Sh4.2bn earthquake relief cash ‘lying idle’

Sh4.2bn earthquake relief cash ‘lying idle’

Mkuu BAK vipi materials hesabu yake imewekwa pande zipi.......hadi sasa wanahamasisha watu kutoa michango/misaada lakini hakuna kinachoendelea wangeaanza basi na wazee wanaowatangaza kila mara.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi serikali kama serikali (Kupitia Kamati ya Maafa-Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo hutengewa pesa kila mwaka) imetoa shs ngapi? Naona kama serikali yenyewe ina-organize tu kupokea na kutoa misaada lakini haijachangia hata senti. Hii ni kama mweka hazina wa kamati ya harusi asichangie kwa vile yeye anakusanya, kutunza na kuidhinisha il-hali ni mwanakamati. Katika kuhudumia wananchi wake (welfare), hii awamu naipa 45%. Madawati, mostly tumejichangisha.
 
Huu ni uongo wa hali ya juu. Uingereza pekee yake imetoa shilingi 6.7 billion kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi iweje Serikali iseme zimekusanywa bilioni 5 tu!? List ya wachangiaji wote na kiasi walichochanga iwekwe hadharani mara moja ili kama kuna wizi umefanywa katika pesa hizi basi hao wezi wanaanikwe hadharani kwa kuiba pesa za wahanga wa tetemeko.
Hili la tetemeko linatatiza sana

Kwanza, tetemeko limeathiri watu na mali zao. Kwa hesabu zao zilihitajika Bilioni kadhaa kurudisha hali
Kwa minajili ya mjadala tuseme ni Bilioni 20. Hivi kweli serikali inayokusanya 1.2T imeshindwa kutoa bilioni 20 hadi tuite mabalozi kwa misaada?

Mh Makamba alitueleza, katika kero za muungano JMT ilitoa bilioni 29 kwa budget support ya Zanzibar
Serikali hiyo hiyo imeshindwa kutenga kiasi cha bilioni 20 kwa Walipa kodi wa Kagera!

Pili, tulisikia Kenya na Uganda wamechangia yakiwemo mataifa mengine na watu binafsi
Leo namba zinapishana, mara bilioni hizi mara zile
Ni wakati sasa kila kitu kiwekwe wazi wananchi wajue nini kilichangwa na kimeelekezwa wapi

Tatu, leo waziri mkuu bado anatembelea magofu ya shule. Ina maana hakuna kilichofanyika hadi wakati huu
Hivi hatuna wataalamu wanaoweza kuchora, na contractors wanaoweza kujenga shle katika muda mfupi?

Ile dhana ya hapa kazi ipo wapi?
 
Huu ni uongo wa hali ya juu. Uingereza pekee yake imetoa shilingi 6.7 billion kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi iweje Serikali iseme zimekusanywa bilioni 5 tu!? List ya wachangiaji wote na kiasi walichochanga iwekwe hadharani mara moja ili kama kuna wizi umefanywa katika pesa hizi basi hao wezi wanaanikwe hadharani kwa kuiba pesa za wahanga wa tetemeko.
Kuna tetesi kwamba zinatarajiwa kujenga nyumba za watumishi makao mapya Dodoma .
 
%25255BUNSET%25255D.jpg

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokea tarehe 10 Septemba 2016.

Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera.

Shilingi 1.4 bilioni zimekusanywa katika harambee iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili kusaidia wananchi waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera Jumamosi iliyopita.
Kiasi hicho ni fedha taslimu na ahadi zimetolewa na wafanyabiashara na mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini.

Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:-

= TBL Wamechangia Milioni 100

= Azania Group Wanatanguliza Milioni 20

= Wafanyabiashara wa Mafuta wa rejareja watakusanya Milioni 250 na watakabidhi ijumaa ya week hii

= Kagera Sugar wanatoa Milioni 100 na tani 10 za sukari.

= Serengeti wanatoa saruji mifuko 800

= Pepsi Cola 50 Millioni

= Hatiamaye Regnald Mengi anatoa mchango wake wa Milioni 110.

