Sh4.2bn earthquake relief cash ‘lying idle’

Sh4.2bn earthquake relief cash ‘lying idle’

Serikali isidhulumu hata senti moja ya pesa za wahanga. Watuwekee list ya wote waliochangia ili tuthibitishe ukweli wa kauli yao kwamba pesa zilizochangwa ni 5.4 billion tu kitu ambacho hakina ukweli wowote.
hii serikali mi imenishinda jamani, hadi hela za wahanga zinaliwa tena wazi wazi, mi sijawah ona
 
mafisadi warudishe hela zetu..
tuliwachangia ndugu zetu na si vinginevyo..
ivi mbaya ni nani..
kati ya yule aliyetaka kuchangisha ili ziwafikie wahanga kwa haraka akatumbuliwa?
na huyu aliyechangisha akatokomea nazo kusikojuilikana ?
Mbaya ni aliyechangisha akatokomea nazo.
 
Huu ni uongo wa hali ya juu. Uingereza pekee yake imetoa shilingi 6.7 billion kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi iweje Serikali iseme zimekusanywa bilioni 5 tu!? List ya wachangiaji wote na kiasi walichochanga iwekwe hadharani mara moja ili kama kuna wizi umefanywa katika pesa hizi basi hao wezi wanaanikwe hadharani kwa kuiba pesa za wahanga wa tetemeko.
Mkuu hutakiwi kuziita pesa, sema rambirambi kabisa tena kwa herufi kubwa ili kila mtu ajue kwamba rambirambi za wahanga wa tetemeko kagera hazijawafikia wahusika.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi yule RAS tuliyeambiwa kuwa alifungua akaunti binafsi ili achote fedha za maafa ameishia wapi. Ama alionekana kuwa kikwazo kwa mipango yao ya udhalimu wakaamua kumtengenezea zengwe la kumuondoa...
 
Magufuli is a country bumpkin.

Ivi Jamani ukiLIKE huu ujumbe apo juu si utaitwa pia ni mchochezo??? Yani Kiranga you have made my day pia nimeLIKE (Bumpkin -- == -- Pumpkin) nikiitwa kisutu kwa kosa la kushabikia uchochezi natmai nitawashinda tu
 
Hivi ile mahakama ya mafisadi ilishaanzishwa?
 
kama tulivyosema sisi kina gogo la shamba miaka hii mitano itakwisha kwa kuona na kusikia mengi ya ajabu hasa kutoka kwa watu tuliokuwa tunawategemea kutuletea maendeleo
 
Mgawo wa misaada tetemeko watikisa
www.ippmedia.com/sw/habari/mgawo-wa-misaada-tetemeko-watikisa

Hali hiyo imejitokeza baada ya Serikali mkoani Kagera kutangaza kuwa sehemu kubwa ya fedha zilizopatikana kutoka katika michango ya watu na taasisi mbalimbali zitaelekezwa zaidi katika kujenga miundombinu kama ya barabara, tangazo lililoibua mjadala mkali huku baadhi ya watu wakipinga uamuzi huo na kutaka fedha hizo zielekezwe moja kwa moja kwa wananchi walioathirika kwa kuharibiwa makazi yao na mali mbalimbali kiasi cha kuwalazimu maelfu miongoni mwao kuendelea kulala nje.

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa kipimo cha ‘ritcher scale’ 5.9 lilitokea saa 9:30 alasiri ya Septemba 10, mwaka huu na kuathiri maeneo kadhaa ya mikoa ya kanda ya ziwa, hasa mkoani Kagera.

Mbali na kuharibiwa kwa miundombinu, watu 17 walifariki dunia, wengine 560 wakajeruhiwa huku nyumba kadhaa zikiharibiwa vibaya.

Akaunti malumu kwa ajili ya tetemeko ilifunguliwa, huku hamasa kubwa ikitolewa kwa kila mmoja kuchangia ili kuwafariji waathirika ambao wengi wao walijikuta wakipatwa na umaskini usiotarajiwa baada ya kupoteza mali na makazi.

Jana, wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ikijitosa jumla kwenye suala hilo na kutoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha hizo za misaada ili kuondoa kile ilichokiita upotoshaji juu ya matumizi ya michango kwa wathirika, wabunge wa chama tawala (CCM) na wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) watokao mkoani Kagera walitangaza kuitana kwa dharura ili kujadili kwa kina suala hilo.

