Sh1.2 bilioni zakarabati hospitali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sh1.2 bilioni zakarabati hospitali

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by sumasuma, Feb 8, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Gasper Andrew, Singida
  HOSPITALI Teule ya Wilaya ya Singida ya Makiungu, imetumia zaidi ya Sh1.2 bilioni kugharimia ujenzi wa hosteli ya kisasa na upanuzi wa wodi ya wazazi. Hayo yalielezwa juzi na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Maria Borda, wakati akitoa taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone, muda mfupi baada ya mkuu huyo kuyafungua majengo hayo.

  Alisema Sh529.2 milioni zilitumika katika upanuzi na ukarabati wa wodi ya wazazi, lengo likiwa ni kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka siku hadi siku. Dk Borda alisema, wamekuwa wakitoa elimu kwa wajawazito juu ya uzazi salama na hatua hiyo imesababisha ongezeko kubwa la wanawake hao kukimbilia kujifungua hospitalini hapo.

  “Hali hii imesababisha msongamano mkubwa wa wajawazito katika wodi iliyopo, hivyo wengi wao hulazimika kutandika magodoro sakafuni kwa kukosa vitanda. Hali hii imesababisha hitaji la kukarabati na kupanua zaidi wodi ya wazazi ambao wanatibiwa bure", alisema.

  Aidha, mganga huyo alisema wametumia Sh682.8 milioni kugharimia ujenzi wa hosteli ya kisasa ya ghorofa mbili, kwa ajili ya watumishi na wageni mbalimbali, wanaotembelea hospitali hiyo. “Mradi huu wa hosteli ulibuniwa kutokana uhaba mkubwa wa nyumba za kuishi watumishi wa kada za juu pamoja na wataalamu wengi wa kujitolea, wanaokuja kila mwaka kusaidia katika fani mbalimbali”, alifafanua Dk Borda.

  Dk Borda alitumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wafadhili waliosaidia kufanikisha ujenzi huo ambao ni Maltesa Mission Fund na Cork,Singida Partinership kwa upande wa hosteli.Pia Shirika la Cordaid kupitia Stichting Makiungu la nchini Holland, Maltese Mission fund na Ubalozi wa Nigeria nchini kwa upande wa upanuzi na ukarabati wa wodi ya wazazi. Hospitali ya Makiungu ilianzishwa mwaka 1954 na masista wa Kanisa la Katoliki kwa sasa inaendeshwa kwa ubia na Halmashauri ya Wilaya ya Singida.:A S 465:
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Sumasuma, shauri lako, Habari kama hizi hazitakiwi humu, wataanza kusema katoliki wanapendelewa!!!!!!! Mgogoro wa MoU na District designated hospitals na serikali haujaisha wewe unaleta tena habari kutonesha vidonda.!!!!
   
 3. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nyingi au kidogo??? ujumbe ni nini unataka toa
   
Loading...