= Protas Ishengoma anatoa msaada wa Milioni 5.

= GBP, MOIL na OILCOM wameahidi kujenga shule mbili (Ihungo na Nyakato) zilizoharibiwa vibaya.

= Puma wanachangia 50 Milioni

= Agusta Tanzania wanatoa Milioni 10

= Camel Oil wanachangia mifuko 1,000 ya Cement

= Tippa waachangia milioni 20

= Orexy wanachangia Milioni 50

= Waislamu wa madhehebu ya Al-Shafy, Ijumaa na Adhuhuri wanachangia Milioni 1.

= Sahara Tanzania wanachangia Milioni 20

Wizara ya Mambo ya Nje watafanya matembezi ili kuhamashisha uchangishaji wa fedha na wataanzia Polisi Oysterbay.

MAJUMUISHO:

Waziri Charles Mwijage nafanya majumuisho ya fedha zilizopatikana ni kama ifuatavyo:

1. Fedha taslimu ni Milioni 646,

2. Ahadi ni Milioni 705,

3. Dola za Kimarekani 10,000

4. Yuro 10,000.

5. Mfuko ya Sementi zaidi ya 2800,

6. Ahadi ya ujenzi wa Shule mbili ndani ya siku 30.

JUMLA KUU, Bilioni 1 na Na Zaidi ya Milioni 300
======
 
Mkuu kapiga hela, hasa zile bil.6 za Uingereza ndo maana anaona hata aibu kwenda Kagera maana anajua kawaibia!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu Mr Rocky ahsante sana Mkuu. Hawa jamaa kwa kutotaka maovu yao yaanikwe hadharani wakaamua kulishusha hadhi neno "uchochezi" hivyo kila anayeanika uovu wao hadharani basi "huwachonganisha wananchi na Serikali" yao. Hata CAG naye ni mchochezi siku awamu hii maana kaanika hadharani ukwapuzi wa nyumba za Serikali, uongo Bungeni wa upotevu wa mabilioni ya pesa wizara ya ujenzi na pia ununuzi wa boti la MV ufisadi. Anavutiwa pumzi tu ili atimuliwe na nafasi yake apewe kikaragosi mwingine ambaye hataweza kuanika uovu wowote ndani ya Serikali ili kulinda ajira yake. Tembo hawatufai Mkuu. Salam zangu nyingi kwa familia yote Mkuu.

Mkuu BAK huu ni uchochezi na kumbuka mkuu hajaribiwi
Walishaaambiwa wajitetemekee na wajenge nyumba zao wenyewe
Usimchokoze mkuu
 
Mkuu Mr Rocky ahsante sana Mkuu. Hawa jamaa kwa kutotaka maovu yao yaanikwe hadharani wakaamua kulishusha hadhi neno "uchochezi" hivyo kila anayeanika uovu wao hadharani basi "huwachonganisha wananchi na Serikali" yao. Hata CAG naye ni mchochezi siku awamu hii maana kaanika hadharani ukwapuzi wa nyumba za Serikali, uongo Bungeni wa upotevu wa mabilioni ya pesa wizara ya ujenzi na pia ununuzi wa boti la MV ufisadi. Anavutiwa pumzi tu ili atimuliwe na nafasi yake apewe kikaragosi mwingine ambaye hataweza kuanika uovu wowote ndani ya Serikali ili kulinda ajira yake. Tembo hawatufai Mkuu. Salam zangu nyingi kwa familia yote Mkuu.

Nashukuru sana mkuu Bak byzo I.T Tunaogopa sana kucomment kwenye maeneo kama haya maana hatuna mil 7 za kwenda kujilipia faini na ushaona kule bungeni wanalalamika hata hiyo faini wanasema ni ndogo hivyo kesi kama hiyo unaweza ukajikuta unadaiwa mil mia
Yuende hivyo hivyo mkuu tutafika na tutaona tunaelekea wapi
Asante kwa salam na wewe salam kwa familia
 
  • Thanks
Reactions: BAK
wanasubiri mkuu ndiye atoe maagizo namna gani ya kufanya, nchi nzima inasubiri kichwa cha mtu mmoja
ndiye aamue mambo yote, si mnakummbuka siku anamkabidhi pesa za michango pm alimwambia waziwazi
kuwa nakukabidhi ili nije nikudhibiti iwapo utazitumia vibaya.
 