Vyama vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na NLD.

Akizungumza na Nipashe jana, Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CCM), Rwegasira Mukasa, alisema yeye na wenzake wamechanganywa na taarifa ya Serikali na hivyo wameamua kuitana ili kulijadili suala hilo na kuamua nini cha kufanya.

Alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kuwa wapiga kura wao wangali wakitaabika kutokana na hali ngumu inayowakabili na tumaini lao kuu lilikuwa ni pamoja na kupata mgawo wa misaada hiyo ili kuwapunguzia makali ya maisha.

"Ndani ya siku tatu, nne wabunge wote wa mkoa wa Kagera tutakutana na kutoka na kauli moja," alisema Mukasa.

“Pale msaada unapotolewa kwa waathiriwa, wapo wanaoguswa na mwathiriwa moja kwa moja… aliyemuona analala nje, na si kupeleka msaada katika kituo cha afya au elimu.

“Tunajiandaa na kikao ambacho ni cha dharura. Wabunge wote wa Kagera tutajadili suala hili maana (suala) hili lilitokea wakati tukiwa bungeni na hatukupata muda wa kulijadili kwa sababu kulikuwa na misiba."

Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare, akizungumza suala hilo jana, alisema Serikali kuelekeza fedha za msaada za waathiriwa wa tetemeko kwenye miradi ya maendeleo kunaonyesha namna inavyoshindwa kuandaa bajeti ya kitengo cha maafa kusaidia wanaokumbwa na maafa.

Alisema hatua hiyo inaweza kuwakatisha tamaa baadhi ya wachangiaji na kwamba tatizo lililopo ni udhaifu katika usimamizi wa fedha.

“Hakuna chanzo chenye fedha kwa ajili ya waathiriwa wa maafa yanayotokea, licha ya masuala kama haya kutokea ghafla. Tunayashuhudia miaka mingi, Serikali imeonekana kuwatumia waathiriwa ili kufanikisha miradi yake,” alisema Lwakatare.

OFISI YA WAZIRI MKUU YAJITOSA
Katika taarifa yake ilitolewa kwa vyombo vya habari jana, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge, Uledi Mussa, alidai kumekuwa na upotoshaji kuhusu hatua zinazochukuliwa ilhali serikali kwa kushirikiana na wadau imesaidia waathirika kwa kutoa matibabu bure kwa majeruhi wote 560 na kuandaa na kugharimia mazishi ya watu 17 waliofariki dunia na kutoa mkono wa pole wa Sh. milioni 1.8 kwa familia zilizopatwa na msiba.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa tathmini za wataalamu na makadirio ya awali yanabainisha takribani Sh. bilioni 104.9 zinahitajika kurejesha hali ya mkoa wa Kagera kufuatia maafa hayo.

Ilieleza kuwa kiasi hicho cha fedha kitatumika katika ujenzi wa makazi ya muda kwa awaathirika wa nyumba 16,667 ambazo zitagharimu Sh. bilioni 41.7.

Mchanganuo huo unaonyedsha zaidi kuwa Sh. bilioni 1.92 ni kwa ajili ya kodi ya miezi sita kwa wapangaji waliotoka kwenye nyumba zilizoharibika, ukarabati wa shule za msingi 153 ambao utagharimu Sh. bilioni 12.7 na za sekondari 57 ambazo zinahitaji Sh. bilioni 45.66,

Aidha, vituo vya afya na zahanati 32 zitagharimu Sh. milioni 772 na pia majengo ya taasisi 20 ambazo zinahitajika Sh. bilioni 1.3.

MICHANGO YA WADAU
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa fedha taslimu zilizokusanywa kupitia benki ni Sh. bilioni 5.413, Sh. milioni 17.579 zimepokewa kupitia mitandao ya simu, ahadi ni Sh. bilioni 6.703, hivyo jumla ya ahadi na fedha taslimu hadi kufikia Novemba 13 ni Sh. bilioni 12.134.

