi.

Ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo alimpigia mama mkwe wake na kumueleza kua ajiandae kupokea mzoga wake. Alimpeleka mkewe nyumbani kwao na kumtelekeza nje ya geti na yeye kutokomoea kusikojulikana hadi alipokamatwa Mei 27, eneo la Himo, Kilimanjaro.

Baada ya kusoma maelezo hayo, Jamhuri ilisema itakuwa na mashahidi watano na kielelezo kimoja katika kesi hiyo ambayo mtuhumiwa huyo anajitetea mwenyewe.

Aidha Jamhuri wamewasilisha maombi madogo ya kuomba mshtakiwa huyo asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake na usalama wa mwathirika.

Kufuatia maombi hayo hakimu huyo ameahirisha kesi hiyo kwa muda hadi saa tisa alasiri kwa ajili ya kutolea uamuzi mdogo.

Chanzo: Mwananchi
 
Familia nyingi zinasambaratika kutokana na michepuko,ndugu wa ukoo,jamaa na marafiki kuendekeza vitendo vya ushirikina na uchawi.
Yawezekana huyu jamaa alitupiwa pepo, akatenda yaliyonuiwa na waovu na sasa kamiumiza mwenzi wake.
Mungu atusimamie sana,kwenye jamii na familia wivu wa maisha umetawala sana
 
View attachment 2641529
Isack Robertson (45) mkazi wa Sombetini jijini Arusha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha akikabiliwa na kosa moja la shambulio la kudhuru mwili.

Mshitakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Mei 31, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Jenipher Edward.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 80/2023 Wakili wa Jamhuri Charles Kagirwa alimsomea mshitakiwa huyo kosa moja la shambulio la kudhuru mwili.

Alidai Mei 23 mwaka huu saa tano usiku, Osunyai alimjeruhi mkewe Jackline Mkonyi (38) kwa kumng'oa jino, kumpiga na mkanda usoni, mgongoni na maeneo mengine ya mwili na kumsababishia madhara ikiwemo kushonwa nyuzi nane chini ya jicho.

Baada ya kumsomea kosa hilo, mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa jamhuri ulieleza kuwa upelelezi umekamilika na kumsomea maelezo ya awali.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Mei 23, 2023 mwathirika alikuwa nyumbani na watoto wake na alisikia honi ya gari nje ya geti ambapo alikuwa anajiandaa kwenda kufungua, alikuta mtoto wao mkubwa ameshaenda kufungua.

Alidai kuwa mshitakiwa alipoingia ndani hakutoa salamu kwa mke wake na badala yake alielekea chumbani na mwathirika aliamua kumfuata chumbani. Mtuhumiwa alimvuta hadi sebuleni na kuanza kumpiga mateke, kumpiga kwa mkanda wake wa suruali maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumng'oa jino kwa kutumia plaizi jambo lililomfanya mwathirika atokwe na damu nyingi.

Ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo alimpigia mama mkwe wake na kumueleza kua ajiandae kupokea mzoga wake. Alimpeleka mkewe nyumbani kwao na kumtelekeza nje ya geti na yeye kutokomoea kusikojulikana hadi alipokamatwa Mei 27, eneo la Himo, Kilimanjaro.

Baada ya kusoma maelezo hayo, Jamhuri ilisema itakuwa na mashahidi watano na kielelezo kimoja katika kesi hiyo ambayo mtuhumiwa huyo anajitetea mwenyewe.

Aidha Jamhuri wamewasilisha maombi madogo ya kuomba mshtakiwa huyo asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake na usalama wa mwathirika.

Kufuatia maombi hayo hakimu huyo ameahirisha kesi hiyo kwa muda hadi saa tisa alasiri kwa ajili ya kutolea uamuzi mdogo.

Chanzo: Mwananchi
So sad , anaenda kufungwa na fidia atamlipa huyo mke wake
 
Jamaa ni memba wa JF Arusha Wing! Niliwai intaract nae few yrs ago! Wana JF walioendaga Arusha trip wanaweza mkumbuka tulienda nae Tarangile,
 
Back
Top Bottom