Pesa iliyochangwa ni bilion 16 mpaka sasa......

Hizo zingine ni polojo tu............

Za watu wasimuogopa mungu.....
Kenya, uganda, uingereza, wafanya biashara, taasis na wananchi michango yao ni tsh4.7bln? Kuna walakin hapo
 
Shukrani sana Mkuu. Ndiyo hivyo Mkuu Bunge la MACCM kwa kutaka kuendelea kuficha uozo ndani ya Serikali yao ni lazima waone milioni 7 ni ndogo. Soon tutaingia mitini humu ili kuwapa furaha waitakayo ya kuimarisha udikteta uchwara wao.

Nashukuru sana mkuu Bak byzo I.T Tunaogopa sana kucomment kwenye maeneo kama haya maana hatuna mil 7 za kwenda kujilipia faini na ushaona kule bungeni wanalalamika hata hiyo faini wanasema ni ndogo hivyo kesi kama hiyo unaweza ukajikuta unadaiwa mil mia
Yuende hivyo hivyo mkuu tutafika na tutaona tunaelekea wapi
Asante kwa salam na wewe salam kwa familia
 
Museveni, Kagame,Kenyatta wasaidia tetemeko Kagera

%25255BUNSET%25255D.jpg

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokea tarehe 10 Septemba 2016.

Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera.

Shilingi 1.4 bilioni zimekusanywa katika harambee iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili kusaidia wananchi waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera Jumamosi iliyopita.
Kiasi hicho ni fedha taslimu na ahadi zimetolewa na wafanyabiashara na mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini.

Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:-

= TBL Wamechangia Milioni 100

= Azania Group Wanatanguliza Milioni 20

= Wafanyabiashara wa Mafuta wa rejareja watakusanya Milioni 250 na watakabidhi ijumaa ya week hii

= Kagera Sugar wanatoa Milioni 100 na tani 10 za sukari.

= Serengeti wanatoa saruji mifuko 800

= Pepsi Cola 50 Millioni

= Hatiamaye Regnald Mengi anatoa mchango wake wa Milioni 110.

= Protas Ishengoma anatoa msaada wa Milioni 5.

= GBP, MOIL na OILCOM wameahidi kujenga shule mbili (Ihungo na Nyakato) zilizoharibiwa vibaya.

= Puma wanachangia 50 Milioni

= Agusta Tanzania wanatoa Milioni 10

= Camel Oil wanachangia mifuko 1,000 ya Cement

= Tippa waachangia milioni 20

= Orexy wanachangia Milioni 50

= Waislamu wa madhehebu ya Al-Shafy, Ijumaa na Adhuhuri wanachangia Milioni 1.

= Sahara Tanzania wanachangia Milioni 20

Wizara ya Mambo ya Nje watafanya matembezi ili kuhamashisha uchangishaji wa fedha na wataanzia Polisi Oysterbay.

MAJUMUISHO:

Waziri Charles Mwijage nafanya majumuisho ya fedha zilizopatikana ni kama ifuatavyo:

1. Fedha taslimu ni Milioni 646,

2. Ahadi ni Milioni 705,

3. Dola za Kimarekani 10,000

4. Yuro 10,000.

5. Mfuko ya Sementi zaidi ya 2800,

6. Ahadi ya ujenzi wa Shule mbili ndani ya siku 30.

JUMLA KUU, Bilioni 1 na Na Zaidi ya Milioni 300
======
 
.Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ,Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupoka msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 kutoka Idara ya Maendeleo ya Nje ya nchini
Mkuu wa Idara ya DFID hapa nchini,Vel Gnanendran akizungumza na waandishi wa habari juu ya Serikali ya Uingereza kutoa msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 wenye lengo la kusaidia waathirika wa tetetmeko la ardhi hususan kwa shule zilizoathiriwa na tetemeko hilo,kulia ni Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ,Profesa Joyce Ndalichako.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Na: Frank Shija, MAELEZO.

