Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha!

mkuu nakubaliana NA mtoa mada elfu 5000,ni kubwa sana, MM japo sikua serious nilinunua kifaranga cha mtetea ambacho hakijaanza kutaga(huwa napendaga sana kuku) nikawa nakifuga home chakuka kilikua mabaki ya msosi home ambayo yalikua yanatosha kikuku kimoja kilivyo zoea nikawanakiachia nje mtaani jioni kinarudi,miezi ikapita kikawa kinataga jogoo alipata huko huko mtaani, nikajastuka simuoni kumtafuta nikakuta kamejificha kanatamia, nikawa sina uhakika wa mayai coz jogoo sikuwa nalo,baada ya mda kaja na vifaranga nane nikashangaa na kufurahi pia, hapo nikaenda tandale pumba ndoo 1 sh 2000 nikavitunza saiv wapo wengi sana home. Nauza mayai tuu nayawekaga dukani kwa bi mkubwa, trey 15000 ni reja reja. Saivi. nipo mbali nipo chuo Ila naambiwa wapo vizuri coz nilishawajengea kibanda.
 
ndyoko huo ni uwongo
sukari robo kwa lita 5???hata ukitumia kk(kimoja kimoja)haikolei
unaijua KK au unakurupuka amu au ndo unachangia.KK ni kiboko maana vijiko 5 vya ubwabwa vinakoleza maji lita30 ni kiboko ya chumvi..
 
Last edited by a moderator:
Kuna mtu amependekeza kuanza biashara kwa sh 5000, kama kawaida waungawana humu jf wamedai apeleke huo uzi wake joke forum. Lakini mie nna mtazamo tofauti hapa. Kwamba bado hiyo elfu tano inaweza kukutoa kabisa kama kweli uko serious. kwa namna gani inaweza kukutoa, hebu fuatilia hapa chini:

Nimeamua kufanya biashara ya kuuza juisi ya matunda.

Mananasi 2 sh 2000
Parachichi 2, sh 1500
Sukari robo 1000
Jumla 4,500

Baada ya kuitengeneza zitatoka walau lita tano, ambazo kwa kiwango cha chini, ntapata jumla ya glass zisizopungua 15. Kwa bei ya gsh 500 kwa glass moja, ikiisha ntapata jumla ya sh 7500.

Kumbuka hapo nimemaliza chuo, bado mie ni mtu wa kula kulala-yaani nakaa geto. Nimeshatengeneza faida ya shi 3000, kwa siku. Hii ina maana kama ni ajira basi nalipwa 90,000 kwa mwezi. Hivi ntalala njaa kweli nikiamua kuwa serious na hii bishara?

Hivi kwa hesabu ndogo kama hii, kuna haja kweli ya mtu kulia njaa jamani. Mi nadhani kinachotusumbua wengi ni kale katabia kwamba hiyo kazi ni ya kufanywa na mtu ambaye hana shule, lakini hela haina shule, na sioni kama hapo kuna kudhalilika kwa aina yeyote. Jamani, let us start from the scratch kama hatuna mbadala wa aina yeyote ktk ajira zetu.

Tanzania hii kila kitu kinawezekana, sio ufisadi pekee tu!

Ni kweli kabisa inatosha!! Mimi ni mwanafunzi wa chuo flan hapa dsm!! Me nilianza na mtaji wa 14000/= hivi sasa nalaza kwa cku faida kama 10000/= hapo nimeshatoa gharama za msosi kila kitu!!

UKIJITUMA INAWEZEKANA!!!
 
haya mimi nataka nitoke kwa tsh. 5,000/=. mchanganuo ni kama ifuatavyo.

Nitafanya biashara ya mchicha na spinach/chinees. nitaziuza kilimahewa stend eneo ambalo wengi wanashuka kwa kasi. Kwa biashara hii, nitakuwa naenda kuchukua bidhaa yangu kwa mkulima moja kwa moja.
1. Chinees 15 kwa sh. 200/- bei ya jumla. nitoa fungu 3 kila moja ikiwa na chinees 5. nitauza kwa tsh 200/- kwa fungu moja nitatengeneza 400 faida. faida itazidi mtaji.

kwa hiyo ukichukua 5,000/200= 25.
fungu 25 za jumla zitaleta fungu 25*3=75
75*200=15,000/=

kwa mapato hayo kwa siku, natengeneza 10,000 kama faida. kwa mwezi 300,000/= nadhani kula, kupanga chumba na sebule nitaweza. baada ya miaka miwili nanunu kiwanja na kujenga chumba kimoja kwanza, nahamia kwangu

Hapo kwenye nyumba ndo utakapofilisikia. Kuza mtaji nyumba yako ya kuishi itokane na faida ya biashara.
 