"Serikali imepokea misaada mingine yenye thamani ya Sh. bilioni 2.25; unga tani 58.12, sukari mifuko 1,150, mchele tani 133.98, maharage tani 19.666, mahindi tani 70.1, majani ya chai tani tatu, maji katoni 1,570, mafuta lita 6,022, sabuni katoni 443, shuka 495, blanketi 6,125, vuandarua 1,821, magodoro 1,146, mahema 367 na turubai 6,237," ilifafanua zaidi taarifa hiyo.

Katibu Mkuu huyo, katika taarifa yake hiyo, alieleza kuwa baadhi ya wadau ikiwamo serikali ya Uingereza imeahidi kutekeleza ahadi zao moja kwa moja katika ujenzi wa shule mara baada ya Wakala wa Majengo (TBA) kuanisha viwango na gharama.

Aidha, alieleza kuwa tangu kutokea kwa maafa hadi Novemba 13, Serikali imetumia Sh. milioni 969.238, mifuko ya saruji 17,423, bati 5,348 na misumari kilo 1,107 kufanya ukarabati mkubwa na mdogo katika shule za msingi na sekondari pamoja na ukarabati wa zahanati katika halmashauri za mkoa wa Kagera.

Alisema kuwa ingawa haijafikia lengo la Sh. bilioni 104.9 zinazohitajika kurejesha hali ya mkoa mzima, serikali itaendelea kutumia kwa uadilifu na uwazi kwa faida ya waathirika wenyewe.

WAPEWA MABATI
Katika hatua nyingine, mpango wa kutoa misaada kwa wananchi ambao waliathiriwa na tetemeko hilo umeanza kufanyiwa utekelezaji kwa kutoka mabati 20 kila kaya na mifuko ya saruji mitano kwa makundi ya wasiyojiweza katika wilaya sita za mkoa huo.

Katika kutekeleza mpango huo, Kamati ya Maafa imeanza na kundi la wazee, walemavu, wajane na watu wasiojiweza kiuchumi.
Awali Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mtaafu Saalim Kijuu, alisema kuwa vifaa vya ujenzi kwa makundi hayo utafanyika kwenye wilaya za Muleba, Misesenyi, Karagwe, Bukoba na Bukoba Vijijini.

Alisema hatua ya awali imehusisha kaya 200 ambazo utekelezaji wake umeanza kwa kuwagawia wazee wa kata ya Kashai mtaa wa Rwome na kata Nyakato katika kijiji cha Ibosa kwa kuwakabidhi mifuko ya saruji na mabati matano.

WAATHIRIKA WALONGA
Aneth Kiiza, mkazi wa Mtaa wa Rwome, Kata ya Kashai, akizungunza na Nipashe kwa niaba ya mama yake, Imelda Kiiza (95), aliwashukuru viongozi waliopita kutoa msaada huo kwa kuwa nyumba aliyokuwa akiishi ilianguka na kukosa mahali pa kuishi kwa kipindi chote tangu kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi.

Kiiza alisema misaada aliyopewa mama yake, itasaidia kupata walau chumba kimoja cha kuishi.

Khafisa Khamis (75), mkazi wa kijiji cha Ibosa, Kata ya Nyakato, ni mjane anayeishi kwenye nyumba ambayo ina nyufa kila kona. Katika mazungumzo na gazeti hili jana, aliishukuru serikali kumpatia mifuko mitano ya saruji na mabati 20.

"Hapa nilipo naishi peke yangu sina watoto, nina mjukuu mmoja ambaye naye anaishi mbali nami na hana uwezo kabisa kifedha," alisema.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Vedasto Mayengo, alisema msaada unaotolewa na mkoa hautoshelezi kwa wananchi kulingana na mahitaji ya wananchi hasa wanaopambana kurejesha makazi yao yaliyoharibiwa na tetemeko.

Alisema wananchi wanapoona misaada inapelekwa kwa baadhi ya kaya, wamekuwa wakielekeza lawama zao kwa viongozi wa ngazi ya kata na vijiji kwa "kutokumbuka kwa michango iliyotolewa kwa ajili ya kusaidia waathirika."

*Imeandikwa na Restuta Damian (BUKOBA) na Christina Mwakangale (DAR)

Bujibuji, angalia zile kelele zetu humu zilikofikia. YES WE CAN!
 
Back
Top Bottom