MSAADA wa Shilingi bilioni 6.3 umetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyo haribika baada ya kuathiriwa na tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba mkoani Kagera.

Hayo yabainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuhusu huo.

Profesa Ndalichako amesema kuwa msaada huo umetokana na ziara aliyoifanya tarehe 17 na 18 mkoani Kagera ambapo mwakilishi kutoka DFID nchini alishiriki katika zaiara hiyo na kutembelea shule zilizo haribika kutoka na tetemeko hilo.

“Baada ya bunge kuisha tarehe 17 na 18 nilifanya ziara ya kutembelea shule zilizoharibika kutokana na tetemeko, kwa bahati wadau wetu wa maendeleo DFID waliungana name kutembelea shule za Ihungo na Rugambwa kutokana ziara ile wameamua kutusaidia” Alisema Ndalichako.

Kufuatia ziara hiyo ambapo walijionea uharibifu mkubwa wa majengo ya shule ya Ihungo na nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa, DFID waliguswa na athari walizozikuta na kuamua kusaidia ujenzi wa Shule ya Ihungo na nyumba 10 za walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa.

Amesema kuwa msaada huo umelenga kujenga upya shule ya Sekondari ya Ihungo ikiwa ni pamoja na kujenga maabara ya kisasa na kununua samani zilizoharibika. Mpaka sasa wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wapo mkoani Kagera mabapo leo wanakabidhiwa shule hizo na Manispaa ya Bukoba ili waanze ujenzi wake unaotarajiwa kukamilika mwezi Januari mwakani.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa nchini (DFID Tanzania) Vel Gnanendran amesema kuwa Serikali ya Uingereza imeguswa sana na athari zilizotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

“Kwa niaba ya Serikali ya Uingereza tunatoa pole sana kwa Mhe. Rais Magufu na waathirika wote wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kwa ni tukio lisilo pangwa”. Alisema Mkuu huyo. Vel amesema kuwa lengo kubwa la wao kutoa msaada huo ni kuhakikisha miundombinu ya shule zilizoharibika kujengwa haraka ili wanafunzi waweze kurejea mashuleni katika wakiwa katika hali ya kawaida.

“Tumeguswa sana na athari zilizotokana na tetemeko la Kagera, Serikali ya Uingereza kupitia ofisi ya DFID Tanzania imetoa msaada wa pound milioni 2.23 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 6.3 za Kitanzania”. Alisema Vel.

DFID ni idara iliyo chini ya Serikali ya Uingereza ambayo imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali ya maendeleo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
 
Michango yenyewe inapokolewa na kila mtu si ajabu mpaka leo hakuna majumuisho, wala mkakati unaoleweka wanasaidia vipi. Sana sana leo peleka unga wa sembe kesho mabati kwa utaratibu wa sandakalawe mwenye kupata apate mwenye kukosa akose muhimu picha tu waonekane wanafanya kitu.

Lakini si kwamba kuna proper assesments kujua individually watu wanasaidiwa vipi. Hivi tangia Nyerere kuna kiongozi gani mwingine kawai kufanya japo kitu kimoja tu successfully.
 
Dikteta kumbe ni tapeli na mpenda dhuruma.Pesa za waathirika kazichimbia ale mke wake.

Ndio maana ameshindwa hata kuwatembelea wahanva hadi leo! halafu anasubiri 2020 akawaombe kura hao hao aliowaibia! na kwa walivyo na akili mbovu za kitanzania basi watampa tu! huu ni ujinga wa kiwango cha juu kabisa!
 
Hahahahha kabla ya kufahamu ni kiasi gani kimechangwa at least watuambie hizo ambazo wanasema wanazo watueleze zimefanya kazi gani so far...., then ndio tuje kwenye kutajiana majina na amount. Hii serikali ya CCM sijui hii laana ya wizi nani kawaachia. sijui kwa kweli
Laana itawatafuna maisha.yao yote
 
Back
Top Bottom