Sh. 5000 ni mtaji tosha wa kipesa.

Kumbuka sehemu ya mitaji mingine utaipata hapo home.

Kwa mfano jana, nimekutana na kijana anauza karanga za kukaanga, ninamfahamu akaniambia amechoka kukaa kijiweni. Basi, nilikuwa nimesimama barabarani karibu na kwangu , nikanunua za Sh. 500, jamaa yangu mmoja akapita akamnunulia mkewe za sh. 300. Unaona, ghafla akawa ameshauza kwetu na lakini ameshauza kwa wengine.

Mambo yanawezekana, tatizo la watanzania ni visingizio. Hizo post nyingi ni visingizio, blenda zipo nyingi , hata nyumbani anapokaa, kama hakuna unaweza ukapata kwa jirani au ukatumia njia mbadala, kwani blenda zilikuwepo miaka yote.

Unaweza kupika vitafunio, kwa mfano kwa sh. 5000 inatosha, kupika kalimati na nyumbani wanapika kila siku kwa mtaji huo.

Wengine, wanasema itakuchukua muda mrefu, swala si muda ila, unahitaji nia ambayo ndio mtaji mkubwa. Eti wengine wanasema, labda ingekuwa dollar 5000 ya USA, unafikiri mambo ni rahisi kwa vile una hela nyingi, waulize waliofilisika biashara za maduka ya nguo kariakoo.

Unachohitaji ni wazo, nia isiyoyumba na wapi unataka ufike hakika utafika.

Mi nakubaliana kabisa na ww, achen kukatishana tamaa jaman cha msingi nikutoa option ya kufanya kitu kingne ambacho kina uhitaj mdogo wa vitendea kazi out from hyo yenye gharama kubwa from ze same amount of money
 
... Tuache visingizio jamani. We uko radhi utumie laki moja kula nyama choma na bia badala ya kuanzisha kibanda kidogo cha juisi. Kama unaogopa kuuza wewe mwenyewe, weka kijana akuuzie hizo juisi basi.

"Jana nimetumia zaidi ya laki unusu. Leo hadi sasa saa10 na dk 10 nishatumia laki na elfu themanini. Usiulize mapato yangu maana haviendani. Nakula akiba!"

Mkuu, hapo nawakilisha jamii pana ya 'wasomi' wenye ajira zao za kudumu. Hivi angeamua kuajiri hata nduguye asiye na kazi kwa mtaji huo wa laki 3, miaka 10 ijayo angekua wapi? WaTz wanahitaji upako wa kijasiriamali. Wengi wataendelea kuhadithia tu utajiri 'wetu' ilhali hata wao wangeweza kuwa upande huu.

Kuna chalii mmoja alikua anauza bidhaa za umeme kimachinga. Kakua hadi kuwa na kiduka uchwara. Kakua hadi anasafiri kwenda China. Kiduka kimekua japo muuzaji ye mwenyewe akisafiri anafunga.

Majuzi ananiomba ushauri eti anataka kununua Verossa. Nimemwambia aache huo ujinga. Gari litamgharimu sana. Hakuniskia. Kajitutumua kanunua subaru Forrester. Si unajua watoto wa Arusha wanavozipenda!

Hapa namuhesabia kufilisika kwake. Na nitainunua hiyo gari kwa chee maana anavyoitunza! Halafu nitaiuza cha juu kumuumiza roho ajifunze vipaumbele. Navyoandika, naye keshajiunga na kundi linaloilalamikia Januari utadhani hakujua inakuja!!

Bottom line. 5000 inatosha kwa mwenye ujasiri wa amali. Mitaji mingine ni kama ujuzi, mtandao wa wateja/watu, uaminifu, kauli tamu, n.k.
 
Naona Vipofu Mnaongozana kuvuka Barabara!
Hapo Bado Hujasolv Tatizo La Barafu,
Vitendea Kazi
Mgambo
n.k
Sio Rahis Kama Mnavyozani

Jigo, vitu vingine mali kauli. Mtaji huo wa 5000 ni wa hela. Upungufu mwingine tumia mbinu za kuzaliwa kuvipata au azima. Barafu tafuta jirani mwenye friza, ugandishe kwa ahadi ya kumlipa kitu kidogo biashara ikianza. Na hivi luku ghali, wengi hawakatai.
 
Back
Top Bottom